Nchi Ya Moto

Nchi ya Moto (ndiyo tafsiri ya jina Tierra del Fuego) ambayo ni funguvisiwa kwenye kusini kabisa ya Amerika Kusini.

Imetengwa na bara kwa Mlangobahari wa Magellan. Rasi ya Hoorn ambayo ni ncha ya kusini kabisa ya Amerika, iko hapa.

Nchi Ya Moto
Tierra de Fuego - Nchi ya Moto.
Nchi Ya Moto
Bandari ndogo ya Porto Williams upande wa Chile.

Visiwa vyote vina eneo la kilomita za mraba 73,746 na kisiwa kikuu Isla Grande de Tierra del Fuego kina km2 47.000.

Tangu mwaka 1881 funguvisiwa limegawiwa kwenye longitudo ya magharibi ya 69° 31' kwa nchi mbili za Chile na Argentina. Upande wa mashariki, katika mkoa wa "Tierra del Fuego", kuna wakazi wapatao 127.000, upande wa magharibi, katika mkoa wa Magellanes wa Chile, kuna watu 8,000.

Jina linatokana na kumbukumbu ya wapelelezi Wahispania waliovuka Amerika Kusini kwenye mwaka 1520. Walipopita hapa hawakuona watu wowote lakini wakati wa usiku waliona mioto mingi, hivyo Magellan aliandika "Nchi ya moto" katika ramani yake.

Hata baada ya kuanzishwa kwa ukoloni wa Hispania katika sehemu za kaskazini ya Amerika Kusini, wenyeji Waindio, waliokuwa wavuvi na wawindaji, waliendelea kuishi tu bila usumbufu kwa muda mrefu hadi karne ya 19.

Kuanzia mwaka 1860 wafugaji wa kondoo kutoka Argentina na wachimbaji madini kutoka Chile walianza kuingia kwenye Tierra del Fuego. Pamoja na kunyang'anywa ardhi yao wazalendo wengi walikufa baada ya kuambukizwa magonjwa kutoka Ulaya ambayo hawakuzoea, sawa jinsi ilivyowahi kutokea kwa Waindio wengi tangu kuingia kwa Wazungu. Leo ni wachache sana waliobaki.

Eneo ni baridi mno kwa kilimo lakini hadi leo ufugaji wa kondoo na biashara ya sufi ni msingi wa uchumi. Kampuni ya nguo Bennetton inamiliki maeneo ya kilomita za mraba milioni moja kwa ufugaji wa kondoo.

Tanbihi

Marejeo mengine

  • Bridges, Lucas. 1948. Uttermost Part of the Earth. Reprint with introduction by Gavin Young, Century Hutchinson, 1987. ISBN|-7126-1493-1
  • Keynes, Richard. 2002. Fossils, Finches and Fuegians: Charles Darwin's Adventures and Discoveries on the Beagle, 1832–1836. HarperCollins Publishers, London. Reprint: 2003.
  • Bollen, Patrick. 2000. "Tierra del Fuego" B/W Photobook. Lannoo Publishers, Tielt, Belgium. ISBN 90-209-4040-6
  •  

Tovuti za Nje

Nchi Ya Moto  Tierra del Fuego travel guide kutoka Wikisafiri

Nchi Ya Moto 
Wiki Commons ina media kuhusu:

54°S 70°W / 54°S 70°W / -54; -70

Tags:

AmerikaAmerika KusiniBaraFunguvisiwaJinaKusiniMlangobahari wa MagellanTafsiri

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Lil WayneZuchuNyaniMkoa wa KageraFasihiMkoa wa KilimanjaroRobin WilliamsKunguruNembo ya TanzaniaKilwa KivinjeKiarabuRihannaNgeli za nominoAdhuhuriMkoa wa MwanzaMacky SallUsultani wa ZanzibarInstagramKigoma-UjijiKuhani mkuuDioksidi kaboniaUtamaduniKalenda ya KiyahudiMbeguMaishaMofolojiaNamba za simu TanzaniaKondoo (kundinyota)Uundaji wa manenoBrazilUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius NyerereUwanja wa Taifa (Tanzania)MtaalaJuma kuuVidonda vya tumboKisononoLahajaMizimuViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)MarekaniNzigeNetiboliHomanyongo CTenziMashariki ya KatiCristiano RonaldoChatuPonografiaAunt EzekielHistoria ya EthiopiaKalendaTanzaniaMahakamaMkoa wa KataviAfrika ya MasharikiHadithi za Mtume MuhammadKitenzi kikuu kisaidiziSenegalMafarisayoJuaKondomu ya kikeKunguniAganoVipaji vya Roho MtakatifuMwaka wa KanisaUbatizoUislamuKitenziMazungumzoChakulaAir Tanzania🡆 More