Homanyongo C

Kwa ugonjwa tofauti ambao wakati mwingine jina lake linachanganywa tazama Homa ya manjano

Homa ya nyongo C (Hepatitis C)
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B17.1, B18.2
ICD-9070.70,070.4, 070.5
OMIM609532
DiseasesDB5783
MedlinePlus000284
eMedicinemed/993 ped/979
MeSHD006526

Homa ya nyongo C (pia homanyongo C, kwa Kiingereza Hepatitis C) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoshambulia zaidi ini.

Virusi vya Homanyongo C ndivyo vinavyosababisha ugonjwa huu wa ini.

Kwa kawaida Homa ya nyongo C haionyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali, lakini ugonjwa ukiendelea unaweza ukasababisha makovu katika maini, na baada ya miaka mingi ini linapata vidonda (cirrhosis). Kwa wagonjwa wengine vidonda hivi vinaweza kusababisha ini kukosa kufanya kazi, saratani ya ini, au mishipa iliyovimba sana ya umio na tumbo, ambayo yanaweza kufanya mtu avuje damu hadi kufa.

Watu wanaambukizwa virusi vya Homa ya nyongo C kwa kupitia mkondo wa damu kwa njia ya kujidunga sindano za dawa za kulevya, kutumia vifaa vichafu vya hospitali, na kuongezewa damu.

Kadri ya watu milioni 130–170 wameathirika na Homa ya nyongo C. Wataalamu walianza kuchunguza HCV katika miaka ya 1970, na walithibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo mnamo mwaka 1989. Haijulikani kama ugonjwa huu unawaambukiza wanyama.

Peginterferon na ribavirin ndizo dawa pekee zinazotumika sana dhidi ya HCV. Kati ya wagonjwa asilimia 50-80 wanaotibiwa huwa wanapona. Watu wanaopata uharibifu mkubwa na kovu kwa ini (cirrhosis) au saratani ya ini wanaweza kuhitaji ini la kupandikizwa, lakini virusi huwa vinarejea baada ya kupandikiza. hakuna chanjo ya kuzuia Homa ya nyongo C.

Viashiria na dalili

Homa ya nyongo C inasababisha dalili katika wagonjwa asilimia 15 tu, mara nyingi zaidi agonjwa hawaonyeshi dalili zozote.

Dalili ni kama zifuatazo: kupungua hamu ya kula, uchovu, kichefuchefu, maumivu ya viungo au misuli, kupungua uzito wa mwili. Ni wagonjwa wachache ambao ni mahtuti na wanapata homa ya manjano.

Kadri ya wagonjwa asilimia 10 hadi 50 wanapona bila kupata matibabu, na kati ya hao wengi ni wasichana wadogo.

Uambukizo sugu

Asilimia themanini ya watu walioambukizwa virusi wanapata madhara ya uambukizo sugu. Wagonjwa wengi hawaonyeshi dalili zozote kwenye hatua za awali za ugonjwa huo, ingawa uambukizo sugu wa Homa ya nyongo C unasababisha uchovu. Homa ya nyongo C ni chanzo kikubwa cha ini kupata vidonda pamoja na saratani ya ini kwa watu ambao wameathirika na ugonjwa huu kwa muda mrefu. Kati ya asilimia 10–30 ya watu wameambukizwa baada ya miaka 30 ya kuwa na vidonda katika ini. Pia watu wenye HomanyongoB au UKIMWI, walevi sugu, na wanaumme huwa wanapata vidonda katika ini. Kwa watu wenye vidonda katika ini uwezekano wa kupata saratani ya ini ni mara ishirini zaidi ya kawaida, kiasi cha asilimia 1 hadi 3 kwa mwaka. Kwa walevi sugu, uwezekano wa kupata ugonjwa ni mara 100 zaidi ya kawaida. Homa ya nyongo C inasababisha vidonda vya ini katika asilimia 27 ya wagonjwa na inasababisha saratani ya ini kati ya asilimia 25 ya wagonjwa.

