Paka-kaya ni mnyama mdogo alaye nyama na ambaye amefugwa na binadamu tangu miaka maelfu.
Paka-kaya | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Paka-kaya | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Paka ni mwana wa familia ya Felidae wanaojumlisha paka pamoja na gwagu (paka-pori) na spishi kubwa kama simba, chui na duma.
Asili ya paka ni paka za porini (kwa hakika paka-jangwa, F. s. lybica) walioanza kutafuta chakula karibu na makazi ya watu wa kale na kuwazoea. Watu walipenda paka kwa sababu paka hushika panya na wanyama wengine wadogo wanaoonekana ni waharibifu katika makazi ya watu. Kwa hiyo paka waliendelea kwa muda mrefu katika mazingira ya kibinadamu kama wawindaji wa panya waliolishwa na watu wakipewa mabaki ya chakula pia. Katika mazingira ya mjini paka hufugwa mara nyingi kama mnyama kipenzi hapati tena nafasi ya kuwinda.
Kwa sababu ya kuishi karibu sana na binadamu, magonjwa ya paka huenda yakaambukizwa kwa binadamu. Paka huenda akawa na virusi, bakteria, fungi au hata vimelea kama chawa ambao wataambukizwa kwa binadamu. Maradhi huenda yakawa hayaonekani kwa paka lakini akiambukizwa binadamu huwa basi yanaonekana. Magonjwa haya ni kama salmonella, kujikunakuna (cat scratch disease) na toxoplasmosis. Ili kujikinga, yafaa paka apulizwe kwa dawa na pia kupelekwa kwa daktari wa wanyama mara kwa mara.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Paka-kaya, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.