Nato

Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (kwa Kiingereza: North Atlantic Treaty Organization, kifupi: NATO; kwa Kifaransa: Organisation du traité de l'Atlantique nord, kifupi: OTAN) ni ushirikiano wa kujihami wa kambi ya magharibi.

Unaunganisha nchi 29 za Ulaya pamoja na Marekani na Kanada. Nchi wanachama zimeahidi kuteteana kama nchi moja inashambuliwa na nchi ya nje.

Nato
Bendera ya NATO
Nato
Nchi wanachama wa NATO mnamo mwaka 2024 kwa rangi ya buluu.
Nato
Uenezi wa NATO hadi mwaka 2020.

Makao makuu yapo Brussels.

Historia

NATO ilianzishwa mwaka 1949 wakati wa vita baridi kama maungano ya nchi za Ulaya ya magharibi pamoja na Marekani dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na nchi shiriki zake katika Mapatano ya Warshawa. Nchi wanachama wa kwanza walikuwa Marekani, Ubelgiji, Uholanzi, Luxemburg, Ufaransa, Uingereza, Kanada, Ureno, Italia, Norwei, Udeni na Isilandi. 1952 Ugiriki na Uturuki zilijiunga pia zikafuatwa na Ujerumani ya Magharibi.

Baada ya mwisho wa vita baridi nchi zilizokuwa chini ya Umoja wa Kisoveti kama sehemu ya kambi ya kikomunisti zilijiunga na NATO kuanzia mwaka 1999. Ndizo Hungaria, Ucheki, Polandi (1999), halafu Estonia, Latvia, Lituanya, Slovenia, Slovakia, Bulgaria, Romania (2004), Kroatia, Albania (2009), Montenegro (2017), Masedonia Kaskazini (2020), Ufini (2023), na Uswidi (2024).

Viungo vya Nje

Nato 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

KanadaKifaransaKifupiKiingerezaMagharibiMarekaniUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Wimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiOksijeniMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaBarack ObamaWilaya ya Unguja Magharibi AMfumo wa upumuajiMitume na Manabii katika UislamuKanisaKassim MajaliwaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaKishazi huruJulius NyerereMajira ya mvuaMkoa wa NjombeViwakilishi vya sifaKinyongaLafudhiIyungaUtoaji mimbaWakingaSeli za damuNathariMohammed Gulam DewjiMakabila ya IsraeliKiunzi cha mifupaPichaKanisa KatolikiKen WaliboraLigi Kuu Uingereza (EPL)Haki za binadamuMapinduzi ya ZanzibarMafurikoUenezi wa KiswahiliUfugajiMagonjwa ya machoMbooShinikizo la juu la damuSitiariGongolambotoAfrika ya Mashariki ya KijerumaniOrodha ya nchi za AfrikaBata MzingaKanga (ndege)Malengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaMadhara ya kuvuta sigaraMkoa wa SingidaVivumishi vya idadiOrodha ya Watakatifu WakristoHali ya hewaKimara (Ubungo)Chemsha BongoIlluminatiZama za MaweHistoria ya KanisaWilaya ya KigamboniMtaalaSamakiMsituMkoa wa MbeyaTawahudiBenjamin MkapaWaziri Mkuu wa TanzaniaSemantikiVivumishi vya kumilikiJohn Samwel MalecelaKamusiMfumo wa mzunguko wa damuNamba tasaKataMvua ya maweMweziEverest (mlima)Waha🡆 More