Hildegarda Wa Bingen

Hildegarda wa Bingen, O.S.B., kwa Kijerumani Hildegard von Bingen, kwa Kilatini Hildegardis Bingensis (Bermersheim vor der Höhe, Rhineland, Dola Takatifu la Kiroma, 1098 hivi - Bingen am Rhein, 17 Septemba 1179).

alikuwa mwanamke mmonaki, mwanafalsafa na mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali kutoka Ujerumani wa leo.

Hildegarda Wa Bingen
Hildegarda Wa Bingen
Hildegarda akipata njozi na kumsimulia karani wake.

Toka zamani abesi huyo anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, halafu na Waanglikana na Walutheri kama mtakatifu.

Papa Benedikto XVI alithibitisha utakatifu wake tarehe 10 Mei 2012 na kumtangaza mwalimu wa Kanisa tarehe 7 Oktoba 2012.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Septemba.

Maisha

Hildegarda alizaliwa Bermersheim vor der Höhe, Rhineland, 1098 hivi, na Hildebert na Mekthilde katika familia tajiri ya kisharifu kama mtoto wa kumi, mgonjwa tangu mwanzo.

Katika kitabu chake Maisha, Hildegarda anasimulia kwamba alianza kupata njozi akiwa na miaka 3 tu, na kwamba alipofikia miaka 5 alianza kutambua ni karama kutoka kwa Mungu.

Labda kwa sababu hiyo wazazi wake walimtoa kwa Mungu akiwa na umri wa miaka 8, amtumikie utawani kulingana na Kanuni ya Mt. Benedikto, wakamweka kwa malezi ya kiutu na ya Kikristo kwanza chini ya Uda wa Gölklheim, mjane aliyewekwa wakfu, halafu chini ya Jutta wa Sponheim, aliyekwisha kuvikwa shela katika monasteri changa ya wanawake Wabenedikto.

Hakuna kumbukumbu za miaka 24 aliyoishi na Jutta.

Kwa vyovyote, walikuwa wamejifungia huko Disibodenberg, katika msitu wa Palatinate. Jutta pia alikuwa na njozi, jambo lililovutia wengi kumtembelea.

Jutta alimfundisha kusoma na kuandika, lakini hakuweza kumsaidia katika ufafanuzi wa Biblia.

Inawezekana kuwa wakati huo ndio alipojifunza muziki na kuanza utunzi wake.Hildegarda alivikwa kimonaki na askofu Oto wa Bamberg akaweka nadhiri mwaka 1115.

Baada ya Jutta kufariki mwaka 1136, Hildegarda alichaguliwa na wamonaki wenzake kwa kauli moja kushika nafasi yake kama "magistra" (yaani mwalimu na kiongozi) wa jumuia yao ya kike.

Hapo alitimiza kazi yake kwa kutumia vipawa vyake kama mwanamke mwenye elimu na maisha ya Kiroho ya hali ya juu, akikabili vema majukumu ya uongozi. Alilenga hali bora jumuiani kwa busara na kiasi inavyodaiwa na Kanuni ya Mt. Benedikto.

Baada ya miaka michache, kutokana pia na wingi wa miito iliyojitokeza kujiunga naye, alimuomba Abati Kuno wa Disibodenberg aweze kuhamia hali ya kifukara zaidi huko Rupertsberg.

Alipokataliwa, alimkimbilia Askofu mkuu Henry I wa Mainz: hatimaye akakubaliwa na abati akahamia na wenzake 20 hivi katika monasteri ya Rupertsberg mwaka 1150, ambapo paroko mmonaki Volmar akawa muungamishi na pia karani wake pamoja na sista Richardis wa Strade.

Mwaka 1165 Hildegarda alianzisha monasteri nyingine huko Eibingen, upande wa pili wa mto Rhine, akawa abesi wa zote mbili na kustawisha hasa maisha ya pamoja, elimu na liturujia. Alichochea watawa washindane katika kupeana heshima, kutumikiana na kutenda mema.

Njozi

Ingawa Hildegarda alisema haiwezekani kuyasimulia aliyojaliwa kujua kwa mwanga wa Mungu kupitia hisi zake na alisita kuyashirikisha mwaka 1141, akiwa na miaka 42, alisadiki Mungu amemuagiza ayaandike yote.

