Punjab (pia: Panjab; kwa Kipunjabi: ਪੰਜਾਬ panjāb, maji tano au nchi ya mito mitano) ilikuwa jimbo la Uhindi wa Kiingereza lililogawiwa tangu 1947 kati ya nchi za Uhindi na Pakistan.
Kijiografia ni tambarare ya mito mitano inayoingia katika mto Indus upande wa mashariki. Hali ya hewa ni yabisi lakini maji ya mito ni msingi wa kilimo cha umwagiliaji. Kilimo hicho chazalisha sehemu kubwa ya chakula cha Uhindi na Pakistan.
Panjab ni chanzo cha ustaarabu wa Uhindi wa Kale na maghofu ya Harappa yako huko. Hadithi nyingi za maandiko matakatifu ya Uhindu kama Rig Veda, Upanishadi na Mahabarata yaliandikwa huko.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Punjab kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Punjab, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.