Bratislava

Bratislava ni mji mkuu wa Slovakia wenye wakazi 450,000.

Majina mengine ya kihistoria ya mji huu yalikuwa Pressburg (kwa Kijerumani) au Pozsony (kwa Kihungaria). Uko kando Ya mto Danubi.

Bratislava
Mandhari ya Bratislava
Bratislava
Bendera ya Bratislava
Bratislava
Mahali pa Bratislava nchini Slovakia

Ishara ya mji ni boma la Bratislava lililosimama tangu karne za kati.

Jiografia

Bratislava iko kwenye mpaka wa kusini-magharibi ya Slovakia karibu na Austria na Hungaria, si mbali na mpaka wa Ucheki.

Bratislava 
Uwanja Mkuu.

Historia

Eneo la mji lilikaliwa tangu milenia nyingi. Kiini cha mji wa leo kilikuwa boma la Bratislava lililojulikana tangu mwaka 805 BK.

Utawala wa eneo la mji ulibadilika mara kadhaa, lakini tangu mwaka 907 mji ulikuwa sehemu ya ufalme wa Hungaria hadi mwaka 1918. Kati ya miaka 1524 na 1830 ulikuwa mji mkuu wa Hungaria. Wakazi wake walikuwa hasa Wajerumani na Wahungaria pamoja na Waslovakia.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia eneo la mji liliingizwa katika nchi mpya ya Chekoslovakia, na jina likabadilishwa kuwa Bratislava. Mji ukawa mji mkuu wa sehemu ya Kislovakia ya nchi.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na tena baada ya kugawanyika kwa Chekoslovakia mwaka 1993 Bratislava imekuwa mji mkuu wa Slovakia.

Bratislava 
Barabara kuu ya kitaifa D1 kando ya Bratislava

Biashara

Bratislava ni mji wa viwanda: kuna viwanda vya motokaa, kemia, mashine na vifaa vya stima.

Usafiri

Mji ni njiapanda ya barabara kuu, pia ya reli. Usafiri wa majini hutumia bandari ya Bratislava kwenye mto Danubi. Kuna pia Uwanja wa ndege wa kimataifa.

Usafiri wa mjini ni kwa mabasi, reli za barabarani na mabasi ya umeme.

Picha za Bratislava

Viungo vya nje

Bratislava 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Bratislava  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bratislava kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Bratislava JiografiaBratislava HistoriaBratislava BiasharaBratislava UsafiriBratislava Picha za Bratislava Viungo vya njeBratislavaKihungariaKijerumaniMji mkuuMto DanubiSlovakia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UpendoSintaksiSoko la watumwaMuhammadNenoHisiaMohamed HusseinTwigaMaghaniPhilip Isdor MpangoUnyevuangaUzazi wa mpangoMkopo (fedha)Ufahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi andishiMnururishoOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaMobutu Sese SekoWilaya ya KinondoniMisemoNgano (hadithi)Nomino za dhahaniaNguzo tano za UislamuMkoa wa ManyaraIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)MbooHalmashauriHistoria ya KenyaMbeziRayvannyMohamed HusseiniKinyereziAfro-Shirazi PartyTetemeko la ardhiKishazi tegemeziUaminifuNileAfrika KusiniMmeaOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaMkoa wa DodomaKarafuuWilaya ya TemekeWilaya ya NyamaganaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaTambikoMbuBarua rasmiAina za ufahamuAntibiotikiNomino za pekeeDemokrasiaNg'ombeBurundiMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaSeli za damuShairiMahindiAdolf HitlerAbedi Amani KarumeMfupaMofolojiaMaigizoOrodha ya nchi kufuatana na wakaziUandishiTamthiliaSanaaNgeliRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMoscowHaki🡆 More