Hata hivyo aliendelea kusitaakitamani uthibitisho wa watu wenye hekima kwa kuogopa amedanganyika.

Alipoomba shauri la Mt. Bernardo wa Clairvaux, alimuandikia: “Njozi inateka nafsi yangu yote: siioni kwa macho ya mwili bali inanitokea katika roho ya mafumbo… Natambua maana ya dhati ya maneno ya Zaburi, ya Injili na ya vitabu vingine, kama nilivyoonyeshwa katika njozi. Hiyo inawasha kama mwali wa moto katika kifua changu na katika roho yangu na inanifundisha kuelewa matini kwa dhati”. Alijibiwa kwamba asijali sana njozi, ila aendelee kutenda mema kwa bidii.

Kitabu cha Maisha yake kilianza kuandikwa na Godfrey wa Disibodenberg chini ya usimamizi wa Hildegarda.

Kati ya Novemba 1147 na Februari 1148, wakati wa Sinodi ya Trier, Papa Eugenio III alipata habari za maandishi hayo akayathibitisha kuwa mafunuo ya Roho Mtakatifu, akimruhusu kuandika njozi zake na hata kuhubiri hadharani, tofauti na kawaida ya wanawake wa wakati ule.

Tangu hapo alizidi kuheshimiwa akaitwa “nabii wa kike wa Kijerumani”. Kwa mamlaka ya kiroho aliyopewa tena na Papa Adrian IV na Papa Aleksanda III, miaka yake ya mwisho alisafiri sana ili kusema na taifa la Mungu, bila kujali uzee wake na ugumu wa safari.

Katika nyanja za miji na katika makanisa makuu, kama vile ya Koln, Trier, Liège, Mainz, Metz, Bamberg na Würzburg, wote walimsikiliza kwa makini, hata alipozungumza kwa ukali, kwa kuwa waliamini ni mjumbe wa Mungu.

Watu wengi wa kila aina, wakiwemo maaskofu, maabati na watawala, walimuomba shauri. Ndiyo sababu tuna barua zake nyingi, karibu 400. Humo tunashuhudia alivyozingatia matukio ya wakati ule, akiyafafanua kwa mwanga wa fumbo la Mungu.

Kaisari Fredrick I aliposababisha farakano ndani ya Kanisa kwa kukubali Maantipapa walau watatu dhidi ya Papa Aleksanda III, Hildegarda hakusita kumuandikia alichosikia katika njozi: “Utajutia mwenendo huo mwovu kama wa mtu asiye na Mungu na anayenidharau! Sikiliza, ee Mfalme, ukitaka kuishi! La sivyo upanga wangu utakuchoma”.

Zimetunzwa hotuba 58 alizozitoa kwa masista wenzake kama ufafanuzi wa Injili ambazo zilitumika katika sikukuu za mwaka wa liturujia.

Nje ya monasteri alijitahidi kuimarisha imani na maisha ya Kikristo. Alihimiza hasa wamonaki na wakleri kuishi inavyodaiwa na wito wao, lakini alipinga sana Wakatari waliotaka urekebisho mkali wa Kanisa. Aliwalaumu kwa kujaribu kupindua umbile halisi la Kanisa akawakumbusha kwamba urekebisho halisi unategemea roho nyofu ya toba na mchakato mgumu wa wongofu kuliko mabadiliko ya miundo tu.

Maandishi yake yalitokana hasa na mang’amuzi yake ya juu katika sala, hivyo yanajitokeza kwa udhati, usahihi na upekee wa mitazamo. Kwa kutumia mawazo na maneno ya mazingira yake, na zaidi lugha ya kishairi na ya kifumbo, alifafanua Maandiko matakatifu kwa mwanga wa Mungu na kuhusiana na maisha yalivyo. Ndiyo sababu wale wote waliomsikiliza walijisikia haja ya kuishi Kikristo kweli.

Njozi zake zina maana kubwa upande wa teolojia, zikihusu matukio makuu ya historia ya wokovu na kufanana na zile za manabii wa Agano la Kale. Kwa mfano, kitabu chake maarufu zaidi, “Scivias” (yaani “Zijue Njia”), njozi 35 zinajumlisha habari za kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwisho wa nyakati.

