Vuguvugu La Uarabuni

Vuguvugu la Uarabuni au Vuguvuru la Kiarabu, Mchipuko wa Uarabuni (Kiarabu: الربيع العربي ‎, kutoka kiing.

Vuguvugu La Uarabuni
       Serikali imeondolewa madarakani       Vurumai endelevu za raia wanaodai mabadiliko ya kiserikali       Maandamano na hatimaye mabadiliko ya kiserikali
      Maandamano makubwa kabisa       Maandamano madogo       Maandamano nje ya ulimwengu wa Kiarabu

Watawala waliolazimika kutoka madarakani huko nchini Tunisia, Misri (mara mbili), Libya na Yemen. Machafuko ya kiraia yalitokea huko nchini Bahrain na Syria. Maandamano makubwa katika historia yalitokea huko nchini Algeria, Iraq, Jordan, Kuwait, Morocco na Sudan. Maandamano madogo yalitokea huko nchini Mauritania, Omani, Saudia, Jibuti, Sahara ya Magharibi na Palestina. Kulikuwa na maandamano kiasi kutoka katika nchi ambazo sio sehemu ya Ulimwengu wa Waarabu kama vile Uajemi na Israel.

Kulikuwa na mikinzano huko mipakani mwa nchi ya Israel, na maandamano ya Wakhuzestan wachache wa Kiarabu uliyotokea mwaka 2011. Huko Mali, wapiganaji wa Kituareg wakati wanarudi kutoka katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Libya walichochea mzozo uliotafsiriwa kama sehemu ya "Vuguvugu la Kiarabu"" kwa upande wa nchi za Afrika Kaskazini. Mikinzano ya vikundi vya kimadhehebu iliyotokea huko Lebanoni ilionekana kuchochewa na machafuko ya Syria hivyo basi imechukuliwa kama Vuguvugu la Kiarabu.

Maandamano haya yaliambatana na kampeni za kupinga mambo mbalimbali, migomo, mashambulizi, matembezi ya miguu kwa masafa marefu, vilevile matumizi ya mitandao ya kijamiii kwa kuhamasisha na kuongeza ufahamikaji wa suala lenyewe katika jamii husika katika ulimwengu wa intaneti..

Vuguvugu nyingi za Kiarabu ziliambatana na fujo za kila aina hasa kwa kufuatia mamlaka kutaka kuzuia harakati hizi. Kwa maana hiyo, waandamanaji nao hawakubali kurudi nyuma katika suala zima la kupigania hicho walichokuwa wanakiamini. Msemo mkubwa uliokuwa unatumiwa na wagomaji katika ulimwengu wa Kiarabu ulikuwa Ash-sha`b yurid isqat an-nizam ("watu wanataka kuuangusha utawala wa kidhalimu").

Baadhi ya watafiti wamelifananisha suala hili kama zile vuguvugu za mapinduzi yaliyotokea mwaka 1989 huko Ulaya ya Mashariki au Mapinduzi ya 1848 katika majimbo ya Ujerumani.

Kuanza kwa vuguvugu

Mfululizo wa migomo na maandamano katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ulianzia nchini Tunisia mnamo tarehe 18 Desemba 2010 kwa kufuatia Mohamed Bouazizi kujilipua na mafuta ya taa kwa kupinga manyanyaso na rushwa kutoka kwa maafisa wa polisi. Maandamano haya yaliamsha fujo nyengine nje ya mji ambao tukio hili limetokea na kupelekea fujo na maandamano katika nchi mbalimbali za Kiarabu.

Matukio

Safu hii inaonesha baadhi ya mifululizo ya matukio yaliyotokana na vuguvugu la kwanza la Tunisia kisha kuhamia nchi nyingine za Uarabuni.

