Brahmagupta (Kisanskrit: ब्रह्मगुप्त)) (597–668 BK) alikuwa Mhindi mtaalamu wa Hisabati na astronomia anayekumbukwa kwa maandishi yake kuhusu fani hizo mbili.
Alikuwa msimamizi wa paoneaanga mjini Ujjain (Madhya Pradesh).
Brahmagupta alikuwa mwanahisabati wa kwanza anayejulikana kutunga sheria za kupiga hesabu kwa kutumia sifuri. Alitunga pia sheria za hesabu kwa namba hasi.
Katika fani ya astronomia alipinga mafundisho ya siku zake kuwa dunia ni tambarare akasisitiza ni tufe. Pia alipinga mafundisho kuwa mwezi uko mbali kuliko jua akaonyesha kuwa sharti mwezi uwe karibu zaidi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Brahmagupta, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.