Vidonda vya ini vinaweza kusababisha msukumo mkubwa wa damu katika mishipa iliyoungana na ini, kujaa maji tumboni, kuumia kirahisi au kuvuja damu, mishipa kuvimba, hasa tumboni na kwenye umio, homa ya nyongo (ngozi inakuwa ya manjano), na majeraha katika ubongo.

Athari nje ya ini

Homa ya nyongo C mara chache inasababisha ugonjwa unaojulikana kama Sjögren's syndrome (madhara dhidi ya kinga ya mwili), upungufu sio kawaida wa idadi ya blood platelets, magonjwa sugu ya ngozi, kisukari, pamoja na aina Fulani ya aina saratani ya damu iitwayo non-Hodgkin lymphomas.

Chanzo

Virusi vya Homa ya nyongo C ni vidogo, vilivyo ndani ya kibahasha, na kiuzi kimoja, vina RNA yenye virusi. Ni jamii ya hepacivirus ya familia iitwayo Flaviviridae. Kuna aina saba muhimu za genotypes of HCV. Nchini Marekani, genotype 1 inasababisha asilimia 70 ya magonjwa, genotype 2 inasababisha asilimia 20 ya magonjwa, na kila aina ya genotypes zingine zinasababisha asilimia 1. Genotype 1 ndio inayojulikana zaidi katika nchi za Amerika ya Kusini na Ulaya.

Maambukizi

Njia ya kawaida ya uambukizaji katika nchi zilizoendelea ni kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano. Katika nchi zinazoendelea njia za kawaida za utoaji damu na utaratibu usio salama wa kimatibabu Katika asilimia 20% ya wagonjwa, chanzo cha uambukizaji hakijulikani; lakini vyanzo vingi vinaweza kuwa ni matumizi ya dawa ya kulevya kwa kujidunga sindano.

Madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano

Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano ndiyo sababu kubwa ya kusambaza Homa ya nyongo C katika nchi nyingi duniani. Uchunguzi uliofanya katika nchi 77 zimeonyesha kwamba katika nchi 25 ambayo Marekani ni mojawapo, asilimia ya watu wanaopata Homa ya nyongo C kwa kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano ni asilimia 60 hadi 80 na Uchina. Nchi kumi na mbili zina zaidi ya asilimia 80. Zaidi ya milioni kumi ya watumizi wa madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wameambukizwa na Homa ya nyongo C; Uchina (milioni 1.6), Marekani (milioni 1.5), na Urusi(milioni 1.3) jumla ya wagonjwa walioambukizwa ni wengi sana. Kiasi kikubwa cha wafungwa Marekani wana Homa ya nyongo C uwezekano wa kupata ugonjwa ni mara kumi hadi ishirini zaidi ya kiwango cha kawaida cha idadi ya watu, na utafiti umeonyesha hii inasababishwa na tabia za hatari za kutumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano au kujichora chale na sindano ambazo sio safi.

Maambukizi kupitia huduma za afya

Utoaji wa damu, mazao ya damu, na upandikizi wa viungo vya mwili bila kuchunguza HCV ndizo zinazoleta matatizo makubwa ya uambukizaji. Marekani ilirasimisha uchunguzi mnamo mwaka 1992. "Tangu wakati huo kiwango cha maambukizi imepungua kuanzia kati ya mmoja kati ya 200 kwa kila kipimo cha damu hadi moja kati ya 10,000 mpaka 10,000,000 kwa kila kipimo cha damu. Kuna upungufu wa maambukizi kwa sababu kuna kipindi cha siku 11 hadi 70 ambazo ni siku ambazo mtoaji damu mtarajiwa anayepata Homa ya nyongo C na damu yao kuonyesha kwamba imeambukizwa. Nchi zingine bado hazifanyi uchunguzi wa Homa ya nyongo C kwa sababu ya gharama.

