Jangwa La Kalahari

Kalahari ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi na nusu yabisi kusini mwa Afrika lenye kilomita za mraba 900,000 hivi katika Botswana na sehemu za Namibia na Afrika Kusini.

Jangwa La Kalahari
Jangwa la Kalahari (lililoonyeshwa kwa rangi nyekundu nyeusi) na Beseni la Kalahari (rangi ya chungwa).
Jangwa La Kalahari
Kalahari huko Namibia.

Ni tofauti na jangwa la Namib lililopo nyuma ya pwani ya Atlantiki ya Namibia na Angola.

Jina

Jina "Kalahari" linatokana na neno la Kitswana "Kgala", linalomaanisha "kiu kubwa" au kutoka "Kgalagadi" inayomaanisha "pasipo maji". Kalahari ina maeneo makubwa yaliyofunikwa na mchanga tu bila maji ya kudumu.

Tabia

Kalahari huwa na wanyama na mimea kadhaa kwa sababu sehemu kubwa si jangwa kabisa. Kuna kiasi kidogo cha mvua. Majira ya joto ni makali sana. Maeneo yenye ukavu zaidi huwa na milimita 110-200 za mvua kwa mwaka. Maeneo yenye usimbishaji mkubwa zaidi huwa na milimita 500.

Makorongo makavu ya mito ya zamani yanapatikana kaskazini mwa Kalahari, yakijaa maji wakati wa mvua na yanayobaki kama mabwawa madogo kwa miezi kadhaa.

Beseni la Kalahari

Beseni la Kalahari ni pana zaidi likikusanya maji yote yanayotiririkia mle kwenye eneo la km2 milioni 2.5. Beseni hilo huenea hadi Botswana, Namibia na Afrika Kusini, pamoja na sehemu za Angola, Zambia na Zimbabwe.

Kuna mto mmoja wa kudumu pekee ambao ni mto Okavango. Okavango inaishia katika delta ya ndani inayofanya sehemu za vinamasi vyenye wanyamapori wengi.

Sehemu kubwa ya jangwa nchini Botswana imekuwa sehemu ya Hifadhi ya Kalahari ya Kati.

Tanbihi


Marejeo mengine

Kigezo:Commons and category

23°S 22°E / 23°S 22°E / -23; 22

Tags:

Jangwa La Kalahari JinaJangwa La Kalahari TabiaJangwa La Kalahari Beseni la KalahariJangwa La Kalahari TanbihiJangwa La Kalahari Marejeo mengineJangwa La KalahariAfrika KusiniBotswanaKilomita za mrabaKusini mwa AfrikaNamibiaNusu yabisiYabisi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KiumbehaiLugha za KibantuRisalaDiamond PlatnumzMagonjwa ya kukuNdoa katika UislamuRohoHali maadaKisononoWikipedia ya KirusiUgonjwa wa kuharaMsokoto wa watoto wachangaJumuiya ya Afrika MasharikiRwandaNamba tasaUmoja wa AfrikaNetiboliFacebookIsaMkanda wa jeshiUaUandishi wa ripotiKibodiKomaShelisheliMfumo wa upumuajiKoloniViwakilishi vya -a unganifuNguvuSheriaAthari za muda mrefu za pombeMichezo ya watotoMamaMjasiriamaliMsituMnyamaJipuOrodha ya Marais wa ZanzibarUtumbo mpanaSayansiUgirikiZambiaUzalendoIraqHerufi za KiarabuVipaji vya Roho MtakatifuAmaniMabantuSimon MsuvaMkopo (fedha)DhambiMohamed HusseinKiongoziBarua rasmiAfyaSiafuInjili ya LukaRedioMwislamuJulius NyerereKanga (ndege)Kiambishi tamatiHisiaChuraVivumishi vya -a unganifuLahaja za KiswahiliKidoleKaizari Leopold INgome ya YesuOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaMkoa wa IringaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaVipera vya semi🡆 More