Jangwa La Namib

Namib ni jangwa kubwa kwenye pwani ya kusini-magharibi ya Afrika hasa nchini Namibia na kusini mwa Angola.

Eneo lake linaanza kusini kwenye mto Olifants wa Afrika Kusini na huelekea hadi kusini ya Angola.

Jangwa La Namib
Matuta ya mchanga ya kuvutia kwenye Jangwa la Namib
Jangwa La Namib
Sossusvlei, pamoja na beseni la ziwa linalojitokeza katika miaka penye mvua nyingi

Jina la Namib limetokana na lugha ya Wanama likimaanisha "pasipo kitu".

Jangwa hili linazunguka eneo la ukubwa wa takribani kilomita mraba 80,900 (maili mraba 31,200). Umbo la Namib ni kanda yenye urefu wa km 2000 na upana wa km 100-160 kuanzia mwambao wa Atlantiki.

Jangwa hilo limesababishwa na mkondo wa Benguela unaosukuma maji baridi kutoka Antaktika kuelekea pwani ya Afrika. Mkondo huo unazuia mvua kunyesha karibu na mwambao na hivyo kuleta hali ya hewa kavu.

Baada ya kuwa na hali ya ujangwa au nusu jangwa kwa zaidi ya miaka milioni 55, linadhaniwa kuwa jangwa kongwe zaidi duniani. Hali ya ukame ya Namib inasababishwa na hewa kavu ya Hadley Cell, inaposhuka na kupoeshwa na hewa ya baridi ya Benguela kando ya pwani. Ina chini ya milimita 10 (inchi 0.4) ya mvua kila mwaka na ardhi yake iko karibu tasa.

Kuna spishi kadhaa za mimea na wanyama ambazo zinapatikana tu katika jangwa hilo. Mojawapo ni Welwitschia mirabilis, mmea unaofanana na magugu, lakini inakua na majani mawili marefu tu maisha yake yote. Majani hayo yanaweza kuwa mita kadhaa kwa urefu, yaliyokunjika na kupindika kutokana na upepo wa jangwani. Mzizi wa kati wa mmea huu hujiendeleza hadi ukawa kama sinia na umri. Welwitschia ni mashuhuri kwa uwezo wake wa kustahimili ukame mkubwa katika jangwa la Namib, wakati mwingine ukitoa unyevu kutoka ukungu wa mwambao.

Namib haina makazi ya watu isipokuwa miji michache pwani. Miji muhimu ni Swakopmund na Walvis Bay penye bandari kuu ya Namibia. Lüderitz ni mji mdogo tu uliokuwa muhimu zaidi zamani za kuchimba almasi karibu na mji huu.

Kuna pia makazi ya mwaka wote katika eneo la Sesriem, karibu na Sossusvlei iliyo maarufu kutokana na matuta ya mchanga makubwa yanayofikia kimo cha mita 300 na urefu hadi km 30, ni miongoni mwa yale marefu zaidi duniani.

Mwingiliano kati ya hewa iliyojawa na maji kuja kutokea baharini kutoka kwa upepo wa kusini, baadhi ya upepo ulio na nguvu zaidi kando ya jangwa yoyote kwenye fuo za bahari, na ukame wa hewa ya jangwa husababisha ukungu upepo mkali na kusababisha wanamaji kupoteza njia yao. Pamoja na Pwani ya Skeleton kaskazini zaidi, ina sifa mbaya kama mahali meli hubondeka. Baadhi ya hizi meli zilizobondeka zinaweza kupatikana hata mita 50 barani, huku jangwa likisonga magharibi polepole ndani ya bahari, ardhi kuboreshwa itachukua kipindi cha miaka mingi.

Jangwa la Namib ni eneo muhimu kwa ajili ya madini ya Tungsten, chumvi na almasi.

Usafiri ni wa anga kwa kutumia ndege kutoka Windhoek (mji mkuu wa Namibia, karibu kilomita 480 kaskazini-mashariki mwa kituvo cha jangwa), Swakopmund na Walvis Bay kaskazini mwa jangwa, kwa kutumia barabara. Barabara kubwa ya lami kutoka Windhoek kuelekea Swakopmund na nyingine kuelekea Lüderitz zinapita jangwani pamoja na barabara za udongo ambazo zinatunzwa vizuri sana.

Jangwa hili limeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Hifadhi ya picha

Angalia pia

Tanbihi

Marejeo

  • National Geographic, Januari 1992, pp. 54-85.
  • "Dune Patterns, Namib Desert, Namibia". NASA Earth Observatory. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-30. Iliwekwa mnamo 2006-05-05.  Unknown parameter |= ignored (help)

Viungo vya nje

Jangwa La Namib 
Wiki Commons ina media kuhusu:

24°45′07″S 15°16′35″E / 24.75194°S 15.27639°E / -24.75194; 15.27639

Tags:

Jangwa La Namib Hifadhi ya pichaJangwa La Namib Angalia piaJangwa La Namib TanbihiJangwa La Namib MarejeoJangwa La Namib Viungo vya njeJangwa La NamibAfrikaAfrika KusiniAngolaJangwaKusiniMagharibiNamibiaPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MajiMazingiraViwakilishiKanye WestWhatsAppJose ChameleoneWaziriVidonda vya tumboZuchuSinagogiUchawiIsimujamiiMaambukizi nyemeleziKiingerezaInshaUzazi wa mpangoMajeshi ya Ulinzi ya KenyaSayansiSimuMzeituniIsimuMuhimbiliKiunguliaHarmonizePichaHifadhi ya mazingiraKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMamaMbossoUchumiUsawa (hisabati)Mtakatifu PauloMafurikoViunganishiNafsiKifaruWilaya ya NyamaganaShinikizo la juu la damuMivighaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiTupac ShakurMethaliPumuSanaa za maoneshoBaruaUtalii nchini KenyaUgandaMahakama ya TanzaniaBloguJumuiya ya MadolaUbongoUshairiJamhuri ya Watu wa ChinaSaida KaroliShairiUkooPentekosteArsenal FCMtakatifu MarkoNdiziVita ya Maji MajiRaiaMajira ya mvuaYanga PrincessMillard AyoUajemiMajina ya Yesu katika Agano JipyaBaraMeliMange KimambiFani (fasihi)SumakuTanganyikaUbadilishaji msimbo🡆 More