Jimbo ni eneo fulani lililotengwa kwa ajili ya kurahisisha utawala ndani ya dola au nchi fulani.
Neno latumiwa pia kwa vitengo mmndani ya Kanisa.
Majimbo huwa na madaraka mbalimbali, na mazoea katika matumizi ya neno hili ni tofauti kati ya nchi na nchi.
Mara nyingi jimbo ni eneo lenye kiwango kikubwa cha kujitawala hasa majimbo ndani ya muundo wa shirikisho; mifano michache tu ni majimbo ya Afrika Kusini, Nigeria, Marekani au Ujerumani.
Wakati mwingine jimbo ni jina la kihistoria tu hata halina madaraka ya kiutawala tena.
Jimbo la uchaguzi ni eneo ambako mbunge huchaguliwa. Nchi za Afrika ya Mashariki hugawiwa kwa majimbo ya uchaguzi; katika kila jimbo mwakilishi mmoja huchaguliwa na wananchi kwa njia ya kura atakayekuwa mbunge wa eneo hili katika bunge la kitaifa.
Katika nchi yenye muundo wa shirikisho kina pia majimbo yauchaguzi kwenye ngazi za madola au majimbo ya kujitawala ndani ya taifa.
Vilevile ndani ya Kanisa jina linatumiwa tofauti na madhehebu mbalimbali.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jimbo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.