Australia Na Pasifiki: Eneo la kijiografia linalojumuisha Australasia, Melanesia, Micronesia na Polynesia

Australia na Visiwa vya Pasifiki (pia: Oceania, Okeania, Oshania) hujumlishwa mara nyingi pamoja katika hesabu ya mabara.

Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo
Ramani ya Australia na Visiwa vya Pasifiki
* AS: Samoa ya Marekani * AU: Australia * CK: Visiwa vya Cook * FJ: Fiji * FM: Mikronesia * GU: Guam (USA) * KI: Kiribati * MH: Visiwa vya Marshall * MP: Visiwa vya Mariana * NC: Kaledonia Mpya (Ufaransa) * NR: Nauru * NU: Niue (New Zealand) * NZ: New Zealand * PF: Polynesia ya Kifaransa * PG: Papua Guinea Mpya * PN: Pitcairn (Uingereza) * PW: Palau * SB: Visiwa vya Solomon * TL: Timor ya Mashariki * TK: Tokelau * TO: Tonga * TV: Tuvalu * US: Hawaii * VU: Vanuatu * WF: Wallis na Futuna (Ufaransa) * WS: Samoa ya Magharibi Nchi za Asia * [BN]: Brunei * [CN]: China * [ID]: Indonesia * [MY]: Malaysia * [PH]: Ufilipino * [TW]: Taiwan

Hasa watu kwenye visiwa vingi vya Pasifiki wana utamaduni wa karibu. Vilevile historia ya visiwa hivyo kabla ya kuenea kwa ukoloni imefanana katika mengi.

Bara au la?

Hivyo mara nyingi sehemu hii ya dunia imeitwa "Bara la Kiutamaduni". Jina hili si sahihi kijiografia kwa sababu maeneo yake yako juu ya mabamba ya gandunia tofauti, kama vile bamba la Pasifiki, bamba la Australia na mengine madogo. Hata wataalamu hawapatani kuhusu mipaka ya eneo hilo.

Jina

Kwa lugha nyingi za dunia jina la "Oceania" (Okeania, Oshania) limekuwa la kawaida kutokana na neno la Kigiriki "okeanos" (kwa Kilatini: oceanus; kwa Kiingereza: ocean). Hivyo "Oceania" yamaanisha "nchi katika bahari". Ila tu hatuoni faida ya kuingiza neno hili katika lugha ya Kiswahili kwa sababu ni neno lisiloeleweka vizuri. Mara wataalamu hujadili "Oceania" kuwa visiwa vya Pasifiki pamoja na Australia; mara wanaona "Oceania" ni visiwa vile pekee bila Australia na wengine wanasema wenyewe "visiwa vya Pasifiki" ingekuwa jina zuri zaidi kama Australia haihesabiwi.

"Australasia" imekuwa jaribio tofauti la kutaja eneo, hasa kati ya wataalamu wa Australia, ila tu halipendwi na watu wengi visiwani. Hivyo imetumiwa zaidi kwa kanda la Australia na visiwa jirani pekee.

Eneo

Visiwa vyote kwa pamoja (bila Australia yenyewe) hukadiriwa kuwa 7,500 vyenye eneo la nchi kavu la kilomita za mraba milioni 1.3 vilivyosambaa katika eneo la bahari la kilomita za mraba milioni 70. Takriban visiwa 2,100 vimekaliwa na watu milioni 14.9.

Jiolojia

Eneo hili si bara kwa maana ya jiolojia. Visiwa vikubwa vya New Zealand, Guinea Mpya, Kaledonia Mpya na Tasmania ni mabaki ya bamba la Gondwana ya kihistoria. Guinea Mpya imetenganishwa na Australia kwa bahari ya Arafura isiyo na kina kirefu na wakati wa enzi ya barafu iliyopita zilikuwa kama nchi moja kwa sababu uwiano wa bahari ulikuwa chini kuliko leo.

Visiwa vingi katika Pasifiki ni milima ya volkeno inayoinuka kutoka tako la bahari hadi uso wa maji; mara nyingi zinaonyesha kasoko. Visiwa vingine vinajengwa na matumbawe yanayokua juu ya volkeno ambazo zimeishia kidogo chini ya uso wa bahari. Visiwa vingine ni atoli ambako matumbawe yamejenga tuta tumbawe kwa umbo la mviringo kuzunguka kisiwa cha kivolkeno.

Sababu ya kutokea kwa volkeno nyingi ni miendo ya gandunia katika tabaka za ganda la dunia chini ya bahari. Ngozi ya nje au ganda la dunia hufanywa na vipande mbamlimbali (=mabamba ya gandunia) vinavyoelea juu ya tabaka ya mwamba moto na kiowevu. Pale ambako vipande hivi vinagusana mara kwa joto na mwamba moto ulioyeyuka unapanda juu; pale ambao kupanda huku kunatokea haraka tunaona volkeno na hivyo kisiwa kipya kutokea. Mfano ni safu ya visiwa vya Hawaii ambavyo ni safu ya milima ya volkeno inayoanza kwenye tako la bahari, mengine inaonekana kama visiwa, mengine iko chini ya uso wa bahari.

