Wakfu

Wakfu (kwa Kiarabu وقف‎‎) inamaanisha hali ya kutengwa na matumizi mengine, hasa kwa ajili ya matumizi ya kidini au manufaa kwa umma tu.

Wakfu
Mtakatifu Genevieve akiwekwa wakfu na askofu: mchoro wa mwaka 1821 (Ste. Genevieve, Missouri).

Watu, vitu na mahali wanaweza kuwekwa wakfu kwa namna mbalimbali.

Maana ya Kisheria

Kwa maana ya kisheria wakfu (kwa Kiingereza foundation au charitable trust) ni taasisi au shirika lililopokea mali au pesa kwa matumizi ya manufaa kwa umma.

Sheria za Kenya zinaruhusu mali kuwekwa wakfu kwa manufaa ya dini, elimu, utamaduni, sayansi, jamii, michezo au usaidizi wa watu maskini.

Mali ya taasisi ya aina hiyo imo mikononi mwa wadhamini (ing. trustees) wenye wajibu wa kutunza mali ya wakfu kwa madhumuni yaliyoelezwa katika hati ya taasisi na kuandikishwa katika ofisi ya serikali.

Kimsingi taasisi ya wakfu ilipokea mali ambayo ni msingi wa kazi yake, kwa mfano ardhi, majengo, hisa au pesa. Kuna pia mifano ya taasisi za wakfu zisizo na rasilmali zikitafuta zaidi michango ya wafadhili kwa ajili ya kazi yao kulingana na madhumuni.

Ukristo

Katika Ukristo, watu wanaweza kuwekwa wakfu, hasa kwa njia ya sakramenti zisizoweza kurudiwa kwa sababu zinatia alama isiyofutika milele (yaani ubatizo, na kwa madhehebu mengine pia kipaimara na daraja takatifu), lakini pia kwa kushika maisha ya pekee katika useja mtakatifu (kwa kawaida pamoja na ufukara na utiifu).

Vitu na mahali vinaweza kuwekwa wakfu hasa kwa ajili ya ibada, k.mf. vyombo vya ibada, mavazi ya ibada na kanisa.

Uislamu

Katika Uislamu wakfu ni mali iliyotengwa kwa kusudi la kidini. Mifano ya wakfu ni kutoa kiwanja kwa kujenga msikiti, shamba au nyumba ikiwa mapato yake yatagharamia misikiti, madrasa, hospitali, watu maskini au wanafunzi, au pia kutoa pesa kwa makusudi haya.

Tanbihi

Viungo vya nje

Wakfu  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakfu kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Wakfu Maana ya KisheriaWakfu UkristoWakfu UislamuWakfu TanbihiWakfu Viungo vya njeWakfuDiniKiarabuUmma

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Aina ya damuSilabiWimboUislamuLuis MiquissoneAbby ChamsTungo kiraiBaruaAlasiriDhahabuAshokaTungoMkoa wa KataviHekaya za AbunuwasiKiumbehaiHistoriaMichael JacksonUgonjwa wa kupoozaMkoa wa ArushaTupac ShakurBunge la TanzaniaMkoa wa Dar es SalaamKitenzi kishirikishiUbongoDr. Ellie V.DMishipa ya damuWairaqwUwanja wa Taifa (Tanzania)Jumuiya ya MadolaMafuta ya wakatekumeniPesaFonolojiaRamadan (mwezi)Tarehe za maisha ya YesuUchimbaji wa madini nchini TanzaniaKifo cha YesuMauaji ya kimbari ya RwandaMungu ibariki AfrikaUlemavuUtamaduni wa KitanzaniaMivighaKiraiZana za kilimoNafsiKukiFid QHaikuWasukumaHassan bin OmariTajikistanKamusi elezoNdege (mnyama)MaishaTashihisiWameru (Tanzania)Nuru InyangeteMichezo ya watotoKiingerezaViunganishiHadithiJohn MagufuliMapigo yasiyo ya kawaida ya moyoVidonda vya tumboKorea KusiniVita vya KageraKiambishi awaliUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiBikiraNeemaIntanetiKylian MbappéBukayo Saka🡆 More