Mtu mwenye jeraha la sindano kutoka kwa mtu aliyeathiriwa na HCV ana uwezo wa asilimia 1.8 ya kupata ugonjwa Hatari inaongezeka kama sindano inayotumika ina shimo kubwa na jeraha ni kubwa. Kuna hatari kutoka kwa mfichuo wa kamasi hadi kwa damu; ingawa kiwango cha hatari hii ni ndogo, na hakuna hatari yoyote kama damu ikigusa ngozi isiyokuwa na jeraha.

Vifaa vya hospitali pia vinaweza kuambukiza Homa ya nyongo C kama vile: kutumia mara kwa mara sindano na pini,mifuko ya kujaza, na vifaa visivyo visafi vya hospitali. Hali mbaya ya hospitali au za kliniki za madaktari wa meno ndio sababu kubwa za maambukizi ya HCV nchini Misri, ni nchi yenye kiasi kikubwa cha maambukizi duniani.

Uhusiano wa kimapenzi

Haijulikani kama shughuli za ngono zinaweza kuleta maambukizi ya Homa ya nyongo C. Ingawa kuna uhusiano kati ya njia za hatari za kufanya ngono na Homa ya nyongo C, si wazi kama maambukizi ya ugonjwa huo yanatokana na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo hayakutajwa au ngono yenyewe. Ushahidi unaonyesha kwamba hakuna hatari ya maambukizi kwa wapenzi wa jinsia tofauti ambao hawana mapenzi na watu wengine.

Shughuli za ngono zinazoleta viwango vya juu vya majeraha ndani ya mfereji wa mkundu, kama vile kupenyeza mkunduni, au inayotokea wakati wa maambukizo ya zinaa kama yale yanayotokea wakati wa maambukizo ya zinaa, ikiwa ni pamoja na VVU au vidonda sehemu ya siri, zote hizi zinaleta hatari ya maambukizo.

Serikali ya Marekani inapendekeza matumizi ya kondomu kama njia pekee ya kuzuia maambukizi ya Homa ya nyongo C kwa watu wenye wapenzi wengi.< ref>"Hepatitis C Group Education Class". United States Department of Veteran Affairs. 

Kutoboa mwili

Uchoraji wa mwili unaongeza hatari mara mbili au tatu zaidi ya kupata Homa ya nyongo C. Hii inaweza kuwa kwa sababu vifaa vinavyotumiwa sio visafi au kuambukizwa na rangi iliyotumika.

Uchoraji au kujitoboa mwili kama shughuli hizi zilifanywa kabla ya miaka ya kati-1980 au ilifanywa na mtu asiye na ujuzi hasa inaleta wasiwasi, kwa sababu uwezekano wa kusafisha vifaa ni ndogo sana. Hatari ya kuambukizwa inaongezeka mara mbili zaidi kama mchoro ni mkubwa. Karibu nusu ya wafungwa wanatumia kwa pamoja vifaa vya kujichora ambavyo sio visafi. Ni mara chache uchoraji unafanywa katika sehemu zilizosajiliwa kuambukizwa na ugonjwa wa HCV.

Kugusa damu

Vifaa vya maangalizi binafsi kama vile mashine ya kunyolea, mswaki, na mashine ya kukata kucha yanaweza kuwa na damu. Kama zikitumiwa za zaidi ya mtu mmoja uwezekano ni mkubwa wa kuambukizana HCV. Watu wanatakiwa wawe waangalifu na mikwaruzo na vidonda au uvujaji wa damu. HCV haimbukizwi kwa kushikana kama vile kukumbatiana, kupeana busu, au kula kwa pamoja au kutumia kwa pamoja vyombo vya kulia chakula.

Maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto

Maambukizi ya Homa ya nyongo C kutoka kwa mama hadi kwa mtoto hutokea kwa asilimia 10 za mimba. Hakuna njia yoyote ya kupunguza hatari hii wakati wa kuzaa.

