Eire Kaskazini ni eneo la kaskazini mashariki la kisiwa cha Ireland ambalo limo katika Ufalme wa Muungano, tofauti na sehemu kubwa ya kisiwa hicho iliyopata uhuru mwaka 1921.
Ni kwamba baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.
Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.
Ndani yake, mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Ireland ya Kaskazini zilirudishiwa mabunge yao ya pekee.
Kadiri ya sensa ya mwaka 2021, wakazi ni 1,903,100 wanaoishi katika km2 14,130.
Wengi wao ni Wazungu (96.6%), wakifuatwa na Waafrika (0.6%), Wahindi (0.5%) na Wachina (0.5%).
Kiingereza ni lugha mama kwa asilimia 95.4 za wakazi.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo (76.6%), hasa Wakatoliki (42.3%) na Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali (37.3%). Wenye dini tofauti ni 1.3%, wakati 17.4% hawana dini yoyote au hawakujibu swali.
|url-access=
ignored (help)Angalia mengine kuhusu Northern Ireland kwenye miradi mingine ya Wiki: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
OpenStreetMap has geographic data related to: Eire Kaskazini |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Eire Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Eire Kaskazini, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.