Historia

Angalia Historia ya maeneo ya Pasifiki na Historia ya Australia

Kanda

Mara nyingi kanda nne zimetofautishwa:

Maeneo yanayotajwa kwa "Melanesia" na "Australasia" huingiliana.

Nchi na Maeneo ya Australia na Visiwa vya Pasifiki

(Nchi huru zaonekana kwa mwandiko mzito, maeneo yaliyo chini ya nchi nyingine kwa mwandiko wa kawaida)

Jina la eneo,
pamoja na bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(kadiro mnamo
1 Julai 2002)
Msongamano
(watu kwenye km²)
Mji mkuu
Australasia (Australia na New Zealand)
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Australia
7,686,850 20,697,241 2.5 Canberra
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Kisiwa cha Krismasi (Australia)
135 474 3.5 The Settlement
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Cocos (Keeling) (Australia)
14 632 45.1 West Island
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
New Zealand
268,680 3,908,037 14.5 Wellington
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Kisiwa cha Norfolk (Australia)
35 1,866 53.3 Kingston
Melanesia
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Fiji
18,270 856,346 46.9 Suva
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Sehemu za Indonesia
499,852 4,211,532 8.4 Jakarta
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Kaledonia Mpya (Ufaransa)
19,060 207,858 10.9 Nouméa
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Papua Guinea Mpya
462,840 5,172,033 11.2 Port Moresby
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Solomon
28,450 494,786 17.4 Honiara
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Vanuatu
12,200 196,178 16.1 Port Vila
Mikronesia
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Shirikisho la Mikronesia
702 135,869 193.5 Palikir
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Kiribati
811 96,335 118.8 Teinainano
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Marshall
181 73,630 406.8 Majuro
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Nauru
21 12,329 587.1 Yaren
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Mariana ya Kaskazini Marekani
477 77,311 162.1 Saipan
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Guam (Marekani)
549 160,796 292.9 Hagåtña
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Palau
458 19,409 42.4 Melekeok
Polynesia
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Samoa ya Marekani (Marekani)
199 68,688 345.2 Fagatogo, Utulei
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Cook (New Zealand)
240 20,811 86.7 Avarua
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Polynesia ya Kifaransa (Ufaransa)
4,167 257,847 61.9 Papeete
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Hawaii (Marekani)
29,311 1,211,537 42.75 Honolulu
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Niue (New Zealand)
260 2,134 8.2 Alofi
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Kisiwa cha Pasaka (Chile)
163,6 3,791 23,17 Hanga Roa
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Visiwa vya Pitcairn (Uingereza)
5 47 10 Adamstown
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Samoa
2,944 178,631 60.7 Apia
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Tokelau (New Zealand)
10 1,431 143.1
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Tonga
748 106,137 141.9 Nuku'alofa
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Tuvalu
26 11,146 428.7 Vaiaku
Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo 
Wallis na Futuna (Ufaransa)
274 15,585 56.9 Mata-Utu
Total 9,008,458 35,834,670 4.0

Tanbihi

Australia Na Pasifiki: Bara au la?, Jina, Eneo  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

Australia Na Pasifiki Bara au la?Australia Na Pasifiki JinaAustralia Na Pasifiki EneoAustralia Na Pasifiki JiolojiaAustralia Na Pasifiki HistoriaAustralia Na Pasifiki KandaAustralia Na Pasifiki Nchi na Maeneo ya Australia na Visiwa vya PasifikiAustralia Na Pasifiki TanbihiAustralia Na PasifikiBara

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Homa ya mafuaChama cha MapinduziNgiriUkristoRohoKitenziHuduma ya kwanzaKaswendeVasco da GamaDiniTendo la ndoaDhima ya fasihi katika maisha25 ApriliWhatsAppNominoVivumishi vya urejeshiMpira wa mkonoAbedi Amani KarumeKiambishi awaliHaki za wanyamaMnururishoHistoria ya Kanisa KatolikiBawasiriMsamiatiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaUnyenyekevuViwakilishi vya kumilikiWizara ya Mifugo na UvuviOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoBikiraMillard AyoNomino za jumlaOrodha ya Marais wa KenyaHurafaWizara za Serikali ya TanzaniaAsili ya KiswahiliMunguMadiniHisiaLatitudoUnyevuangaMasharikiVidonda vya tumboInstagramOrodha ya makabila ya TanzaniaKiarabuTanganyika (maana)MoyoMbooAdolf HitlerMapambano ya uhuru TanganyikaHistoria ya WapareDawa za mfadhaikoShangaziWilaya ya KinondoniDaktariOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaRita wa CasciaMarie AntoinetteUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaAgano la KaleLiverpool F.C.UkabailaMsituSteven KanumbaUpendoMamaTumbakuLigi Kuu Tanzania BaraMkoa wa LindiNomino za pekee🡆 More