Mzungu

Mzungu ni neno la Kiswahili kumtaja mtu anayeonekana ametoka Ulaya.

Mzungu
Wote Watu wa Ulaya lakini si wazungu! (Waingereza wazawa mbunge Diane Abbott, mwigizaji wa filamu Adewale Akinnuoye-Agbaje, waziri Paul Boateng, modeli Naomi Campbell, mwimbaji Craig David)

Neno la kumaanisha rangi ya mtu

Ni neno ambalo zaidi linalenga rangi ya mtu na kumtofautisha yule anayetajwa na Mwafrika, Mwarabu, Mhindi au Mchina.

Si neno kamili sana kwa sababu watu wanaoitwa Wazungu wanaweza kutokea kila sehemu ya dunia; Wamarekani weupe huitwa Wazungu na pia makaburu kutoka Afrika Kusini, Wakenya weupe na pia Waaustralia. Vilevile mtu kutoka nchi za Ulaya ya Kusini kama Hispania au Ugiriki anaweza kusababisha wasiwasi kama yeye ni Mzungu au Mwarabu kwa sababu wengi wao hufanana na watu wa Afrika ya Kaskazini.

Ikitumiwa kwa maana ya "watu wa Ulaya" inaeleweka kwa jumla isipokuwa siku hizi nchi za Ulaya hujaa watu ambao wenyewe au mababu wao walihamia huko kutoka pande nyingi za dunia jinsi inavyoonekana kwenye nyuso yao.

Neno la kutaja sifa ya mbari pamoja na jiografia

Kiasili neno lilijitokeza wakati ambako watu waliweza kuamini ya kwamba kila sehemu ya dunia ilikuwa na rangi yake. Kwa namna hiyo inafanana na maneno katika lugha nyingine kwa mfano "negroe/negre/Neger" katika lugha za Ulaya kwa watu wanaoonekana kama wenye asili ya Kiafrika. Haina dharau ndani yake kama neno la Kiarabu "abdi" linalotaja watu weusi pamoja na watumwa.

Kizungu kwa lugha

Neno "Kizungu" latumiwa mara nyingi kwa maana ya lugha ya Kiingereza, lakini wakati wa ukoloni wa Ujerumani katika Tanzania bara ("Afrika ya Mashariki ya Kijerumani") lilitaja pia Kijerumani.

Asili ya neno

Asili ya neno haijulikani kikamilifu.

Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katika Kiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katika kamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yake mnamo mwaka 1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile: 1) kitu cha ajabu au cha kushangaza, 2) mbinu ya kujiondoa katika tatizo, 3) aina ya muhogo, 4) silika au akili ya wanyama.

Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".

Wengine wamehisi kwa utani ya kwamba kuna uhusiano na kitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutaja tabia ya wapelelezi, wamisionari na wafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaa mahali pamoja bali walizungukazunguka kote Afrika.

Marejeo

Tags:

Mzungu Neno la kumaanisha rangi ya mtuMzungu Neno la kutaja sifa ya mbari pamoja na jiografiaMzungu Kizungu kwa lughaMzungu Asili ya nenoMzungu MarejeoMzunguKiswahiliUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Tungo sentensiIbadaAunt EzekielIntanetiStephane Aziz KiKataYouTubeUfugaji wa kukuNyumbaMagonjwa ya kukuRufiji (mto)Steve MweusiUongoziIsimuMtandao wa kompyutaBiashara ya watumwaMichoro ya KondoaSimbaMkoa wa MbeyaUtataArusha (mji)MandhariSikukuuOrodha ya nchi za AfrikaKabilaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarNyasa (ziwa)AsiliMamba (mnyama)Azimio la ArushaMaana ya maishaNathariKiambishi tamatiNyotaLenziSamakiOrodha ya miji ya TanzaniaKiboko (mnyama)AntibiotikiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuJinaUlayaMkataba wa Helgoland-ZanzibarNileFalme za KiarabuWimboWaluguruMkwawaMkoa wa ManyaraDamuUkoloni MamboleoNguzo tano za UislamuUrusiVita ya Maji MajiKitabu cha Yoshua bin SiraNyokaOrodha ya Marais wa UgandaMtotoMkoa wa NjombeTabianchi ya TanzaniaViwakilishiBikiraAgano JipyaKiburiLugha ya kwanzaNomino za pekeeFasihi andishiMimba kuharibikaPapaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiHistoria ya WokovuNgiriKata za Mkoa wa Dar es SalaamAthari za muda mrefu za pombeNikki wa PiliUwanja wa Taifa (Tanzania)🡆 More