Ubepari ni mfumo wa uchumi ambamo biashara, viwanda na vitegauchumi vingine vinatawaliwa na watu binafsi kwa kiasi kikubwa na kwa lengo la kupata faida.
Nafasi ya serikali ni ndogo. Vilevile lengo la kuhudumia jamii katika mahitaji yake haliongozi mipango.
Kati ya sifa za ubepari kuna ulimbikizaji wa mtaji, ushindani katika soko huria na kazi zinazolipwa mshahara.
Katika mfumo huo, pande zinazokabiliana zinapanga zenyewe bei kwa makubaliano, bila kuingiliwa na mamlaka yoyote ya nje.
Ubepari una viwango tofauti vya uhuru huo, kadiri ya nchi:Kiingereza kinaainisha laissez-faire capitalism, welfare capitalism, crony capitalism na state capitalism.
Kihistoria, ubepari uliwahi kuwepo tangu zamani kwa namna mbalimbali, lakini ulianza kutawala baada ya mifumo ya Karne za Kati za Ulaya kupitwa na wakati na mapinduzi ya viwanda kushika kasi. Ubeberu, ukoloni, halafu utandawazi vimefanya ubepari uenee duniani kote.
Katika karne ya 20 ubepari ulishindana na mfumo mbadala wa ukomunisti ambao ulitia mkazo juu ya majukumu ya serikali katika uchumi mpaka kuwanyima wananchi nafasi ya kuwajibika. Hata hivyo, baada ya kushinda, ubepari pia umeingiza uchumi wa dunia katika hali tete, kama ilivyojitokeza mwanzoni mwa karne ya 21.
Watetezi wa ubepari wanasisitiza kwamba mfumo huo unaleta ustawi wa jamii ulio mkubwa kuliko ule unaoletwa na mifumo mingine yoyote, kiasi kwamba hatimaye wote wanafaidika, si matajiri tu. Critics of capitalism variously associate it with economic instability,
Wengi wanapinga hoja hiyo kwa kuonyesha umati unaokosa kazi na huduma za msingi kutokana na pesa kutiwa maanani kuliko binadamu na mazingira kutumika kuliko uwezo wake wa kustahimili.. Kanisa Katoliki limejitokeza kwa namna ya pekee kati ya dini mbalimbali kukosoa ubepari kama ulivyokosoa na hatimaye kuangusha ukomunisti wa Ulaya Mashariki (1989) likiongozwa na Papa Yohane Paulo II.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ubepari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ubepari, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.