Maneno Saba

Maneno saba katika Ukristo ni yale ambayo Yesu aliyatamka akiwa msalabani na yamerekodiwa katika Injili nne.

Maneno Saba
Alichokuwa anaona Yesu msalabani, mchoro wa James Tissot, 1890 hivi.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Kati yake, matatu yanapatikana katika Injili ya Luka tu, mawili katika Injili ya Yohane tu. Lingine linapatikana katika Injili ya Mathayo na Injili ya Marko vilevile. Lingine tena limerekodiwa na Yohane lakini Mathayo na Marko wamelidokeza.

Katika Mathayo na Marko, Yesu Kristo anamlilia Mungu. Katika Luka, yeye anawasamehe wauaji wake, anamfariki mhalifu aliyetubu, na kumkabidhi Baba roho yake. Katika Yohane, Yesu anasema na mama yake na mwanafunzi mpendwa, anatokeza kiu yake, na kutangaza utimilifu wa kazi na maisha yake yote kadiri ya mpango wa Mungu.

Maneno ya buriani ya mtu yeyote yanatiwa maanani sana. Yanaweza kusaidia kuelewa nini ilikuwa muhimu kwake. Ilikuwa hivyo hasa kwa Yesu aliyeweza kusema machache tu kutokana na hali yake.

Tangu karne ya 16 maneno hayo yametumika sana katika mahubiri ya madhehebu mbalimbali siku ya Ijumaa kuu, na vitabu vingi vimetungwa kuyafafanua.

Watunzi mbalimbali waliyatia katika muziki.

Mpangilio wa kawaida ni huu:

  1. Lk 23:34
  2. Lk 23:43
  3. Yoh 19:26–27
  4. Math 27:46 na Mk 15:34
  5. Yoh 19:28
  6. Yoh 19:30
  7. Lk 23:46

Tanbihi

Marejeo

  • The Reader's Encyclopedia, Second Edition 1965, publisher Thomas Y. Crowell Co., New York, editions 1948, 1955, pp. 917–18

Viungo vya nje

Maneno Saba  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maneno saba kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

InjiliMsalaba wa YesuNneUkristoYesu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ViwakilishiMohammed Gulam DewjiMnyamaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaTambikoUlimwenguWayahudiKilimoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaKiimboFananiVitendawiliFasihi andishiTungo kishaziSinagogiDalufnin (kundinyota)MusaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaFutiLiverpool F.C.Mwanza (mji)Jay MelodyKongoshoMadhara ya kuvuta sigaraSimba (kundinyota)Wilaya ya ArushaMbogaEthiopiaTanganyika (ziwa)Aunt EzekielMfumo katika sokaWema SepetuMtandao wa kijamiiSimuMavaziSwalaMethaliGoba (Ubungo)Athari za muda mrefu za pombeMeliRushwaWaziriUturukiWajitaMajeshi ya Ulinzi ya KenyaMuda sanifu wa duniaMwaniMandhariSamakiUhakiki wa fasihi simuliziMimba za utotoniHaki za watotoMatumizi ya LughaSaratani ya mlango wa kizaziMzabibuFigoTume ya Taifa ya UchaguziMkoa wa RuvumaHoma ya matumboTafsiriKataTumbakuUlumbiMajiPasakaIntanetiKimeng'enyaLugha ya taifaUnyagoKichochoNabii EliyaMisimu (lugha)InstagramNdoa🡆 More