Prussia

Prussia ni jina muhimu katika historia ya Ujerumani pia ya Poland na Ulaya wote.

Katika karne ya 19 hadi 1933 sehemu kubwa ya Ujerumani ilikuwa chini ya dola la Prussia lililokuwa awali nchi ya pekee na baadaye jimbo kubwa la Ujerumani.

Prussia
Frederick I wa Prussia

Nchi ya Waprussia

Kisasili lamaanisha nchi ya Waprussia waliokuwa kabila ya Kibalti kaskazini-mashariki ya Poland kwenye pwani za bahari ya Baltiki. Mnamo mwaka 1200 BK Waprussia walikuwa katika hali ya vita na Poland. Mwaka 1226 mtawala wa Poland aliomba usaidizi wa jeshi wa wamisalaba Wajerumani akiwaahidi mali katika maeneo watakaoteka baada ya kushinda Waprussia.

Dola la Wamisalaba Wajerumani

Wamisalaba walifaulu kutekea eneo lilioitwa baadaya "Prussia ya mashariki" na kujenga himaya yao. Wamisalaba hawakuwa watemi wa kawaida bali wamonaki na wanajeshi. Dola la wamisalaba lilikuwa wakati mwingine chini ya mfalme wa Polandf, wakati mwingine dola la kujitegemea. Waliita walowezi na wakulima kutoka pande zote za Ujerumani na kuanzisha miji mingi.

Prussia 
Brandenburg na Prussia kati ya 1600 na 1800
buluu nyeusi: Brandenburg asilia; Kijani nyeusi: nyongeza 1618 ya Prussia; kijani: nyongeza nyingine 1600 hadi 1772; njano: nyongeza kutokana na ugawaji wa Poland

Kuunganishwa na Brandenburg

Baada ya farakano kati ya Wakatoliki na Waprotestant himaya ya wamisalaba ilipokea uprotestanti na wamisalaba waliondoka katika maisha ya umonaki. Mkuu alikuwa mtemi mtawala akaoa.

Mkuu wa mwisho wa wamisalaba alikuwa mwana wa familia ya watemi wa Brandenburg katika Ujerumani hivyo Prussia imekuwa sehemu ya urithi wa familia hii iliyoendelea kutawala Prussia pamoja na maeneo yake ndani ya Ujerumani.

Ufalme wa Prussia

1701 mtemi Friedrich wa Brandenburg alijiwekea taji ya Mfalme wa Prussia.

Prussia 
Friedrich II wa Prussia

Ufalme wa Prussia uliendelea kuwa muhimu kati ya madola ya Ujerumani. Watemi wa Brandenburg walirithi au kupata maeneo kwa njia ya vita hata katika magharibi ya Ujerumani. Mfalme Friedrich II wa Prussia alishindana na mataifa makubwa ya Ulaya katika vita ya miaka saba (1756-1763). Alikamata maeneo makubwa katika ugawaji wa Poland.

Prussia ilitokea kama dola la pili katika Dola Takatifu la Kiroma baada ya Austria.

Baada ya vita za Napoleoni mwanzo wa karne ya 19 umuhimu wa Prussia uliendelea kukua.

Mwaka 1815 ilijiunga na Shirikisho la Ujerumani lililounganisha maeneo mengi ya Dola Takatifu la awali; katika maungano hayo Prussia ilikuwa nchi kubwa ya pili baada ya Austria ilipaswa kumkubali Kaisari wa Austria kwenye nafasi ya mwenyekiti wa shirikisho.

Prussia kama kiongozi wa Ujerumani

Katika ya Vita ya Kijerumani ya 1866 Prussia ilishinda Austria na kuwa dola kiongozi kati ya madola ya Ujerumani. Mwanasiasa mkuu wa nyakati zile alikuwa Otto von Bismarck kama waziri mkuu wa Prussia na baadaye kama chansella wa Ujerumani. Baada ya kushinda Ufaransa katika vita ya 1870/1871 sehemu zote za Ujerumani isipokuwa Austria ziliunganika chini ya uongozi wa Prussia na kuanzisha Dola la Ujerumani. Mfalme Wilhelm IV wa Prussia alichaguliwa kuwa Kaisari wa Ujerumani. Alifuatwa na mtoto wake Friedrich III aliyekufa mapema halafu na Wilhelm II. Wakuu wale walitawala kwa cheo cha "Kaisari ya Ujerumani na mfalme wa Prussia".

Prussia 
Prussia (buluu nyeupe) ndani ya Ujerumani baada ya 1918

Jamhuri ya Prussia ndani ya Ujerumani

Mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ufalme wa Prussia kama vile katika sehemu zote za Ujerumani ilifutwa katika mapinduzi ya Ujerumani ya 1918. Wilhelm II akajiuzulu na kukimbilia Uholanzi. Prussia ilikuwa jimbo jamhuri ndani ya jamhuri la shirikisho la Dola ya Ujerumani.

Baada ya Adolf Hitler kuchukua utawala wa Ujerumani na kujenga udikteta madaraka ya majimbo yote pia ya Prussia yalifutwa.

Mwisho wa Prussia

Mwaka 1945 mataifa washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia waliamua kutangaza mwisho wa Prussia wakiishtaki kuwa sababu ya tabia ya kivita ya Ujerumani. Maeneo ya Prussia yalifanywa kuwa majimbo katika Ujerumani kwa jumla. Prussia asilia yenyewe iligawiwa kati ya Poland na Urusi, wakazi wake Wajerumani walifukuzwa.

Tags:

Prussia Nchi ya WaprussiaPrussia Dola la Wamisalaba WajerumaniPrussia Kuunganishwa na BrandenburgPrussia Ufalme wa Prussia kama kiongozi wa UjerumaniPrussia Jamhuri ya ndani ya UjerumaniPrussia Mwisho wa Prussia1933Karne ya 19PolandUjerumani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

BawasiriMkoa wa MaraUjerumaniMkoa wa DodomaMmeaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMkoa wa MorogoroMbogaFonolojiaZabibuBinadamuMeno ya plastikiMitume wa YesuMwanamkeMtakatifu PauloUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaUkutaPemba (kisiwa)Ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaVielezi vya idadiUNICEFUpepoMshororoHekaya za AbunuwasiRisalaShikamooJoseph ButikuAlama ya uakifishajiHali ya hewaVieleziMaji kujaa na kupwaJokate MwegeloMapinduzi ya ZanzibarMadawa ya kulevyaMajeshi ya Ulinzi ya KenyaVihisishiWingu (mtandao)Wilaya ya NyamaganaNgonjeraMuhammadKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniIsimujamiiKiboko (mnyama)UchumiHadithi za Mtume MuhammadOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaUfugajiMfumo wa mzunguko wa damuMaana ya maishaMnara wa BabeliOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMnururishoAlizetiBahari ya HindiNembo ya TanzaniaPumuVivumishi vya sifaStadi za lughaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaWaheheMfumo wa upumuajiHerufiNominoNusuirabuMeliLakabuSadakaKigoma-UjijiFutiMkoa wa LindiMaambukizi ya njia za mkojoSteven KanumbaKiongoziBabeliMuungano wa Tanganyika na Zanzibar🡆 More