Kilatini

Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule, vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili.

Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na hata leo istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini.

Kilatini
Nahau ya Kilatini ("Kukosa ni jambo la kibinadamu").

Historia

Kilatini 
Ramani ya uenezi wa lugha za Kirumi za leo zilizotokana na Kilatini.

Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi, kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k.

Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wiki.

Kilikuwa

Hadi leo Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya. Tena ni

Urithi wa Kilatini katika Kiswahili

Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.

Mifano:

Kilatini cha kisasa

Kilatini 
Systema Naturae ni kitabu maarufu kilichoandikwa mnamo mwaka 1735 kwa Kilatini na Carl Linnaeus. Ni msingi wa uainishaji wa kisayansi wa mimea na wanyama hadi leo

Kilatini kilikuwa na upanuzi mkubwa kuanzia karne ya 16; misingi ya sayansi ya kisasa ilijadiliwa katika Ulaya kwa Kilatini kilichokuwa lugha ya vyuo vikuu kote Ulaya. Katika karne ya 18 na 19 mataifa mengi yaliimarisha lugha zao na kuzitumia kwa ngazi zote za elimu. Lakini wataalamu wa Ulaya na Marekani waliendelea kutumia majina ya Kilatini kwa kutaja habari za kisayansi na kubuni majina mapya kufuatana na kanuni za Kilatini kwa kutaja vitu na viumbe vilivyotambuliwa na kuelezwa kisayansi. Kazi hii iliendelea hata wakati matumizi ya Kilatini kama lugha ya kujadiliana yalishafikia mwisho wake.

Katika karne ya 20 kulikuwa na harakati ya wapenzi wa lugha kuunda misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019.

Tazama pia

Viungo vya nje

Kilatini  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilatini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kilatini HistoriaKilatini Urithi wa katika KiswahiliKilatini cha kisasaKilatini Tazama piaKilatini Viungo vya njeKilatiniChuo kikuuElimuHistoriaLughaLugha ya kwanzaLugha ya piliShule

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KengeWilaya ya KigamboniSomo la UchumiSarangaMazingiraTanganyikaKitunda (Ilala)Mkoa wa KataviRitifaaUbungoJumuiya ya MadolaMafumbo (semi)ViunganishiLugha za KibantuNairobiTashihisiNgano (hadithi)Mkoa wa SongweGongolambotoEthiopiaKiraiBiblia ya KikristoMkoa wa RuvumaMuunganoDawatiMohamed Gharib BilalMadawa ya kulevyaOksijeniSayariJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaNdoo (kundinyota)DiniOrodha ya viwanja vya michezo TanzaniaBarabaraKichochoKukuKanga (ndege)MJJulius NyerereChemsha BongoMaigizoStafeliBenjamin MkapaAzimio la ArushaLady Jay DeeLugha rasmiNgeliLigi Kuu Tanzania BaraViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)TamthiliaSkeliUhifadhi wa fasihi simuliziSamakiMaghaniUwanja wa Taifa (Tanzania)Muungano wa Madola ya AfrikaKitenzi kikuu kisaidiziMkoa wa ManyaraHussein Ali MwinyiMwenge wa UhuruMashuke (kundinyota)Tulia AcksonMariooHistoriaImaniKupakua (tarakilishi)NyotaVirusi vya CoronaMshororoUchumiMkoa wa LindiWadatoga🡆 More