Pandemia (kutoka Kigiriki παν pan -ote + δήμος demos watu) inamaanisha uenezi wa ugonjwa wa kuambukiza katika eneo kubwa, kwa mfano bara au hata duniani kote.
Kwa kawaida uenezi wa ugonjwa huitwa "epidemia": neno hili lamaanisha kuongezeka kwa wagonjwa kwenye eneo au kikundi, tena katika kipindi fulani. Kama epidemia inapanuka kimataifa inafikia ngazi ya "pandemia".
Historia imehifadhi habari za pandemia mbalimbali. Kwa habari za kale sana si rahisi kuwa na uhakika ulikuwa ugonjwa gani uliosababisha vifo vilivyotajwa.
Lakini tangu zama za kati kuna habari za pandemia za tauni zilizoua milioni kadhaa za watu. Hasa pandemia ya tauni ya karne ya 14 inajulikana iliua watu milioni 25 yaani theluthi moja ya wakazi wa Ulaya wa siku zile.
Katika karne ya 20 ilikuwa hasa pandemia ya homa ya mafua iliyoitwa "influenza ya Kihispania" ambayo iliambukiza watu milioni 500 na kuua milioni 20-25 kote duniani kati ya miaka 1918 na 1920. Inakadiriwa ya kwamba kati yao laki kadhaa walikufa Afrika ya Mashariki.
Tangu mwaka 1980 pandemia ya UKIMWI imeendelea kuenea kote duniani na kuua takriban watu milioni 37 hadi sasa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) imeeleza pandemia kuwa na vigezo 3:
Si kila ugonjwa unaoua watu wengi unaweza kuitwa pandemia: lazima uwe ugonjwa wa kuambukizwa. Kwa mfano kansa inaua watu wengi lakini si pandemia kwa sababu kansa si ugonjwa wa kuambukiza.
Si kila ugonjwa mkali unaweza kuendelea kuwa pandemia. Maana kama ugonjwa ni mkali mno unaua wahanga wake haraka na hivyo kuzuia uenezi wake. Mfano mmojawapo ni homa ya Ebola ambayo ni kati ya magonjwa hatari zaidi, lakini haikuendelea kupitia ngazi ya epidemia.
Leo hii pandemia zinaenea hasa kwa kufuata njia za mawasiliano kwa eropleni. UKIMWI iliyokuwa tatizo la kieneo likaenea kwa njia ya utalii wa kimataifa kuwa ugonjwa unaopatikana kote duniani.
Wakati wa pandemia ya SARS mwaka 2002/2003 ilionekana ya kwamba katika Asia, yenye asili ya maambukizo ugonjwa ulienea kwa kasi ya wastani, ila huko Kanada idadi ilianza kuongezeka haraka - kutokana na kufika kwa watalii na wafanyabiashara waliorudi kwao kutoka Asia kwa ndege.
Tauni ilifika Ulaya kwa njia ya meli za biashara kutoka Asia.
Magonjwa yalienea hata zamani pasipo usafiri wa kisasa lakini uenezi ulikuwa wa polepole zaidi na mara nyingi jiografia ilizuia kufika kwa magonjwa fulani kwenye visiwa au ng'ambo ya milima mirefu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) imetunga mpango wa kujiandaa kwa kutokea kwa virusi mpya za homa ya mafua. Hapo imeeleza ngazi 6 za uenezi wa pandemia pamoja na mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na serikali za nchi husika.
Kipindi kabla ya pandemia:
Kipindi cha tahadhari ya pandemia:
Kipindi cha Pandemia:
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pandemia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Pandemia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.