Hekalu

Hekalu ni jengo la dini mbalimbali, lakini si zote.

Hekalu
Nakala ya Parthenon ya Athens iliyojengwa huko Nashville (Tennessee) nchini Marekani
Hekalu
Hekalu la Kibudha huko Angkor Wat nchiniCambodia

Nyingine zinaita maabadi yao kwa majina tofauti, kutokana na mtazamo wa msingi.

Kwa mfano katika Uislamu jengo la ibada linaitwa msikiti.

Hekalu katika Uyahudi

Hekalu 
Mfano wa hekalu la pili la Yerusalemu.

Katika Biblia lina umuhimu wa pekee hekalu la Yerusalemu, lililojengwa kwanza na mfalme Sulemani, mwana wa Daudi likabomolewa na mfalme Nebukadreza II wa Babuloni mwaka 586 K.K..

Hekalu hilo likajengwa upya (536 K.K. - 515 K.K.) baada ya uhamisho wa Babeli, likatakaswa na kuwekwa wakfu upya na Yuda Mmakabayo (164 K.K.), likapanuliwa na kupambwa na mfalme Herode Mkuu na Wayahudi wote (19-64 BK) hadi miaka michache kabla halijabomolewa tena na Warumi mwaka 70.

Tangu hapo halijajengwa tena, hivi kwamba sadaka zinazodaiwa na Torati hadi sasa haziwezi kutolewa kwa muda wa miaka 2000 hivi.

Tangu wakati wa uhamisho hadi leo Wayahudi wanaendelea kukusanyika katika majengo yanayoitwa masinagogi (yaani "mkutano").

Hekalu katika Ukristo

Yesu Kristo alikuwa ametabiri maangamizi hayo miaka 40 hivi ya nyuma, akisema saa imefika ya kumtolea Mungu Baba ibada mpya katika Roho na ukweli.

Alipotakasa hekalu hilo, alitangaza kuwa mwili wake mfufuka utakuwa ndio hekalu la kweli ambamo watu wote wamuendee Mungu na kumtolea ibada hiyo.

Ndiyo sababu kwa kawaida maabadi ya Wakristo huitwa kanisa (yaani "mkusanyiko"), si hekalu.

Hekalu  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

DiniJengo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KiongoziHadithi za Mtume MuhammadBenki ya DuniaUti wa mgongoOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoHistoriaKonsonantiHurafaLugha ya taifaDagaaMkoa wa KageraRiwayaMkataba wa Helgoland-ZanzibarViganoTungoNdoaTungo kishaziSteve MweusiUandishi wa ripotiUzazi wa mpangoUkabailaKamusiCleopa David MsuyaViwakilishiMbuyuOrodha ya nchi za AfrikaLigi ya Mabingwa UlayaMkoa wa ShinyangaMichezo ya jukwaaniMsamiatiMkoa wa IringaShangaziBiashara ya watumwaSkeliP. FunkVivumishi vya kuoneshaChuiDodoma MakuluUzazi wa mpango kwa njia asiliaFamiliaKiambishi tamatiKiini cha atomuSerikaliSheng22 ApriliMoyoAli Hassan MwinyiMmeaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaSiasaDhima ya fasihi katika maishaLatitudoViwakilishi vya sifaMkoa wa KigomaChristina ShushoFacebookYouTubeWamasoniMwanzoRejistaMahakamaSaidi NtibazonkizaKinywajiDoto Mashaka BitekoMpira wa miguuMsokoto wa watoto wachangaSisimiziSexKishazi tegemeziMnururishoMuzikiInjili ya MathayoMkoa wa ManyaraHaki za binadamu🡆 More