Pasifiki: Bahari

Pasifiki ni bahari kubwa kuliko zote duniani.

Pasifiki: Bahari
Bahari ya Pasifiki katika dunia.

Pasifiki iko kati ya Bara la Amerika upande wa mashariki na Bara la Asia / Australia upande wa magharibi.


Eneo lake ni kilometa za mraba milioni 179.7 ambayo si bahari kubwa tu bali pia ni eneo kubwa kuliko nchi kavu yote duniani: ni karibu nusu ya uso wa dunia.

Kuna visiwa zaidi ya 25,000 katika Pasifiki; vingi ni vidogo sana. Visiwa hivyo huhesabiwa mara nyingi pamoja na Australia kama "Australia na Pasifiki".

Pasifiki ina kina cha wastani wa mita 4,028; kina kirefu katika mfereji wa Mariana kinafikia mita 11,034.

Pasifiki: Bahari
Pasifiki inavyoonekana kutoka angani; Australia iko upande wa kushoto chini.

Bahari za pembeni ziko hasa upande wa Asia / Australia. Kati ya hizo ni: Bahari ya Celebes, Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China.

Jina la Pasifiki (kwa Kilatini: yenye amani, yaani kimya) limetokana na Wazungu wa kwanza waliovuka bahari hii mwaka 1520 BK kutoka Amerika ya Kusini hadi Ufilipino wakaikuta kuwa ni bahari tulivu. ù

Lakini Pasifiki inaweza kuwa na dhoruba kali sana. Ni eneo lenye matetemeko ya ardhi mengi yanayosababisha mawimbi haribifu ya tsunami ambayo yalimaliza miji na vijiji ufukoni.

Pasifiki: Bahari Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

BahariDuniani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KamusiUfaransaMbiu ya PasakaKalenda ya GregoriTrilioniMaana ya maishaDuniaJohn Raphael BoccoMvuaIniNdege (mnyama)Ligi Kuu Tanzania BaraBahari ya HindiMwakaEkaristiAbedi Amani KarumeMsibaKiumbehaiUgonjwa wa uti wa mgongoMohammed Gulam DewjiShambaIsraelUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiUingerezaWashambaaHistoria ya IsraelMofolojiaKalenda ya KiyahudiMapambano ya uhuru TanganyikaCristiano RonaldoBoris JohnsonKilimanjaro (Volkeno)Kondomu ya kikeMaambukizi ya njia za mkojoUandishiUpendoRisalaMombasaAsiaMkanda wa jeshiNgome ya YesuLongitudoOrodha ya milima ya TanzaniaKiingerezaOrodha ya miji ya MarekaniUjamaaJuxChuraSeli nyeupe za damuOrodha ya makabila ya TanzaniaTaasisi ya Taaluma za KiswahiliKupatwa kwa JuaMbeya (mji)Aina za udongoMashariki ya KatiMkoa wa ShinyangaTaswira katika fasihiAngahewaKata za Mkoa wa Dar es SalaamIdi AminJipuWikimaniaKadi za mialikoMisemoHistoria ya AfrikaDiamond PlatnumzKilatiniUfugaji wa kukuKombe la Mataifa ya AfrikaFamiliaSteven KanumbaUshogaKishazi tegemeziMekatilili Wa Menza🡆 More