Esa

ESA ni kifupi cha Kiingereza cha European Space Agency (Mamlaka ya Usafiri wa Angani ya Ulaya).

Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1975 na nchi 10 za Umoja wa Ulaya.

Esa
Mfano wa roketi ya Ariane 1 inayotumiwa na ESA
Esa
Kituo cha kusimamia operesheni kwenye anga-nje huko Darmstadt

Wajibu wake ni kuratibu miradi ya nchi za Ulaya ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. Shabaha ni hasa kuendeleza juhudi za nchi za Ulaya katika teknolojia ya angani iliyokuwa nyuma sana kulingana na kazi za Marekani na Urusi wakati ule.

Mwaka 2014 kulikuwa na nchi wanachama 20, na kati ya hizo kuna nchi 18 wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na Uswisi na Norwei. Kufuatana na katiba yake, ESA inalenga shabaha zisizo za kijeshi pekee.

ESA inashirikiana kwa karibu na Umoja wa Ulaya na taasisi husika za kitaifa, hasa za Ufaransa na Ujerumani.

Katibu Mkuu wa ESA ni Mfaransa Jean-Jacques Dordain.

Ofisi na vituo vya EAS

  • Darmstadt, Ujerumani: Kituo cha kusimamia operesheni kwenye anga-nje (European Space Operations Centre ESOC)
  • Paris, Ufaransa: Ofisi Kuu
  • Noordwijk, Uholanzi: Taasisi ya utafiti na teknolojia ya usafiri wa anga-nje
  • Cologne, Ujerumani: Kituo cha wanaanga (European Astronaut Centre)
  • Oberpfaffenhofen, Ujerumani: ESA Business Incubation Centre (BIC)
  • Frascati, Italia: Taasisi wa utafiti wa anga-nje
  • Villafranca del Castillo, Villanueva de la Cañada, Hispania: Paoneaanga pa Ulaya
  • Kourou, Guyana ya Kifaransa: Kiwanja cha roketi ambako roketi nyingi za Kiulaya zinarushwa
  • Kiruna, Uswidi: Kituo cha Ulaya cha utafiti wa hali ya kimo cha juu na graviti

ESA ina pia ofisi za mawasiliano katika Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ubelgiji. Mwaka 2013 kulikuwa na wafanyakazi wa ESA 2250.

Viungo vya nje

Esa 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

1975KiingerezaUmoja wa Ulaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uhakiki wa fasihi simuliziSikukuu za KenyaTendo la ndoaAfrika Mashariki 1800-1845Orodha ya milima mirefu dunianiNyukiVielezi vya namnaWameru (Tanzania)Simba (kundinyota)Wabunge wa Tanzania 2020Dhima ya fasihi katika maishaHistoria ya AfrikaMoses KulolaBahashaMajiUbaleheMazingiraKiunguliaOrodha ya Marais wa KenyaLionel MessiUingerezaBendera ya ZanzibarUhifadhi wa fasihi simuliziWarakaUtumwaBungeTungoKimara (Ubungo)Mtakatifu PauloMwakaNembo ya TanzaniaAlama ya uakifishajiAlama ya barabaraniLahajaNgono zembeWahadzabeMwanaumeNgeliNguruwe-kayaMkoa wa SingidaSteve MweusiWahayaCristiano RonaldoAndalio la somoKitenzi kikuu kisaidiziMmeaLugha za KibantuNomino za jumlaUzazi wa mpangoWaluguruMkoa wa TaboraUkristoFananiUtumbo mpanaFonolojiaPemba (kisiwa)vvjndMusaIsimujamiiNamba za simu TanzaniaWilaya ya TemekeMapinduzi ya ZanzibarKifaruVita Kuu ya Pili ya DuniaVitenzi vishiriki vipungufuMsituNafsiWamasaiMzeituniMatiniLady Jay DeePijiniSiriWilaya ya NyamaganaStashahadaKiarabu🡆 More