Hatari ya kuambukiza inaongezeka kama muda wa uchungu wa uzazi ni mrefu. Hakuna ushahidi wowote unaosema mtoto akinyonyeshwa maziwa ataambukizwa HCV; lakini, mama aliyeathiriwa hatakiwi amnyonyeshe mtoto kama chuchu zake zina mpasuko au zinavuja, au kama ana kiwango kikubwa cha virusi.

Uchunguzi wa ugonjwa

Homanyongo C 
Serologic profile of Homa ya nyongo C infection

Uchunguzi wa Homa ya nyongo C unaangalia yafuatayo: HCV kingamwili, ELISA, Western blot, pamoja na idadi ya HCV RNA. Polymerase chain reaction (PCR) inagundua HCV RNA wiki mmoja au mbili baada ya kuambukizwa, wakati vikinga mwili huchukua muda mrefu kutengenezwa na kuonekana.

Maambukizo ya muda mrefu ya Homa ya nyongo C, yanayoletwa na virusi vya Homa ya nyongo C ambavyo vinaweza kuishi mwilini kwa muda unaoweza kuzidi miezi sita kama RNA ipo au haipo. Kwa sababu ugonjwa huu kali hauonyeshi dalili zozote kwa muda mrefu, madaktari huwa kwa kawaida wanagudua ugonjwa huu wanapofanya uchunguzi wa maini au wakati wanapofanya utaratibu wa kawaida wa kuchunguza afya za watu walio hatarini. Uchunguzi hauwezi kutofautisha kati ya ugonjwa mahututi na ugonjwa sugu wa maini.

Upimaji damu

Upimaji wa Homa ya nyongo C kwa kawaida huanza na vipimo vya damu ili kugundua uwepo wa kingamwili kwa HCV kwa kutumia kimeng'enya immunoassay. Kama upimaji huu ni chanya, kipimo cha itafanywa ili kuthibitisha immunoassay na kuamua ukali. Uchanganuzi wa recombinant immunoblot inathibitisha immunoassay, na mmenyuko wa HCV RNA polimeresi huamua ukali. Kama hakuna RNA na immunoblot ni chanya, mtu alikuwa na maambukizi ya awali lakini ikaisha na aidha kwa matibabu au yenyewe; kama immunoblot ni hasi, immunoassay ilikuwa na makosa. Inachukua wiki sita hadi nane kwa kufuatia maambukizi kabla ya vipimo vya immunoassay kuonekana kuwa yako.

Vimeng'enya vya ini hubadilika wakati wa sehemu ya awali ya maambukizi; kwa wastani huanza kupanda katika wiki ya saba baada ya kuambukizwa. Ini za vimeng'enya huhusiana vibaya na ukali wa ugonjwa.

Biopsi

Biopsi za ini zinaweza kuamua kiwango cha uharibifu wa ini, lakini kuna hatari kutokana na utaratibu huo. Mabadiliko ya kawaida biopsi hutambua ni lymphocytes ndani ya tishu ya ini, vinyeleo vya limfu katika triad portal, na mabadiliko kwa vichirizi vya nyongo. Kuna idadi ya vipimo vya damu vinavyopatikana ambavyo vinajaribu kuamua kiwango cha uharibifu na kupunguza haja ya biopsi.

Uchunguzi

Watu wachache, kama asilimia 5-50 walioambukizwa nchini Marekani na Canada, wanafahamu hali yao. Kupima inapendekezwa kwa watu walio na hatari ya juu, ambao ni pamoja na watu wenye chale . Uchunguzi pia inapendekezwa kwa watu wenye muinuko wa kimeng'enya ya ini kwani hii ni ishara ya pekee ya homanyongosugu ya mara kwa mara. Uchunguzi wa mara kwa mara hapendekezwi nchini Marekani.

