W

W ni herufi ya 23 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa.

Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

Asili yake ni ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

Maana za W

Historia ya alama W

Historia ya W ina asili za pamoja na U, V, Y na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.

W  W  W  W  W  W 
Kisemiti asilia:
picha ya kingoe
Kifinisia:
Waw
Kigiriki:
ipsilon
Kietruski:
V
Kilatini:
V
Kilatini Kipya:
W

Alama ya W kiasili haikupatikana katika Kilatini cha Kale. Waroma hawakutamka "w" tofauti na "v". Matumizi yake ilikubaliwa wakati wa Kilatini Kipya katika karne ya 16. Wakati ule Kilatini lilikuwa lugha ya kitaalamu ya mataifa ya Ulaya penye wasemaji wengi wa lugha za Kigermanik zilizokuwa na sauti hii lakini iliandikwa kwa kutumia V. Wakati ule wataalamu wa Ulaya walikubaliana kutumia alama ya V mara mbili kwa kuonyesha sauti ile ya w.

Kwa hiyo historia yake ni sawa na V: Waroma walipokea alama hii kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma (tazama F) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "u" lakini pia "v" kama ilikuwa mwanzoni wa neno. Waroma walipokea vile.

Katika lugha za Ulaya zinazotumia alfabeti ya Kilatini kuna lugha kadhaa zisizo na W kwa sababu hawaihitaji. Katika Kijerumani W hutumiwa kwa sauti ya "V" ya Kiswahili. Kiingezera hutamka kama Kiswahili.

Tags:

Alfabeti ya KigirikiAlfabeti ya KilatiniIpsilonKiswahili

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

IsimujamiiUkooWikipediaMkoa wa KageraMjusi-kafiriOrodha ya Watakatifu wa AfrikaImaniNg'ombeOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuWapareDesturiMapachaBarua pepeLigi ya Mabingwa UlayaLatitudoKanisaLeopold II wa UbelgijiVivumishi vya idadiStephane Aziz KiChuraMadhehebuMbwa-mwitu DhahabuOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMbuInsha za hojaMweziMkoa wa KataviMsituBungeMnururishoRitifaaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUtoaji mimbaKishazi tegemeziMagimbiKylian MbappéHoma ya iniAgano JipyaUainishaji wa kisayansiAngahewaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaUgonjwa wa kuharaMamlaka ya Mapato ya TanzaniaMuundoOrodha ya visiwa vya TanzaniaFonetikiMkuu wa wilayaMazingiraDawa za mfadhaikoFilomena wa RomaAlama ya uakifishajiMoshi (mji)MalariaMarie AntoinetteJiografia ya TanzaniaRoho MtakatifuMtaalaVivumishiMbooVokaliOrodha ya miji ya TanzaniaMarekaniNikki wa PiliVivumishi vya jina kwa jinaMakabila ya IsraeliHoma ya mafuaTungoJacob StephenVivumishi vya kumilikiMkoa wa ArushaMaambukizi ya njia za mkojoTendo la ndoaMmeaMajigamboTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaWayahudi🡆 More