Kwa hisia yake ya kike Hildegarda katika kiini cha kitabu chake anafafanua ndoa ya fumbo kati ya Mungu na binadamu iliyofanyika katika [[umwilisho[[. Juu ya msalaba iliadhimishwa arusi ya Mwana wa Mungu na Kanisa lililojazwa neema ili liweze kuzaa watoto wa Mungu wengine katika upendo wa Roho Mtakatifu.

Vitabu vingine viwili vinaripoti pia njozi zake: “Kitabu cha Stahili za Maisha” na “Kitabu cha Kazi za Mungu”, ambacho wengi wanakiona kuwa bora kuliko vyote.

Akiwa msanii, alitunga tenzi, antifona na nyimbo ambazo zilikusanywa kwa jina la “Muziki wa Ulinganifu wa Mafunuo ya Kimbingu” na kutumika kwa furaha monasterini, zikieneza hali ya utulivu.

Maandishi yake mengine, yakizungumzia hata utabibu, sayansi na isimu, yanaonyesha wingi wa elimu uliokuwemo katika monasteri ya kike ya Karne za Kati, nayo yaliathiri watu wengi, yakichangia upyaisho wa teolojia, liturujia, sayansi na muziki.

Hakuna mwanamke wa Karne za Kati anayeweza kushindana naye kwa wingi na ubora wa maandishi wala kwa upana wa mada alizozijadili.

Tena ndani mwake mafundisho na maisha yalilingana kabisa. Akilenga kutimiza matakwa ya Mungu nyuma ya Kristo, alitekeleza maadili yote mfululizo na kwa bidii, akitegemezwa na vitabu vya Biblia, liturujia na Mababu wa Kanisa awe mali ya Bwana tu kadiri ya Kanuni ya Mt. Benedikto.

Masista wenzake waliomzunguka alipofariki Bingen am Rhein tarehe 17 Septemba 1179, walisema kuwa waliona miali miwili ya mwanga kutoka angani na kupitia chumba chake.

Mwanamke huyo anazidi kusema leo kwa upendo wake kwa Kristo na kwa Kanisa (ambalo hata wakati wake alijeruhiwa na dhambi za watoto wake), kwa ujasiri wake katika kutambua ishara za nyakati, kwa jinsi alivyopenda viumbe, kwa utabibu wake na kwa sanaa zake.

Filamu juu yake

  • Patricia Routledge, "Hildegard Von Bingen In Portrait: Ordo Virtutum."
  • Margarethe von Trotta, "Vision - From the Life of Hildegard von Bingen"

