Shaaban (kwa Kiarabu: شعبان, sha‘bān) ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiislamu.
Inafuata Rajabu ikifuatwa na Ramadan.
Ilhali ni mwezi kabla ya Ramadani ni pia wakati ambako mwanzo wa saumu unatangazwa.
Siku ya 15 ya Shaaban inajulikana kama "usiku wa kumbukumbu" au Laylatul Bara-at lakini adhimisho hilo lina utata.. Kufuatana na hadith Mtume Muhammad alitaja tarehe hiyo kuwa siku maalumu, hivyo kuna Waislamu wanaoamini ya kwamba usiku huo una baraka za pekee. Wengine hukaa usiku huo pamoja wakisoma Korani na kushiriki katika sala za pekee. Wengine wanapinga ibada hizo.
Washia Ithna ashari husheherekea tarehe 15 Shaaban kama sikukuu ya kuzaliwa kwa imamu wao wa 12 na wa mwisho, Muhammad al Mahdi.
Ilhali kalenda ya Kiislamu ni kalenda ya mwezi miezi yake huanza wakati wa kutazamwa kwa hilali ya mwezi mpya. Pia kwa sababu mwaka wa mwezi ni mfupi kuliko mwaka wa jua basi tarehe za Shaaban zinapita kwenye majira. Tarehe zake kwa miaka ya karibu ni takriban:
Mwaka baada ya Hijra | Siku yake ya kwanza katika kalenda ya BH / AD) | Siku yake ya mwisho katika kalenda ya BH / AD |
---|---|---|
1437 | 8 Mei 2016 | 5 Juni 2016 |
1438 | 28 Aprili 2017 | 26 Mei 2017 |
1439 | 17 Aprili 2018 | 15 Mei 2018 |
1440 | 6 Aprili 2019 | 5 Mei 2019 |
1441 | 25 Machi 2020 | 23 Aprili 2020 |
1442 | 14 Machi 2021 | 12 Aprili 2021 |
Tarehe za Shaaban baina ya 2016 BK na 2021 BK |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Shaaban (mwezi), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.