Umoja wa Ulaya (kifupisho: EU) ni muungano wa kisiasa na wa kiuchumi wa nchi 27 za Ulaya, baada ya Ufalme wa Muungano kujitoa tarehe 31 Januari 2020, tukio la kwanza la namna hiyo.
Kibulgaria: Европейски съюз Kicheki: Evropská unie Kidenmark: Den Europæiske Union Kieire: An tAontas Eorpach Kiestonia: Euroopa Liit Kifaransa: Union européenne Kifini: Euroopan unioni Kigiriki: Ευρωπαϊκή Ένωση Kihispania: Unión Europea Kiholanzi: Europese Unie Kihungaria: Európai Unió Kiingereza: European Union Kiitalia: Unione Europea Kijerumani: Europäische Union Kikroatia: Europska unija Kilatvia: Eiropas Savienība Kilituanya: Europos Sąjunga Kimalta: Unjoni Ewropea Kipoland: Unia Europejska Kireno: União Europeia Kiromania: Uniunea Europeană Kislovakia: Európska únia Kislovenia: Evropska Unija Kiswidi: Europeiska unionen | |
Ulianzishwa mwaka 1991 juu ya msingi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya.
Shabaha kuu zilikuwa kujenga uchumi wa pamoja, kuboresha maisha ya watu wa Ulaya na kuzuia vita kati ya nchi za Ulaya.
Nchi 19 za Umoja huo hutumia pesa moja ya Euro.
Nchi nyingi za Umoja zimepatana kufungua mipaka yao bila vizuizi kwa wakazi wote.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ilibadilisha jina lake mwaka 1992 kufuatana na mikataba ya Maastricht kuwa Umoja wa Ulaya.
Nchi wanachama zilipatana kujenga siasa ya pamoja ya kiuchumi, kifedha, kisheria na katika mambo ya nje.
Mapatano ya Schengen ilifungua mipaka ili wakazi wa nchi hizo waweze kusafiri bila pasipoti wala vibali.
Nchi 10 tena zilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004. Mbili zaidi ziliingia 2007 na Kroatia mwaka 2013.
Jumla ya wakazi ni milioni 447 (mwanzoni mwa 2020), sawa na 5.8% za watu wote duniani. Kuna miji 15 yenye watu zaidi ya milioni moja kila mmojawapo, kuanzia Paris ambayo inazidi milioni 10.
Upande wa lugha, lugha rasmi ni 24, lakini lugha inayotumika zaidi ni Kiingereza, kinachoweza kuzungumzwa na 51% za wakazi wote, ingawa ni lugha ya kwanza ya 1% tu. Lugha nyingine ambazo ni za kwanza kwa wananchi wengi ni: Kijerumani (18%), Kifaransa (13%) na Kiitalia (12%). Pia kuna lugha 150 hivi za kieneo.
Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo (71.6%), hasa Wakatoliki (45.3%), Waprotestanti 11.1% na Waorthodoksi 9.6%. Waislamu ni 1.8%. Wafuasi wa dini nyingine ni 2.6%. Wengine 24% hawana dini au ni Wakanamungu.
Kila mtu mwenye uraia wa nchi ya Umoja anaruhusiwa kuhamia nchi yoyote nyingine na kufanya kazi au biashara huko bila vibali vya pekee.
Vilevile bidhaa zote zinazotengenezwa kote katika Umoja wa Ulaya zinaweza kuuzwa katika kila nchi. Hii ni sababu ya kuwa na sheria za pamoja zinazotawala masharti ya bidhaa na uzalishaji.
Halmashauri hii ni mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama. Wanakutana mara mbili kwa mwaka na kutoa maazimo muhimu.
Nafasi ya uraisi hubadilika kila baada ya miezi 6. Ufini ilishika uraisi kati ya Julai 2006 hadi Desemba 2006, ikafuatiliwa na Ujerumani tangu Januari hadi Juni 2007.
Katika baraza hizi mawaziri ya Kilimo, Sheria, Mambo ya Nje hukutana na kupanga siasa ya pamoja.
Hii ni kamati ya utawala inayotekeleza maazimio ya Halmashauri na bunge. Kuna makamishna 24 na mwenyekiti. Inaelekea kuwa serikali lakini haina madaraka ya serikali bado.
Bunge la Ulaya lina wabunge 751 wanaochaguliwa na wananchi kila baada ya miaka mitano.
https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/2/2c/EU_PESCO_map.svg
Tovuti rasmi:
Mandhari na data:
Taarifa:
Misaada ya kufundishia:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Umoja wa Ulaya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Umoja wa Ulaya, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.