Wiki Foundation ni shirika lisilo la kiserikali lililopo Marekani linaloendesha mradi wa Wikipedia pamoja na miradi mingine.
Shabaha yake ni usambazaji wa elimu huria inayopatikana bure kwa watu wote kwa njia ya mtandao. Lilianzishwa na Jimmy Wales mwaka 2001. Shirika linaendeleza maendeleo ya programu huria za wikiwiki zinazomruhusu msomaji si kusoma tu bali kuandika na kuhariri vilevile.
Kwa ujumla karibia miradi yote ya Wiki Foundation si ya kibiashara na maudhui yote yaliyomo katika miradi hiyo hutungwa na wachangiaji wengi wanaojitolea bila malipo kutoka karibia pande zote za Dunia.
Mapato ya shirika hutokana na michango ya watu binafsi. Makampuni makubwa kama Amazon na Google yamewahi kutoka zawadi za dolar milioni, na mfadhili Georg Soros alituma pia zawadi ya dolar milioni 2 .
Mnamo mwaka 2018/2019 mapato ya taasisi yalifikia dolar milioni 120 ilhali matumizi yake yalikuwa milioni 91.
Miradi mingine ya Wiki Foundation ukiacha ule wa Wiki ni pamoja na Wikamusi (Wiktionary), Wikiquote, Wikisource, Wikinews, Wikibooks, Wikiversity, Wiki Commons na Meta-Wiki.
Shirika hili haliangalii yaliyomo kama makala ya Wikipedia ambayo hutungwa na jumuiya za watumiaji katika lugha zinazofikia karibu 200.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wiki Foundation kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Wiki Foundation, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.