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Primary sources
    Editions and manuscripts of Hildegard's works
  • Hildegardis Bingensis, Opera minora. edited by H. Feiss, C. Evans, B. M. Kienzle, C. Muessig, B. Newman, P. Dronke, Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis CCCM 226 (Turnhout: Brepols, 2007), ISBN 978-2-503-05261-8
  • Wiesbaden, Hessische Landesbibliothek, Hs. 2 (Riesen Codex) or Wiesbaden Codex (ca. 1180–85)
  • Dendermonde, Belgium, St.-Pieters-&-Paulusabdij Cod. 9 (Villarenser codex) (ca. 1174/75)
  • Otto Müller Verlag Salzburg 1969: Hildegard von Bingen: Lieder (modern edition in adapted square notation)
  • München, University Library, MS2∞156
  • Leipzig, University Library, St. Thomas 371
  • Paris, Bibl. Nat. MS 1139
  • Beate Hildegardis Cause et cure, edidit L. Moulinier, Berlin, Akademie Verlag, 2003, CXVII + 384 p.
  • Hildegardis Bingensis, Epistolarium pars prima I-XC edited by L. Van Acker, Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis CCCM 91A (Turnhout: Brepols, 1991)
  • Hildegardis Bingensis, Epistolarium pars secunda XCI-CCLr edited by L. Van Acker, Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis CCCM 91A (Turnhout: Brepols, 1993)
  • Hildegardis Bingensis, Epistolarium pars tertia CCLI-CCCXC edited by L. Van Acker and M. Klaes-Hachmoller, Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis XCIB (Turnhout: Brepols, 2001)
  • Hildegardis Bingensis, Scivias. A. Führkötter, A. Carlevaris eds., Corpus Christianorum Scholars Version vols. 43, 43A. (Turnhout: Brepols, 2003)
  • Hildegardis Bingensis, Liber vitae meritorum. A. Carlevaris ed. Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis CCCM 90 (Turnhout: Brepols, 1995)
  • Hildegardis Bingensis, Liber divinorum operum. A. Derolez and P. Dronke eds., Corpus Christianorum Continuatio Mediaevalis CCCM 92 (Turnhout: Brepols, 1996)
  • Hildegard of Bingen, Two Hagiographies: Vita sancti Rupperti confessoris, Vita sancti Dysibodi episcopi, ed. and trans. Hugh Feiss & Christopher P. Evans, Dallas Medieval Texts and Translations 11 (Louvain and Paris: Peeters, 2010)
    Other sources
  • Friedrich Wilhelm Emil Roth, "Glossae Hildigardis", in: Elias Steinmeyer and Eduard Sievers eds., Die Althochdeutschen Glossen, vol. III. Zürich: Wiedmann, 1895, 1965, pp. 390–404.
  • Analecta Sanctae Hildegardis, in Analecta Sacra vol. 8 edited by Jean-Baptiste Pitra (Monte Cassino, 1882).
  • Patrologia Latina vol. 197 (1855).
  • Explanatio Regulae S. Benedicti
  • Explanatio Symboli S. Athanasii
  • Homeliae LVIII in Evangelia.
  • Hymnodia coelestis.
  • Ignota lingua, cum versione Latina
  • Liber divinorum operum simplicis hominis (1163-73/74)
  • Liber vitae meritorum (1158–63)
  • Libri simplicis et compositae medicinae.
  • Physica, sive Subtilitatum diversarum naturarum creaturarum libri novem
  • Scivias seu Visiones (1141–51)
  • Solutiones triginta octo quaestionum
  • Tractatus de sacramento altaris.

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Hildegarda Wa Bingen 
WikiMedia Commons


Tags:

Hildegarda Wa Bingen MaishaHildegarda Wa Bingen NjoziHildegarda Wa Bingen Filamu juu yakeHildegarda Wa Bingen Tazama piaHildegarda Wa Bingen TanbihiHildegarda Wa Bingen VyanzoHildegarda Wa Bingen MarejeoHildegarda Wa Bingen Marejeo mengineHildegarda Wa Bingen Viungo vya njeHildegarda Wa Bingen1098117917 SeptembaBingen am RheinDola Takatifu la KiromaKijerumaniKilatiniMmonakiMwanafalsafaMwanamkeO.S.B.Ujerumani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MashineAlasiriVitamini CBaraza la Maaskofu Katoliki TanzaniaMariooNamba za simu TanzaniaKitenzi kishirikishiJumuiya ya Afrika MasharikiNguruweAlfabetiMagharibiUzalendo28 MachiHaki za binadamuMatamshiNomino za kawaidaNahauShahawaLugha ya piliYesuSayari ya TisaTanganyika (ziwa)WaheheHomoniChe GuevaraUgonjwa wa uti wa mgongoTungo kishaziBarua pepeKishazi tegemeziUkraineMsumbijiVirutubishiEmmanuel OkwiBurundiViunganishiNyweleMikoa ya TanzaniaMadhara ya kuvuta sigaraFeisal SalumKanga (ndege)WamasaiMagavanaGesi asiliaBara ArabuChadNandyMbuga wa safariTupac ShakurCédric BakambuHoma ya mafuaUkoloni MamboleoSeli za damuFigoNdege (mnyama)Everest (mlima)IsraelMaajabu ya duniaMkoa wa MorogoroHaki za wanyamaMlongeKamusi ya Kiswahili - KiingerezaMaumivu ya kiunoUkristoPopoTreniHarakati za haki za wanyamaJiniKipajiVidonge vya majiraZakaKiarabuIntanetiBenjamin MkapaWayahudiFananiChunusiWiki🡆 More