Galenos

Galenos wa Pergamon (pia Galen; 129 – mnamo 216) alikuwa tabibu na mwanafalsafa Mgiriki mashuhuri katika Dola la Roma.

Anakumbukwa kwa uchunguzi wa mambo ya tiba aliofanya na nadharia zake kuhusu afya na magonjwa. Nadharia zake ziliathiri tiba ya nchi za Ulaya na za Waislamu kwa miaka 1000 hadi mwisho wa enzi ya kati.

Galenos
Galen

Maisha

Galenos 
Galenou Apanta, 1538

Galenos alizaliwa Pergamon (leo hii: Bergama katika Uturuki), mji wa Ugiriki ya Kale ambao ulikuwa na hekalu muhimu la Asklepios aliyeheshimiwa kama mungu wa tiba.

Baba yake Nikon alikuwa msanifu akamfundisha falsafa, hisabati na sayansi.

Tangu mwaka 146 Galenos alijishughulisha na tiba hasa akaisoma alipohudumia wagonjwa kwenye hekalu la Asklepios. Akaedelea kusafiri hadi Aleksandria wa Misri iliyokuwa kitovu cha elimu ya tiba katika Dola la Roma na mahali pa pekee ambako matabibu waliruhusiwa kufanya utafiti kwenye maiti za watu. Hapa alipata pia nafasi ya kusoma mengi katika maktaba mashuhuri ya Aleksandria.

Mwaka 158 alirudi Pergamon akaajiriwa na kuhani mkuu wa Asia kama tabibu wa wapigaji upanga wake. Galenos alijifunza mengi kutokana na kutibu vidonda na majeruhi; katika maandiko yake aliita kidonda "dirisha la kutazama ndani ya mwili". Alifaulu kwa sababu katika kipindi chake walikufa wajeruhiwa 5 tu, wakati kwenye kipindi cha mtangulizi wake zaidi ya wapiganaji 60 walikufa.

Mwaka 160 alihamia Roma na baada ya kumponya mwanafalsafa mashuhuri Eudemos wa Pergamon alikuwa tabibu wa makabaila wa Roma. Ugonjwa wa tauni ulipoenea mjini alikimbia Roma mwaka 166 akarudi Pegamon. Mwaka 168 aliombwa na Kaisari Marcus Aurelius arudi Italia akawa mshauri na tabibu wa mtoto wa Kaisari na baadaye wa Kaisari Septimius Severus.

Galenos alikufa Roma mnamo mwaka 216.

Mafundisho yake

Galenos aliacha mafundisho yake katika vitabu 16 vya "Methodi medendi" (mbinu za kutibu). Hapa anafundisha ya kwamba yote yanayotokea au kuonekana yana kusudi lake.

Alikubali mafundisho ya Empedokles kuhusu elementi 4 za moto, ardhi, hewa na maji zinazounda vitu vyote. Hizi elementi zinalingana na viowevu 4 ndani ya mwili (damu, belghamu, nyongo njano na nyongo nyeusi). Hizi tena zinalingana na tiba 4 za joto, baridi, bichi na kavu.

Katika mafundisho ya Galen mwanadamu ni umoja wa mwili na roho. Ndani ya umoja huu uwiano wa viowevu na tabia zote 4 ni muhimu.

Kutokana na mafundisho hayo aliona ya kwamba kila dawa linaongeza au kupunguza tabia na viowevu mwilini. Alitofautisha madawa ya msingi (yenye tabia 1), madawa ya maungano (yenye tabia 2) na madawa ya pekee.

Kwenye madawa alitofautisha tena kutokana na ukali:

  1. . isiyoonekana sana
  2. . inayoonekana
  3. . kali kiasi, inaweza kuleta hasara kiasi
  4. . kali sana, inaleta hasara kwa afya

Galen aliongeza elimu yake kwa kuchunguza miili ya wanyama aliyoikata na kutazama. Kukata miili ya kibinadamu kwa uchunguzi kulipigwa marufuku katika Dola la Roma.

Maandiko ya Galen yalikuwa msingi wa tiba kwa karne nyingi za baadaye. Yalitafsiriwa baadaye pia kwa Kiarabu na kuathiri tiba ya Waislamu.

Tanbihi

Tags:

129216AfyaDola la RomaEnzi ya katiMagonjwaMgirikiMwanafalsafaNadhariaTabibuTibaUlayaWaislamu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Elimu ya bahariMkoa wa KigomaUandishiKinjikitile NgwaleBaraza la mawaziri TanzaniaHadhiraMapinduzi ya ZanzibarMfumo wa JuaOrodha ya Magavana wa TanganyikaMkoa wa DodomaMjasiriamaliUchawiChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)MfupaIsimujamiiInsha ya wasifuVivumishi vya urejeshiMshororoKiburiTungo kishaziNyangumiSteven KanumbaUandishi wa barua ya simuMkopo (fedha)TenziNyotaPaul MakondaEe Mungu Nguvu YetuJangwaTamathali za semiVitendawiliKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMkoa wa TaboraFonimuElimuUmaskiniKilimoTwigaSarufiVieleziUjimaUkongaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMaishaJinaTawahudiUkristoWilayaJoziVita ya uhuru wa MarekaniWilaya ya KinondoniMandhariMishipa ya damuKatibaMkoa wa TangaVisakaleKito (madini)NairobiNdiziLenziMkoa wa Unguja Mjini MagharibiKongoshoWanyamweziMashuke (kundinyota)ArudhiTambikoWazaramoKaswendeMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifa🡆 More