Bahari ya Barents (Kinorwei: Barentshavet; Kirusi: Баренцево море Barentsevo More) ni tawi la Bahari ya Aktiki, na iko kaskazini kwa Urusi, Norwei na funguvisiwa la Svalbard pamoja na Kisiwa cha Dubu.
Visiwa vya Novaya Zemlya vinaitenganisha na Bahari ya Kara.
Eneo lake ni la km² 1,424,000. Jina limetokana na baharia Mholanzi Willem Barents.
Sehemu hii ya bahari haina kina kirefu, kwa wastani ni mita 230 pekee. Kiuchumi ni muhimu kwa uvuvi na uchumbaji wa gesi na mafuta ya petroli.
Hata kama ni sehemu ya Bahari ya Aktiki, inaweza kupitiwa na meli karibu mwaka wote kwa sababu inapokea maji ya vuguvugu kutoka Mkondo wa Ghuba wa Bahari Atlantiki unaoishia hapa. Maji ya vuguvugu ni msingi kwa kuota kwa planktoni ambayo ni lishe kwa aina nyingi za samaki.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bahari ya Barents, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.