Kinga

Kufikia mwaka 2011, hakuna chanjo iliyopatikana kwa homa ya nyongo C. Chanjo zinatengenezwa, na baadhi zimeonyesha matokeo ya kutia moyo. Mchanganyiko wa mikakati ya kuzuia, kama vile mipango ya kubadilishana sindano na matibabu ya matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, hupunguza hatari ya homa ya nyongo C katika watumiaji wa madawa ya kujindunga kwa mishipa kwa karibu asilimia 75. Kuwachunguza watoaji damu ni muhimu katika kiwango cha kitaifa, kama ni kufuata tahadhari za ulimwenguni ndani ya vituo vya afya. Katika nchi ambako kuna ugavi usiotosha wa sindano hasi, watoa huduma wanapaswa kupeana madawa kwa mdomo badala ya kupitia sindano.

Matibabu

HCV inasababisha maambukizi sugu katika asilimia 50-80 ya watu walioambukizwa. Takriban asilimia 40-80 ya kesi hizi humalizika kwa matibabu.

Katika matukio machache, maambukizi yanaweza kuisha bila ya tiba. Watu wenye homa ya nyongo C sugu ni lazima wajiepushe pombe na madawa yaa sumu kwa ini, na wanapaswa kupatiwa chanjo ya homa y a manjano A na homanyongoB Watu walio na cirrhosis wanapaswa kuwa na vipimo vya ultrasound vya saratani ya ini.

Madawa

Watu wenye maambukizi ya ini ya HCV yaliyothibitika yasiyo ya kawaida wanapaswa kutafuta matibabu. Matibabu ya sasa ni mchanganyiko wa pegylated interferon na madawa ya kupunguza makali ya ukimwi ribavirin kwa muda wa wiki 24 au 48, kulingana na aina ya HCV . Matokeo bora hutokea kwa asilimia 50-60% ya watu waliotibiwa. Kuchanganya ama boceprevir au telaprevir na ribavirin na peginterferon alfa inaboresha matokeo ya homa ya nyongo C genotype 1. Madhara kwa matibabu ni ya kawaida, nusu ya watu wanaotibiwa hupata dalili kama homa ya mafua, na theluthi ya watu hupata matatizo ya mhemuko. Tiba katika miezi sita za kwanza ni bora zaidi kuliko baada ya homa ya nyongo C kuwa sugu. Kama mtu anapata maambukizi mapya na haijaisha baada ya wiki nane hadi kumi na mbili, wiki 24 ya pegylated interferon inapendekezwa. Kwa watu wenye thalasemia (ugonjwa wa damu), ribavirin inaonekana kuwa muhimu, lakini huongeza haja ya upaji wa damu.

Watetezi wanadai tiba kadhaa mbadala kuwa na manufaa kwa homa ya nyongo C ikiwa ni pamoja na maziwa mbigili, ginseng, na colloidal silver Hata hivyo, hakuna tiba mbadala imeonekana kuboresha matokeo katika homa manjano C, na hakuna ushahidi upo ambao tiba mbadala ina athari yoyote kwenye virusi wakati wote .

Ubashiri

Majibu ya matibabu hutofautiana kulingana na genotype. Majibu endelevu ni kadiri asilimia 40-50 kwa watu wenye HCV genotype 1 kwa muda wa wiki 48 ya matibabu. Majibu endelevu hutokea katika asilimia 70-80 kwa watu walio na genotypes HCV 2 na 3 kwa muda wa wiki 24 ya matibabu. Majibu endelevu ni kadiri ya asilimia 65 kwa watu wenye genotype 4 kwa muda wa wiki 48 ya matibabu. Ushahidi wa matibabu katika ugonjwa genotype 6 kwa sasa ni chache, na ushahidi uliopo ni wa muda wa wiki 48 ya tiba katika vipimo sawa na ugonjwa wa genotype 1.

