San Marino

San Marino (kwa Kiitalia maana yake ni Mtakatifu Marino) ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani.

Eneo lake lote limo ndani ya mipaka ya Italia, kati ya wilaya za Rimini na Pesaro-Urbino, karibu na mwambao wa bahari ya Adria.

San Marino


San Marino
Mtazamo kutoka San Marino hadi bahari ya Adria.

Eneo lote la km² 61,19 ni la milima.

Historia

San Marino inatajwa kuwa jamhuri yenye umri mkubwa kuliko zote duniani. Ilianzishwa na Wakristo waliokimbia dhuluma ya Kaisari wa Roma Diokletiano wakitafuta kimbilio mlimani.

Kati yao, shemasi Marino na padri Leo ndio maarufu zaidi.

Tangu hapo imefaulu kudumisha uhuru wake. Ndiyo sababu tangu mwaka 2008 imeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Watu

San Marino ina wakazi 33,909 (2019) katika vijiji 9. Karibu wote (97.2%) ni waumini wa Kanisa Katoliki (jimbo la San Marino-Montefeltro) na wanaongea Kiitalia kwa lahaja ya Kiromagna.

Siasa

San Marino imetunza utaratibu wa serikali inayofanana na muundo wa jamhuri ya Roma ya kale. Serikali inaongozwa na watawala wawili ("Capitani Reggenti") wanaochaguliwa kwa muda wa miezi sita tu kama zamani konsuli wa Kiroma.

Bunge linaitwa Halmashauri Kuu ("Consiglio Grande e Generale") likichaguliwa kila baada ya miaka mitano. Halmashauri inateua pia kamati ya watu 12 ("Consiglio dei XII") inayotekeleza kazi ya mahakama.

Wananchi wote hukutana mara mbili kwa mwaka kama mkutano mkubwa wa "Arengo" wakiamua juu ya matamko na mapendekezo kwa serikali.

San Marino  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu San Marino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

AdriaBahariDunianiItaliaKiitaliaMwambaoPesaroRiminiUrbinoWilaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

NdoaMlongeHistoria ya TanzaniaFasihi andishiKiimboWabena (Tanzania)Upinde wa mvuaMorogoro VijijiniNangaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniLafudhiMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaRisalaBinadamuWema SepetuUajemi ya KaleAli Hassan MwinyiMkoa wa TaboraUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiMichezo ya watotoMnururishoBabeliMaajabu ya duniaSakramentiUtawala wa Kijiji - TanzaniaMaziwa ya mamaKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaOrodha ya vitabu vya BibliaIyumbu (Dodoma mjini)TeknolojiaSentensiSkeliKitenzi kishirikishiUgonjwa wa kuambukizaUgonjwa wa uti wa mgongoKanga (ndege)SarangaKata za Mkoa wa Dar es SalaamVita ya Maji MajiInsha ya wasifuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMichezoMbuBenki ya DuniaChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)Meta PlatformsFalsafaAdolf HitlerMizunguBurundiNomino za kawaidaMakabila ya IsraeliOrodha ya nchi za AfrikaWamasaiBahashaUkristo nchini TanzaniaBarua rasmiAfrika ya Mashariki ya KijerumaniHedhiTarbiaHistoria ya uandishi wa QuraniVivumishi vya jina kwa jinaKifua kikuuArusha (mji)Somo la UchumiIyungaTausiPhilip Isdor MpangoMilango ya fahamuMoyoTetemeko la ardhiMilaGhana🡆 More