Mohenjo-Daro

Mohenjo-Daro ilikuwa mji mkubwa katika ustaarabu wa Indus uliostawi kwenye bonde la Mto Indus.

Iko katika jimbo la Sindh, Pakistan ya leo.

Mohenjo-Daro
Mohenjo-Daro
Ramani ya miji mikubwa zaidi ya utamaduni wa Harappa.
Mohenjo-Daro
Sanamu ya "Binti anayecheza" iliyopatikana Mohenjo-Daro.
Mohenjo-Daro
Sanamu ya kiongozi anayeaminiwa kuwa mfalme na kuhani mnamo 2,500-1,500 BK iliyopatikana kati ya maghofu ya Mohenjo-Daro.

Mji ulijengwa mnamo mwaka 2600 KK na kuwa kati ya miji ya kwanza duniani inayojulikana. Mohenjo-Daro ilistawi wakati mmoja na tamaduni za Misri ya Kale na Mesopotamia.

Mabaki ya mji yamepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.

Historia

Mohenjo-Daro ilijengwa mnamo karne ya 25 KK. Ilikuwa kati ya miji mikubwa ya utamaduni wa Harappa ulioenea katika bonde la mto Indus. Utamaduni huo ulianza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea juu ya sehemu kubwa za Pakistan na Uhindi ya Kaskazini ya leo. Miji muhimu iliyotambuliwa na wanaakiolojia ilikuwa Harappa, Mohenjo-Daro, Lothal, Kalibangan, Dholavira na Rakhigarhi.

Mohenjo-Daro ilikuwa mji mkubwa wa Zama za Shaba yaani kipindi ambapo watu walikuwa wameshaanza kutumia metali badala ya zana za mawe tu lakini bado hawakutumia chuma.

Wataalamu wametambua kiwango cha juu wa kupangwa kwa mji huu. Wajenzi wake walitumia tayari matofali yaliyosanifishwa kwa kutumia vipimo vya sentimita 6 × 13 × 27.

Mji wote ulikuwa na mfumo wa visima vya maji zaidi ya 700 na pia mifereji kwa maji machafu. Watu wake walikuwa pia na mwandiko ambao haujatafsiriwa.

Mnamo mwaka 1900 KK utamaduni wa Harappa uliporomoka kwa sababu ambazo hazikueleweka bado na wakazi waliondoka mjini.

Mohenjo-Daro 
Maghofu ya majengo ya Mohenjo-Daro.

Tanbihi

Mohenjo-Daro  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohenjo-Daro kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BondeJimboMjiMto IndusPakistanUstaarabu wa Indus

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ligi ya Mabingwa AfrikaMnazi (mti)Nguzo tano za UislamuPijini na krioliWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiNamba za simu TanzaniaLeonard MbotelaLafudhiDodoma (mji)Umoja wa KisovyetiBungeMikoa ya TanzaniaIniAbrahamuKambaleMsikitiWahaMajira ya mvuaUandishi wa inshaDivaiKiboko (mnyama)Jay MelodyOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMapinduzi ya ZanzibarKanadaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaWahayaMkatabaAgano JipyaAbedi Amani KarumeKarafuuElimuInjili ya MathayoMkurugenziBendera ya KenyaIsha RamadhaniMjasiriamaliOrodha ya miji ya Afrika KusiniBustaniSteven KanumbaUtamaduniLigi Kuu Tanzania BaraP. FunkWilaya ya KinondoniUchumiBawasiriMfumo wa upumuajiSimba S.C.Historia ya UislamuHistoria ya Afrika KusiniHistoria ya WapareMzabibuUbuntuBinamuVivumishi vya -a unganifuArudhiGabriel RuhumbikaMisriChanika (Ilala)TundaJulius NyerereMkoa wa MaraOrodha ya Marais wa TanzaniaSarufiKifaruTaswira katika fasihiWarakaNominoVivumishi vya pekeeMalariaMartin LutherUfeministiChumba cha Mtoano (2010)Mwenge wa UhuruChuiOrodha ya Marais wa Zanzibar🡆 More