S ni herufi ya 19 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa.
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
Asili yake ni Sigma ya alfabeti ya Kigiriki.
Kisemiti asilia alama ya meno | Kifinisia shin | Kigiriki Sigma | Kietruski S | Kilatini S |
---|---|---|---|---|
Asili ya herufi S ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na alama ya "shin" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya meno wakitumia alama tu kwa sauti ya "sh" na kuiita kwa neno lao kwa meno "shin". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "sigma" bila kujali maana asilia ya "meno". Kwao imekuwa sauti tu ya "s" kwa sababu hawakujua "sh".
Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi wakigeuza mwelekeo wake. Waroma wakaichukua kutoka hapa lakini walilainisha kona kali kuwa S jinsi ilivyo hadi sasa.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article S, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.