  • Desemba 18, 2010: Vuguvugu La Uarabuni  Tunisia, maandamano yanaanza, baada ya Mohammed kujilipua na moto.
  • Desemba 29, 2010: Vuguvugu La Uarabuni  Algeria, maandamano yanaanza.
  • Januari 13 16, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya, waandamanaji walidhibitiwa.
  • Januari 14, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Jordan, maandamano yanaanza.
  • Januari 14, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Tunisia, serikali imeanguka.
  • Januari 17, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Oman maandamano madogo yalianza.
  • Januari 18, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Yemen, maandamano yanaanza.
  • Januari 25, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Egypt, maandamano yanaanza.
  • Januari 26, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Syria, mtu mmoja kajitia moto.
  • Januari 28, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Palestine, maandamano yanaanza.
  • Januari 28, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Djibouti maandamano madogo yalianza.
  • Januari 30, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Sudan, maandamano yanaanza.
  • Februari 1, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Jordan, serikali imeondolewa.
  • Februari 10, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Egypt, Rais, na makamu wake wamekabidhi madaraka.
  • Februari 10, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Iraq maandamano madogo yalipangwa. Nouri al-Maliki anatangaza ya kwamba uchaguzi ujao hatogombea.
  • Februari 11, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Egypt, Rais Hosni Mubarak anajiuzuru.
  • Februari 14, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Bahrain, maandamano yanaanza.
  • Februari 15, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya kivumbi cha maanadamano kinaanza tena.
  • Februari 19, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Kuwait, maandamano yanaanza.
  • Februari 20, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Morocco, maandamano yanaanza.
  • Februari 25, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Mauritania, maandamano yanaanza.
  • Februari 27, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Lebanon, maandamano yanaanza.
  • Machi 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Djibouti, maandamano yanaisha.
  • Machi 3, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya kiongozi Muammar Gaddafi anapoteza nguvu ya kuingoza Libya.
  • MachI 5, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya Kikosi cha Anga cha Libya chaanza kulipua miji mikubwa. Upinzani ukalazimika kusanda.
  • Machi 11, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Saudi Arabia, maandamano yanaanza.
  • Machi 15, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Syria, maandamano yanaanza.
  • March 19, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya, bombing by foreign air forces began.
  • Aprili 15, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Iran, maandamano yanaanza.
  • Aprili 18, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Iran, maandamano yanaisha.
  • Mei 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Oman, maandamano yanaisha.
  • Mei 15, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Israel, maandamano yanaanza.
  • Juni 5, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Israel, maandamano yanaisha.
  • Agosti 3, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Egypt, Kesi ya Hosni Mubarak inaanza.
  • Agosti 21-22, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya Wapinzani nao wameingia mji mkuu Tripoli.
  • Septemba 29, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Saudi Arabia, chaguzi zilifanyika.
  • Oktoba 20, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya mji wa Sirte, Muammar Gaddafi anauawa na waasi.
  • Oktoba 23, 2011: Vuguvugu La Uarabuni  Libya, vita ya wenyewe kwa wenyewe inaisha.

Marejeo

Tags:

KiarabuKiing.

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WokovuMusaHoma ya manjanoMwislamuMadhehebuSemiKylian MbappéMfumo wa homoniShukuru KawambwaDivaiViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)Uhalifu wa kimtandaoMwanamkeWilaya ya KaratuKifaruMajeshi ya Ulinzi ya KenyaWanyakyusaUtumbo mwembambaDolar ya MarekaniDini asilia za KiafrikaKinjikitile NgwaleShaaban (mwezi)DhamiraAlama ya uakifishajiMkanda wa jeshiVitenzi vishiriki vipungufuMwarobainiBibliaAdhuhuriVivumishi vya kuoneshaUandishi wa ripotiDubaiAnwaniJumuiya ya Afrika MasharikiFamiliaPamboBungeMajiMapafuKiambishi awaliKukuBinamuNimoniaZama za MaweMoses KulolaUkuaji wa binadamuMadiniMkoa wa LindiMamaMbooNadhariaNyanda za Juu za Kusini TanzaniaAndalio la somoChumba cha Mtoano (2010)Arsenal FCUjamaaAlfabetiShinaUsawa (hisabati)Sanaa za maoneshoHistoria ya Kanisa KatolikiMasafa ya mawimbiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuMnazi (mti)UtamaduniPichaOrodha ya Marais wa MarekaniNgono zembeTanganyika (ziwa)WayahudiMkoa wa DodomaKiharusi🡆 More