Ustaarabu Wa Indus

Ustaarabu wa Indus (pia: utamaduni wa Harappa; kwa Kiingereza: Indus Valley civilization) ulikuwa ustaarabu wa Zama za Shaba (3300-1500 KK; kipindi cha kukomaa kikiwa mnamo 2000 KK) uliopatikana katika bonde la mto Indus katika Pakistan na Uhindi ya leo.

Ustaarabu Wa Indus
Ukubwa na mtandao wa ustaarabu wa Bonde la Indus.

Ugunduzi

Habari zake zimepatikana kwa njia ya uvumbuzi wa kiakiolojia kuanzia miaka ya 1880.

Mji wa kwanza kugunduliwa ulikuwa Harappa iliyoangaliwa na Mwingereza Masson aliyedhani ni mmoja wa miji iliyotembelewa na Aleksanda Mkuu; utafiti wa baadaye ulionyesha umri wake ni wa kale zaidi. Mwanaakiolojia Mhindi R. D. Banerji alitambua mnamo 1923 kwamba mabaki ya Harappa yalifanana na yale ya Mohenjo-daro iliyopo kilomita 600 upande wa kusini. Baada ya kugunduliwa kwa sehemu nyingine yenye maghofu ilionekana kwamba hayo ni mabaki ya ustaarabu ulioanza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea katika bonde la mto Indus pamoja na matawimito yake makubwa. Pamoja na miji mingi midogo mabaki ya miji mikubwa mitano yamegunduliwa ambayo ni Harappa, Mohenjo-daro na Ganeriwala katika Pakistan ya leo na Dholavira na Rakhigarhi upande wa Uhindi ya leo..

Miji yake

Ustaarabu huo ulianza wakati wa Zama za Shaba ukaendelea kustawi hadi takriban mwaka 1500 KK. Kwa hiyo ilidumu muda mrefu sana.

Watu wa Bonde la Indus walikuwa wajenzi hodari. Miji yao ilipangwa vizuri. Ilikuwa na mfumo wa majitaka, kwa kuweka mfereji wa majitaka kando ya kila mtaa. Hakuna mifano mingine wa miundombinu hiyo katika sehemu nyingine za Dunia kwa wakati ule. Nyumba zilikuwa na ghorofa moja au mbili, na nyingi zilikuwa na chumba cha bafu lakini kulikuwa pia na bafu za umma. Maji yalipelekwa mjini na kugawiwa kwa matangi ya nyumba. Nyumba zilikuwa pia na choo, na uchafu wa nyumba jirani ulipitishwa kwa kumwaga maji katika mabomba ya kitofali hadi shimo kubwa; mashimo hayo yalisafishwa baada ya muda, labda kwa kutumia yaliyomo kama samadi mashambani.

Tofauti na tamaduni nyingine za milenia ya tatu na ya pili KK katika Misri ya Kale na Mesopotamia hawakuacha majengo makubwa kama mahekalu au majumba ya kifalme. Majengo makubwa zaidi yaliyoweza kutambuliwa yanaonekana kuwa ghala za nafaka.

Maandishi

Ustaarabu Wa Indus 
Maandishi ya ustaarabu wa Indus.

Watu walitumia aina ya maandishi lakini hadi leo haijawezekana kuyasoma. Kwa hiyo haijulikani walitumia lugha gani. Mwandiko ulitumia takribani alama 400 na mifano mingi inaonekana kama mabaki ya mihuri iliyoonyesha asili ya bidhaa fulani au yaliyomo ya chombo. Maandishi yote ni mafupi sana yenye alama chache tu.

Mwisho

Haijulikani ni nini kilichosababisha mwisho wa ustaarabu huo. Tangu mwaka 2000 KK kuna dalili za kushuka kwa hali ya uchumi. Mnamo mwaka 1700 KK miji mingi haikukaliwa tena. Utafiti wa masalia ya binadamu kutoka makaburi ya siku zile unaonyesha kuongezeka kwa majeruhi na dalili ya magonjwa kama ukoma na kifua kikuu. Wengine walifikiri ilikuwa labda uhamiaji wa makabila ya Kihindi-Kiulaya walioanza kuingia Uhindi mwisho wa milenia ya pili. Wengine wanaona ilikuwa mabadiliko ya tabianchi hasa kipindi kirefu cha ukame, pamoja na mfululizo wa matetemeko ya ardhi..

Picha

Marejeo

Viungo vya Nje

Ustaarabu Wa Indus 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Ustaarabu Wa Indus  Mohenjo-daro travel guide kutoka Wikisafiri

Ustaarabu Wa Indus 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Ustaarabu Wa Indus  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ustaarabu wa Indus kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ustaarabu Wa Indus UgunduziUstaarabu Wa Indus Miji yakeUstaarabu Wa Indus PichaUstaarabu Wa Indus MarejeoUstaarabu Wa Indus Viungo vya NjeUstaarabu Wa Indus1500 KK2000 KKKiingerezaMto IndusPakistanUhindiUstaarabuZama za Shaba

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

RohoSabatoKata za Mkoa wa Dar es SalaamBahari ya HindiKihusishiUundaji wa manenoAfrikaMaudhuiShambaJumuiya ya MadolaInstagramUshairiUandishi wa inshaMkoa wa TangaNdovuPijini na krioliUkristo nchini TanzaniaWanyamaporiMkutano wa Berlin wa 1885MatiniUsawa (hisabati)Lionel MessiStephane Aziz KiIsraeli ya KaleWayahudiViwakilishi vya idadiHadhiraNominoWema SepetuJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaNguzo tano za UislamuSerikaliMshororoVivumishi vya -a unganifuMagonjwa ya machoUajemiUchawiKhalifaAlomofuMwanzo (Biblia)Afrika Mashariki 1800-1845Cleopa David MsuyaFasihi andishiTanganyikaIsraelSakramentiEdward SokoineVipera vya semiMaudhui katika kazi ya kifasihiBarua pepeBunge la TanzaniaWilaya ya KinondoniIdi AminEe Mungu Nguvu YetuUlumbiTanganyika African National UnionRita wa CasciaBiblia ya KikristoMichael JacksonRupiaMusaPemba (kisiwa)RejistaStadi za lughaJose ChameleoneInjili ya MarkoJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoUfugaji wa kukuUnyagoMashuke (kundinyota)NevaUpepo🡆 More