Paoneaanga

Paoneaanga (pia: kituo cha nyota, kituo cha astronomia; kwa Kiingereza: astronomical observatory) ni taasisi ya kuangalilia anga na magimba yake kama vile jua, mwezi, nyota, sayari, kometi au galaksi.

Paoneaanga
Paoneaanga pa Griffith Observatory mjini Los Angeles, California. Darubini ziko chini ya kuba zinazofunguliwa wakati wa kutazama anga

Kwa kawaida ni jengo lenye darubini kubwa. Mara nyingi hujengwa juu ya mlima au mbali na miji kwa kusudi la kupunguza athari za machafuko wa hewa au wa nuru za makazi. Ni muhimu kupunguza athari zinazoleta ugumu wa kuona vema mwanga hafifu wa nyota.

Kabla ya kugunduliwa kwa darubini, kulikuwa na majengo maalumu ya kuangalia hasa mahali ambako Jua au nyota fulani iliweza kutazamiwa kuonekana siku maalumu na hii ilikuwa muhimu kwa kukadiria kalenda.

Siku hizi kazi ya paoneanga duniani inasaidiwa na kupanushwa na darubini kwenye anga-nje.

Paoneaanga Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paoneaanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Paoneaanga
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wiki Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano

Tags:

AngaGalaksiGimba la anganiJuaKiingerezaKometiMweziNyotaSayariTaasisi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

AWanyamaporiNgano (hadithi)KonsonantiClatous ChamaAli KibaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiWamasaiRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMajira ya mvuaMoyoRayvannyMkanda wa jeshiJumuiya ya MadolaBarua pepeMnyoo-matumbo MkubwaMachweoDubaiKanga (ndege)PombeNguruweKigoma-UjijiVivumishi vya -a unganifuNikki wa PiliMuungano wa Tanganyika na ZanzibarUchaguziSimbaBiasharaBaraza la mawaziri TanzaniaTarafaMaandishiMaambukizi nyemeleziUtendi wa Fumo LiyongoNdiziKitenziUharibifu wa mazingiraMaishaArsenal FCMkoa wa RukwaSamia Suluhu HassanKiarabuChama cha MapinduziNg'ombeMeliUwanja wa Taifa (Tanzania)VichekeshoDamuLiverpool F.C.NgeliTupac ShakurMimba za utotoniTarakilishiMbuga za Taifa la TanzaniaChakulaUjimaMnyamaMkoa wa NjombeAsili ya KiswahiliUfugajiSheriaTovutiShukuru KawambwaLady Jay DeeWanyakyusaMkoa wa KageraKoroshoMisimu (lugha)Orodha ya Magavana wa TanganyikaTabata🡆 More