C

C ni herufi ya tatu katika alfabeti ya Kilatini.

Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

Katika matumizi ya Kiswahili kwa kawaida inatokea tu pamoja na "h" kuwa "ch". C peke yake si kawaida katika maneno ya Kiswahili isipokuwa katika majina ya kigeni.

Herufi C kwa maandishi mbalimbai
Herufi C kwa maandishi mbalimbai

Maana za C

Historia ya herufi "C"

Kiebrania
gimel
Kifinisia
gimel
Kigiriki
Gamma
Kiitalia
cha awali: C
Kilatini
C
ג C  C  C  C 

Asili ya herufi C ni pamoja na G katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na gimel iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya ngamia wakitumia alama tu kwa sauti ya "g" na kuiita kwa neno lao kwa ngamia "gimel". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "gamma" bila kujali maana asilia ya "ngamia" ilikuwa sauti tu ya "g".

Waitalia ya kwanza hawakuwa na sauti ya "g" wakatumia alama kwa aina ya "k". Waroma wakaipokea hivyo lakini walikuwa na sauti ya "g" hivyo mwanzoni walitumia "C" kwa sauti zote mbili. Baadaye waliona vema kutofautisha kati ya sauti za "k" na "g" wakaongeza mstari kwenye C kuifanya G. "C" ikabaki kwao kwa kuandika sauti ya "k". Lakini katika lugha ya Kilatini matumizi ya awali bado hukumbkwa katika kifupi cha jina "Gaius" linalofupishwa kwa kuandika "C.".

Tags:

Alfabeti ya KilatiniKiswahili

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UfisadiWadatogaOrodha ya nchi za AfrikaVitenzi vishirikishi vikamilifuSerikaliWachaggaUfugaji wa kukuUkristo barani AfrikaKatekisimu ya Kanisa KatolikiRwandaVivumishi vya ambaWayahudiMkutano wa Berlin wa 1885Kamusi ya Kiswahili sanifuUenezi wa KiswahiliMburahatiTanganyika (ziwa)Alama ya barabaraniTanzaniaMuunganoNdoaUzalendoMaarifaMitume na Manabii katika UislamuKisaweJohn Raphael BoccoHifadhi ya mazingiraVidonge vya majiraNominoWakingaMagonjwa ya machoBenjamin MkapaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziOrodha ya Marais wa TanzaniaYombo VitukaLenziUmoja wa AfrikaYoung Africans S.C.Dodoma MakuluBahashaTiktokNgiriEe Mungu Nguvu YetuNgeliAfyaUtamaduniOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMavaziMichezoUchawiUfupishoUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaSheriaUzazi wa mpangoVirusi vya UKIMWIUislamuCristiano RonaldoHifadhi ya Taifa ya NyerereOrodha ya milima ya TanzaniaTashihisiHistoria ya KanisaMazungumzoMkoa wa DodomaSeli nyeupe za damuMsituWhatsAppHali ya hewaSentensiPaul Makonda🡆 More