Mji Moshi

Kwa maana tofauti ya jina hili angalia makala ya maana Moshi

Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Mji wa Moshi
Mji wa Moshi is located in Tanzania
Mji wa Moshi
Mji wa Moshi

Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania

Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E / -3.34000; 37.34000
Nchi Tanzania
Mkoa Kilimanjaro
Wilaya Moshi Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 221,733
Mji Moshi
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi mjini
Mji Moshi
Msikiti Mkuu wa Moshi

Wakazi

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huo una wakazi wapatao 184,292. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 331,733 .

Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanakwenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.

Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.

Hali ya hewa

Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

Utalii

Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.

Kampuni nyingi za utalii zimekuwa zikiendesha shughuli zake miaka na miaka. Shughuli kuu za utalii zikiwa ni kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda mbuga za wanyama kama vile Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ziwa Manyara.

Elimu

Mji wa Moshi una vyuo vikuu vinne:

  • MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) ya Morogoro
  • MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
  • KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
  • OUT (The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam

Utawala

Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.

Mandhari ya Moshi Mjini

Marejeo

Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2022) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Mji Moshi 
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya ya Hai 240,999 17 1,217
Wilaya ya Moshi Vijijini 535,803 32 1,300
Wilaya ya Moshi Mjini 331,733 21 63
Wilaya ya Mwanga 148,763 20 1,831
Wilaya ya Rombo 275,314 28 1,471
Wilaya ya Same 300,303 34 6,221
Wilaya ya Siha 139,019 17 1,217
Jumla 1,861,934 152 13,209
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai.
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro
Mji Moshi  Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania Mji Moshi 

Bomambuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiborloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto

Mji Moshi  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

Mji Moshi WakaziMji Moshi Hali ya hewaMji Moshi UtaliiMji Moshi ElimuMji Moshi UtawalaMji Moshi MarejeoMji Moshi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UchawiIfakaraVivumishi vya kuoneshaSaida KaroliNambaVivumishi vya kumilikiZuchuLigi Kuu Uingereza (EPL)KisononoRufiji (mto)Amri KumiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaEl NinyoRicardo KakaVokaliHaki za watotoAthari za muda mrefu za pombeMahakama ya TanzaniaUgonjwa wa kuharaKanisa KatolikiHoma ya mafuaFasihi simuliziMizimuKimara (Ubungo)Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Afrika KusiniTabianchiMichael JacksonDar es SalaamLatitudoUnyenyekevuMbuniUtumwaKitenzi kikuu kisaidiziNenoUfugajiKongoshoKhalifaMshororoMoyoOrodha ya milima ya TanzaniaKipindupinduSabatoOrodha ya Magavana wa TanganyikaWilaya ya ArushaMkoa wa SongweRaiaUmoja wa AfrikaVidonda vya tumboUkabailaSimba S.C.NduniWarakaMkoa wa MwanzaUenezi wa KiswahiliMshubiriWizara ya Mifugo na UvuviBaruaMkutano wa Berlin wa 1885TiktokMaandishiTanzaniaTovutiHektariMtaalaMwamba (jiolojia)WamasaiNuktambiliYesuOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoAmfibiaWabunge wa Tanzania 2020UfahamuSayansi ya jamiiSimba (kundinyota)Mahindi🡆 More