Uenezi

Homanyongo C 
Maambukizi ya homa ya nyongo C duniani kote mwaka 1999
Homanyongo C 
Disability-adjusted life year ya homa ya nyongo C mwaka 2004 kwa kila wakazi 100,000
     no data      <10      10-15      15-20      20-25      25-30      30-35
     35-40      40-45      45-50      50-75      75–100      >100

Kati ya watu milioni 130 na 170, au ~ asilimia 3 ya idadi ya watu duniani, wanaishi na homa ya nyongo C sugu. Kati ya watu milioni 3-4 huambukizwa kwa mwaka, na zaidi ya watu 350,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa-husiana na homa ya nyongo C. Viwango vimeongezeka pakubwa katika karne ya 20 kutokana na mchanganyiko wa IDU na madawa ya kujidunga katika mishipa au vifaa vya matibabu visivyokifishwa.

Nchini Marekani, kadiri ya asilimia 2 ya watu wana homa ya nyongo C, pamoja na kesi mpya 35,000 hadi 185,000 kwa mwaka. Viwango vimepungua katika nchi za Magharibi tangu miaka ya 1990 kutokana na uchunguzi wa kuboresha damu kabla ya utoaji. Vifo vya kila mwaka kutokana na HCV nchini Marekani ni kadiri kutoka 8,000 hadi 10,000. Matarajio ni kwamba kiwango hiki cha vifo itaongezeka wakati watu walioathirika kwa utoaji damu kabla ya kupimwa HCV kuwa wagonjwa na kufa.

Viwango vya maambukizi viko juu katika baadhi ya nchi za Afrika na Asia. Nchi zilizi na viwango vya juu sana vya maambukizi ni Misri (asilimia 22), Pakistani (asilimia 4.8) na Uchina (asilimia 3.2). Kiwango cha juu nchini Misri inahusishwa na kampeni ya umma ya matibabu ya sasa-iliyositishwa ya schistosomiasis, kwa kutumia sindano za kioo zisizokifishwa vizuri.

Historia

Katika miaka ya 1970 katikati, Harvey J. Alter, Mkuu wa Sehemu ya Magonjwa ya Maambukizi katika Idara ya Madawa ya Kujidunga kwa mishii katika Taasisi ya Kitaifa ya Afya, na timu yake ya utafiti walionyesha kuwa kesi nyingi za utoaji wa baada-damu ya homanyongohazikutokana na viruzi vya homanyongoA au B. Licha ya ugunduzi huu, jitihada za utafiti wa kimataifa za kutambua virusi zilishindiana kwa miaka kumi ifuatayo. Mwaka 1987, Michael Houghton, qui-Lim Choo, na George Kuo katika Shirika la Chiron, wakishirikiana na Dkt. DW Bradley kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, walitumia mbinu mpya ya molecular cloning ya kubaini kiumbe kisichojulikana na kukuza uchunguzi wa ubainishaji.. Mwaka 1988, Alter alithibitisha virusi kwa kuthibitisha uwepo wao katika jopo la vielelezo vya homanyongozisizo A zisizo B. Mwezi Aprili 1989, ugunduzi wa HCV ulichapishwa katika makala mbili katika jarida la "Sayansi". Ugunduzi ulisababisha mafanikio makubwa katika utambuzi na kuboresha matibabu ya kupunguza makali ya virusi. Mwaka 2000, Dkt. Alter na Houghton walitukuzwa na Tuzo ya Lasker ya Utafiti wa Kitabibu ya Hospitali ya "kuongoza kazi inayosababisha ugunduzi wa virusi vinavyosababisha homa ya nyongo C na mbinu za kukuza uchunguzi ambazo zilipunguza hatari ya utoaji damu-ilihusisha homa y a manjano nchini Marekani kutoka asilimia 30 mwaka 1970 hadi karibu sifuri mwaka 2000."

