Waindio au Wahindi wekundu ni watu wanaotokana moja kwa moja na waliokuwa wenyeji wa Amerika kabla ya bara hilo kufikiwa na Christopher Columbus kutoka Ulaya (1492).
Utafiti uliofanywa kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali umekadiria kwamba mababu wao walioenea katika Amerika yote wakitokea Asia kaskazini mashariki miaka 14,500 BK.
Inadhaniwa kwamba hao mababu waliishi muda mrefu na kuzaliana bila mawasiliano na binadamu wengine, labda katika eneo ambalo leo limefunikwa na maji kwenye mlangobahari wa Bering. Inakadiriwa DNA yao ilitokana na ile ya Waasia mashariki (2/3) na Waeurasia (1/3).
Baada ya kuingia bara hilo, ambalo ni la mwisho kukaliwa na watu (tukiacha Antaktiki), kwa karne chache walienea hadi kusini kabisa, kwenye Chile na Argentina ya leo. Katika kusambaa kwao, lugha na utamaduni vilizidi kutofautiana.
Idadi yao inaweza kuwa milioni 60, wengi wao wakiishi Meksiko, Peru, Bolivia na Guatemala.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waindio kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Waindio, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.