Ufeministi

Ufeministi (kutoka mzizi wa Kilatini femina, yaani wa kike; kwa Kifaransa féminisme linamaanisha harakati ya ukombozi wa wanawake‎) ni jina linalojumlisha aina nyingi za misimamo, itikadi na matapo tofautitofauti yanayochanga lengo kuu la kutetea haki za wanawake dhidi ya ubaguzi wa jinsia uliotawala dunia kwa muda mrefu sana upande wa siasa, uchumi, utamaduni, dini na jamii kwa jumla.

Ufeministi
Maandamano katika Sikukuu ya Kimataifa ya Wanawake huko Dhaka, Bangladesh, tarehe 8 Machi 2005.
Ufeministi
Kikosi cha Femen ni Wafeministi wenye itikadi kali.

Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile.

Kati ya haki hizo za msingi, ufeministi umepigania kwa mfano zile za kupiga kura, kupata vyeo serikalini, kufanya kazi, kulipwa mshahara, kumiliki, kupata malezi, kufanya mikataba sawa na wanaume n.k.

Ufeministi umepinga pia ubakaji wa aina zote.

Ufeministi ni kati ya matapo yaliyochangia zaidi mabadiliko katika jamii.

Historia

Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza katika Ulaya wakati haki za binadamu zilipoanza kutangazwa, ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee.

Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kampeni ya awali kuanzia karne ya 19, lakini hasa ya 20.

Mikondo tofauti ya ufeministi leo

Ufeministi 
Alama ya ufeministi mkali

Mgawanyiko umeanza kujitokeza kati ya wale wanaotaka wanawake wafanane kabisa na wanaume na wale wanaoona umuhimu wa kutunza upekee wa mwanamke katika uhusiano wa kukamilishana na mwanamume. Kwa mfano:

  • wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani hoja ya jadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa: wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki katika shughuli zote sawasawa.
  • wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakini tofauti hizo zisiruhusiwe kuwapa wanaume kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa, lakini wasilazimishwe kufanya hivyo, nao wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hiyo ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka waliyoitumia kwa kazi ya nyumbani.
  • wengine husema jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenzi ya wanaume, hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapinduzi katika jamii.
  • kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume, na ni muhimu watoe mchango wao wa pekee.

Kuna namna nyingi za kueleza tofauti katika itikadi ya ufeministi lakini hiai hapa ndizo tatu kubwa:

Ufeministi wa kitamaduni - Hii ni aina ya ufeministi ambayo inaangazia ubaguzi katika kawaida ya jamii. Ndio wanoataka utamaduni uthamini hulka za wanawake kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano hawa wanaweza kusema wanawake wanachukuliwa vibaya katika vyeo vya juu kutokana na wanaume.

Ufeministi wa uhuru - Hii ni aina ya ufeministi ambayo inaangazia haki za wanawake za kufanya usawa na wanaume hasa. Ndio wanaotaka sheria iruhusu yote yanayoruhusiwa tayari kwa wanaume. Kwa mfano haki za kupiga kura, za kuwania wadhifa wa siasa, au kuvaa mavazi yoyote.

Ufeministi mkali (radical feminism) - Hii ni aina ya ufeministi dubwana kupita nyingine inayodai kwamba hakuna tofauti kati ya wanaume na wanawake ila zile zinazofundishwa na jamii. Kwa mfano, kulingana na itikadi hii, tabia kati ya jinsia siyo ya kibiolojia bali ni ya mafunzo tu. Wafausi hao wanaamini tofauti hizi zipo ili wanaume waweze kudhulumu wanawake.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Ufeministi 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Ufeministi  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufeministi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ufeministi HistoriaUfeministi Mikondo tofauti ya ufeministi leoUfeministi TanbihiUfeministi MarejeoUfeministi Viungo vya njeUfeministiDiniDuniaHakiJamiiJinaKifaransaKilatiniMziziSiasaUchumiUtamaduniWanawake

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Injili ya MathayoHistoria ya WasanguInshaWandaliArusha (mji)TabainiIsimilaDoto Mashaka BitekoAli ibn Abu TalibEdward Ngoyai LowassaMuhammadTovutiMofimuAfande SeleKrioliMpira wa kikapuPemba (kisiwa)Nguzo tano za UislamuShikamooMtakatifu PauloAkiolojiaTendo la ndoaKiunguliaBinadamuJuaSudan KusiniRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniNetiboliKunguniFigoJuma kuuUhakikiShetaniUmaskiniJeshiMnururishoBenjamin MkapaUsimbajiMethaliKataUkomeshaji wa Biashara ya WatumwaMkoa wa PwaniMuda sanifu wa duniaHoma ya matumboOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaWayao (Tanzania)Vivumishi vya pekeeAsiaKorea KaskaziniMsituSemiHedhiMbogaMnara wa BabeliMtume YohanePentekosteHekalu la YerusalemuUshairiUtendi wa Fumo LiyongoWikiBakteriaSeli nyeupe za damuHekimaKanisa KatolikiKunguruOrodha ya Marais wa MarekaniNomino za wingiMsalabaVivumishi vya kumilikiHelaNgw'anamalundiLugha ya kwanzaWandengerekoMwezi mwandamoOrodha ya vyama vya siasa Tanzania🡆 More