Chiron aliwasilisha hataza kadhaa kuhusu virusi na uchunguzi wake. Maombi ya mashindano ya hataza na CDC ilikuwa imeshuka mwaka 1990 baada ya Chiron kulipa dola milioni 1,900,000 kwa CDC na dola 337,500 kwa Bradley. Mwaka 1994, Bradley alimshtaki Chiron, wakitaka kubatilisha hataza, alitaka yeye mwenyewe ajumuishwe kama mbunifu mshiriki, na kupokea mapato ya uharibifu na ya mrahaba. Alisitisha mashtaka mwaka 1998 baada ya kupoteza mbele ya mahakama ya rufaa.

Jamii na utamaduni

Mwungano wa Dunia wa Homanyongo inaratibu siku ya Dunia ya Homa ya nyongo, hufanyika kila mwaka tarehe 28 mwezi Julai. Gharama za kiuchumi za homa ya nyongo C ni muhimu kwa mtu binafsi na kwa jamii kijumla. Nchini Marekani wastani ya gharama ya maisha ya ugonjwa huo ilikadiriwa kuwa dola 33,407 za marekani mwaka 2003, na gharama ya kupandikiza ini ni takriban dola 200,000 za Marekani kufikia mwaka 2011. Nchini Canada gharama ya matibabu ya kupambana na virusi yalikuwa juu kama dola 30,000 za Canada mwaka 2003, wakati Marekani gharama ni kati ya dola 9200 na 17,600 za Marekani mwaka 1998. Katika maeneo mengi ya dunia watu wanashindwa kumudu matibabu na madawa ya kupunguza makali ya virusi kwa sababu ya kukosa bima au bima waliyo nayo haitalipa madawa ya kupunguza makali ya virusi.

Utafiti

Kufikia mwaka 2011, karibu madawa mia moja yanakuzwa kwa ajili ya homa ya nyongo C. Dawa hizi ni pamoja na chanjo za kutibu homa ya manjano, immunomodulators, na vizuia vya cyclophilin. Uwezekano wa matibabu haya mapya yamekuja kutokana na uelewa mzuri wa virusi vya homa ya nyongo C.

References

Tags:

Homanyongo C Viashiria na daliliHomanyongo C ChanzoHomanyongo C Uchunguzi wa ugonjwaHomanyongo C KingaHomanyongo C MatibabuHomanyongo C UbashiriHomanyongo C UeneziHomanyongo C HistoriaHomanyongo C Jamii na utamaduniHomanyongo C UtafitiHomanyongo CHoma ya manjano

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UtamaduniUbungoLakabuKongoshoMatumizi ya lugha ya KiswahiliMafurikoBunge la TanzaniaNomino za dhahaniaAmri KumiHektariWema SepetuMkoa wa ManyaraNuktambiliOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaKanga (ndege)MaktabaNyotaKimara (Ubungo)Orodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaWingu (mtandao)Historia ya UislamuVidonda vya tumboMaudhui katika kazi ya kifasihiKiolwa cha anganiDamuAthari za muda mrefu za pombeMahindiBikira MariaHistoria ya Kanisa KatolikiOrodha ya makabila ya KenyaMamaKoroshoRufiji (mto)Orodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoUislamuOrodha ya milima ya TanzaniaInstagramUgonjwa wa kuharaUsanifu wa ndaniMuhammadDini asilia za KiafrikaMalariaSiasaMkoa wa ArushaSoko la watumwaPentekosteMziziTafakuriAlomofuUtoaji mimbavvjndSexViwakilishi vya pekeeSemiShairiSanaa za maoneshoOrodha ya makabila ya TanzaniaRitifaaMwenge wa UhuruUchumiViwakilishi vya kumilikiOrodha ya milima ya AfrikaHistoria ya ZanzibarUshairiMwanaumeLuhaga Joelson MpinaMizimuOrodha ya majimbo ya MarekaniMlongeVita Kuu ya Pili ya DuniaPapa (samaki)Alama ya barabaraniMvua ya mawe🡆 More