Mwana Wa Mungu

Mwana wa Mungu ni jina linalotumiwa katika dini mbalimbali ili kusisitiza uhusiano wa mtu fulani na Mungu au mmojawapo wa miungu.

Kwa maana hiyo lilitumika hasa kwa ajili ya watawala.

Mwana Wa Mungu
Mungu Baba na Roho Mtakatifu pamoja na mtoto Yesu kadiri ya Murillo, 1670 hivi.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Pengine linamaanisha viumbe vingine, kama vile malaika.

Katika Biblia

Katika Biblia ya Kikristo jina hilo linamhusu kwa namna ya pekee sana Yesu, na katika madhehebu karibu yote ya Ukristo linafafanuliwa kumaanisha asili yake ya milele katika Mungu pekee kabla ya kujifanya binadamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya Bikira Maria.

Mwana Wa Mungu 
Ukurasa wa kwanza wa Injili ya Marko: "Mwanzo wa habari njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu", karne ya 14.

Kadiri ya Injili, Yesu Kristo mwenyewe alisisitiza mara nyingi uhusiano wake wa pekee na Baba wa mbinguni kutokana na asili yake toka juu, tofauti na ile ya watu wengine wote.

Mwana Wa Mungu 
Kupaa Bwana kadiri ya Pietro Perugino (1500 hivi), Lyon, Ufaransa.

Kila mmoja kwa namna yake, Mtume Paulo, Wainjili na waandishi wengine wa Agano Jipya walitumia sana jina hilo, hata kuliweka pembeni kidogo jina lingine lililotumiwa sana na Yesu mwenyewe, yaani Mwana wa Adamu.

Katika historia ya Kanisa

Jina hilo lilizidi kutafsiriwa kwa namna tofauti kadiri teolojia ilivyostawi, hasa baada ya kaisari Konstantino Mkuu kuruhusu Ukristo katika Dola la Roma (313).

Kutokana na fujo zilizojitoleza hata kuhatarisha amani ya dola, mwenyewe, akishirikiana na Papa Silvesta I, aliitisha mtaguso mkuu wa kwanza uliofanyika mwaka 325 huko Nisea.

Mtaguso huo ulitunga kanuni ya imani iliyokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa maana ana hali moja na Mungu Baba, hakuumbwa bali alizaliwa naye tangu milele yote.

Mwana Wa Mungu 
Konstantino Mkuu na mababu wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea.

Wakristo wanapomkiri Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu… Amwaminiye yeye hahukumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yoh 1:1,14; 3:18).

Msimamo wa Uislamu

Uislamu unamheshimu Yesu kama nabii mmojawapo, lakini unakanusha kabisa jina hilo na maana yake yoyote ili kusisitiza upekee wa Mungu.

Tanbihi

Marejeo

Mwana Wa Mungu  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwana wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Mwana Wa Mungu Katika BibliaMwana Wa Mungu Katika historia ya KanisaMwana Wa Mungu Msimamo wa UislamuMwana Wa Mungu TanbihiMwana Wa Mungu MarejeoMwana Wa MunguDiniJinaMiunguMtuMunguWatawala

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UbunifuRoho MtakatifuEmmanuel OkwiTabianchiNidhamuVidonda vya tumboHewaItifakiUjerumaniNomino za jumlaMwanamkeBaruaUenezi wa KiswahiliMilki ya OsmaniZana za kilimoMilaInsha ya wasifuVielezi vya mahaliOrodha ya milima mirefu dunianiNyanja za lughaMsengeMjombaJeshiLatitudoOrodha ya Marais wa UgandaVihisishiDhambiRayvannyUgonjwa wa uti wa mgongoChakulaKen WaliboraJuaChris Brown (mwimbaji)MbeguMariooWakingaUti wa mgongoMfumo katika sokaNguzo tano za UislamuMotoPasaka ya KikristoJakaya KikweteKiraiZambiaEngarukaMamaSiafuVieleziHistoria ya KiswahiliSintaksiAbedi Amani KarumeMbooMatamshiAmfibiaKiumbehaiKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaVirutubishiAngkor WatUyahudiKumamoto, KumamotoKatibuBarua rasmiMwanaumeAfrikaKitomeoMafumbo (semi)UkooAzimio la kaziHoma ya iniKitenziOrodha ya vitabu vya BibliaJamhuri ya KongoMbeya (mji)Misimu (lugha)Ufufuko wa Yesu🡆 More