Bbc

British Broadcasting Corporation (BBC) ni shirika la utangazaji la Uingereza. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la British Broadcasting Company Ltd kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma.

British Broadcasting Corporation
Nembo ya BBC
Nembo ya BBC
Kutoka mji London
Nchi Uingereza
Eneo la utangazaji Kote duniani
Kituo kilianzishwa mwaka {{{chanzo}}}
Mwenye kituo Shirika la umma Uingereza
Programu zinazotolewa {{{programu}}}
Tovuti www.bbc.co.uk
Bbc
BBC Broadcasting House, London

BBC ndio shirika la habari kubwa kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya redio, runinga na intaneti.

Tangu mwaka 1957 imerusha habari kwa Kiswahili pia.

Lengo na utawala

Kwa mujibu wa BBC, lengo lake ni kutoa habari, kuelimisha, na kuburudisha. Kauli mbiu yake ni "Nation Shall Speak Peace Unto Nation."

Shirika hili linaongozwa na Bodi ya Magavana wanaochaguliwa na Malkia au Mfalme wa Uingereza kwa ushauri toka kwa mawaziri wa serikali ya Uingereza. Hata hivyo, BBC inasema katika katiba yake kuwa inafanya kazi zake bila shinikizo toka kwa wanasiasa au wafanyabiashara na kuwa linawajibika kwa wasikilizaji na watazamaji wake tu.

Idhaa ya Kiswahili

Matangazo kwa lugha ya Kiswahili yalianza mwaka 1957. Tarehe 27 Juni 1957 sauti ya Kiswahili ilisikika mara ya kwanza; msemaji alikuwa Oscar Kambona aliyekuwa wakati ule mwanafunzi wa chuo kikuu huko London na baadaye waziri wa mambo ya nje wa kwanza baada ya uhuru wa Tanzania.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC imepanuka huduma zake hadi televisheni na intaneti. Tangu 2014 imehamisha ofisi na programu zake zote kuja Afrika ya Mashariki, ikirekodi Dar es Salaam na Nairobi.

Tanbihi

Viungo vya nje

Bbc 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Bbc  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu BBC kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Bbc Lengo na utawalaBbc Idhaa ya KiswahiliBbc TanbihiBbc Viungo vya njeBbc

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UkoloniViwakilishi vya idadiArusha (mji)Mimba za utotoniOrodha ya Marais wa KenyaIdi AminMadhara ya kuvuta sigaraNominoAfrikaNdoaMbagalaHadithiMimba kuharibikaFasihi simuliziDubaiPesaKiumbehaiWizara ya Mifugo na UvuviUpinde wa mvuaWingu (mtandao)Nomino za jumlaKonsonantiIfakaraKamusi za KiswahiliMnyoo-matumbo MkubwaMkuu wa wilayaNgamiaKitenziVitenzi vishirikishi vikamilifuVisakaleMusaHaki za watotoMbuniUgandaLongitudoUtawala wa Kijiji - TanzaniaSikioKishazi huruKiambishi awaliRiwayaAfrika KusiniMkoa wa ArushaBaruaIsimujamiiUtandawaziMkoa wa MaraSah'lomonMuungano wa Tanganyika na ZanzibarBunge la TanzaniaFani (fasihi)JinaLuhaga Joelson MpinaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaUkristo barani AfrikaSimba (kundinyota)KihusishiMkoa wa MorogoroUtendi wa Fumo LiyongoMarie AntoinetteTanganyika (ziwa)Mamba (mnyama)Wilaya ya KinondoniMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya JamiiMazungumzoMr. BlueUbongoWanyakyusaZiwa ViktoriaSimuMadini🡆 More