Boma

Boma ni sehemu au hasa jengo lililoviringishwa kwa vizuizi ili watu wasipite kirahisi kwa shabaha ya kujitetea dhidi ya maadui.

Maana ya neno hili linaweza kuwa karibu na "ngome" lakini linaweza kutaja pia sehemu yoyote iliyoimarishwa kwa mfano "boma la ng´ombe" kama sehemu iliyoviringishwa kwa miiba kwa kutunza mifugo wakati wa usiku.

Boma
Boma huko Katanga kwenye karne ya 19
Boma
Old Boma Building, Blantyre
Boma
Boma la Wajerumani pale Saadani, mnamo 1912

Historia

Krapf (1882) alitoa ufafanuzi "Boma, a palisade or stockade serving as a kind of fortification to towns and villages. The boma may consist of stones or of poles, or of an impenetrable thicket of thorns.".

Wakati wa ukoloni wa Wajerumani walieneza utawala wao kwa kujenga nyumba imara zilizofaa kwa kujitetea yaani maboma. Kutokana na vyanzo hivi "boma" liliendelea kutaja makao ya maafisa wa kiutawala na kwa maana hiyo hadi leo hata majengo ya wakuu wa wilaya mara nyingi huitwa "boma". Kwa njia hii "boma" au "bomani" imekuwa sehemu ya majina ya maeneo na kata mbalimbali katika Tanzania.

Kuna pia matumizi ya neno "boma" inayoweza kufanana na "kaya" kwa maana ya makazi ya familia. Katika vitabu vya watalii nyumba za Wamasai wakati mwingine huitwa pia "boma" lakini hii si lugha ya wenyewe.

Huko Kenya Ngome ya Yesu hutwa pia "Boma la Yesu".

Marejeo

Tags:

Ngome

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ufahamu wa uwezo wa kushika mimbaMalariaMauaji ya kimbari ya RwandaKaswendeAlama ya uakifishajiUandishi wa ripotiJimbo Katoliki la GeitaAdolf HitlerMatendo ya MitumeDemokrasiaTungo kiraiHerufiMtakatifu PauloNomino za wingiAlasiriRuge MutahabaKumaBustani ya wanyamaClatous ChamaMbwaOrodha ya viongoziIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MitaaWasabatoMarekaniChelsea F.C.Mgawanyo wa AfrikaTambikoTamathali za semiMkoa wa ShinyangaLigi Kuu Tanzania BaraNchiMisaleMitume na Manabii katika UislamuVielezi vya namna au jinsiWahaKifua kikuuMwanga wa juaTungo kishaziMsituMiundo ya mashairiMziziMaambukizi nyemeleziMadhara ya mabadiliko ya hali ya hewaHistoriaXKitenzi kishirikishiUsawa (hisabati)FasihiKishazi huruKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniBahari ya HindiBongo FlavaAfrika Mashariki 1800-1845GhanaUhakiki wa fasihi simuliziMusaSilabiKibodiKinyongaViwakilishi vya kuoneshaWanu Hafidh AmeirBarabara16KitufeMkoa wa NjombeVielezi vya namnaUenezi wa KiswahiliMafurikoNomino za kawaidaHistoria ya TanzaniaYouTubeOksijeniGeorge Washington🡆 More