Chile

Chile ni nchi ya Amerika Kusini.

Chile

Eneo lake ni kama kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki.

Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina.

Ni sehemu za Chile pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka (Rapa Nui), Kisiwa cha Salas y Gómez, Visiwa vya Juan Fernández (pamoja na kisiwa cha Robinson Crusoe), visiwa vya Desventuradas, Visiwa vya Ildefonso na visiwa vya Diego Ramirez.

Chile inadai ya kuwa sehemu ya bara la Antaktika ni eneo lake.

Chile
Ramani ya Chile.

Mji mkuu ni Santiago, yaani Mtakatifu Yakobo.

Jiografia

Chile ina urefu wa kilomita 4,200 kufuata pwani ya Pasifiki na milima ya Andes. Umbali huu ni kama kutoka Cape Town kwenda Dar es Salaam. Lakini upana wa wastani wa eneo lake ni kilomita 180 tu: sehemu nyembamba ya nchi ina upana wa kilomita 90, sehemu pana zaidi ina kilomita 240.

Nje ya maeneo yenye uwanja mwembamba wa pwani, nchi yote ni ya milima na mabonde. Sehemu kubwa ya nchi ina safu mbili za milima:

  • Andes katika mashariki na
  • Cordillera de la Costa (safu ya pwani) katika magharibi.

Katikati ya safu hizo mbili kuna bonde la kati (Valle Central) lenye makazi ya idadi kubwa ya wananchi na ardhi yenye rutuba kwa kilimo.

Kuelekea kusini kimo cha nchi hushuka hadi kufikia chini ya uwiano wa bahari. Milima ya safu ya pwani huonekana sasa kama visiwa.

Kaskazini mwa nchi hakuna bonde kubwa la kati. Nchi inapanda juu kutoka mwambao wa bahari hadi kuwa tambarare yenye kimo cha mita 1,000 - 1,500 inayoendelea mpaka mwanzo wa safu ya Andes.

Milima

Andes za Chile ni kati ya milima ya juu duniani: kuna vilele kadhaa juu ya mita 6,000.

Watu

Chile 
Atacama.

Wakazi wengi (85%) wanaishi mijini. Utafiti juu ya DNA yao unaonyesha kwa asilimia 52% hivi ina asili ya Ulaya, 43% ni ya Kiindio na 5% ni kutoka Afrika. Kwa jumla, wengi wana mchanganyiko wa damu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.

Upande wa dini, 66.6% ni Wakatoliki na 17% ni Waprotestanti. Asilimia 12.4 haina dini yoyote.

Tazama pia

Viungo vya nje

Chile 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Chile  Makala hii kuhusu maeneo ya Chile bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Chile JiografiaChile WatuChile Tazama piaChile Viungo vya njeChileAmerika Kusini

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UaminifuChatuVita ya Maji MajiUtataUgonjwa wa uti wa mgongoJumapiliMkoa wa LindiSaida KaroliUlayaUharibifu wa mazingiraJoyce Lazaro NdalichakoMkoa wa SingidaMshale (kundinyota)VisakaleUti wa mgongoPonografiaDuniaNgano (hadithi)MwalimuCleopa David MsuyaUlimwenguInsha ya wasifuWapareVidonda vya tumboUongoziAbedi Amani KarumeKondomu ya kikeJumuiya ya Afrika MasharikiMohamed HusseinUjerumaniPentekosteRadiMartin LutherKatibuOrodha ya Magavana wa TanganyikaFutiWanyama wa nyumbaniKiambishi awaliNdovuNdoaMchungaji mwemaMalariaUhindiUtoaji mimbaWachaggaMnyoo-matumbo MkubwaSamia Suluhu HassanHistoria ya IsraelMkoa wa NjombeHistoria ya RwandaAsili ya KiswahiliMwanza (mji)Mohamed Omary MchengerwaNyangumiSomaliaVirusi vya UKIMWIKenyaHarmonizeKidole cha kati cha kandoTungoMwaka wa KanisaChotaraHistoria ya AfrikaKata za Mkoa wa Dar es SalaamAlama ya uakifishajiNgw'anamalundiSaidi NtibazonkizaElimuYouTubeUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaTamthiliaKunguruMsamahaTamathali za semi🡆 More