V

V ni herufi ya 22 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa.

Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

Asili yake ni ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

Maana za V

Historia ya alama V

Historia ya V ina asili za pamoja na U, W, Y na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.

V  V  V  V  V 
Kisemiti asilia:
picha ya kingoe
Kifinisia:
Waw
Kigiriki:
ipsilon
Kietruski:
V
Kilatini:
V

Alama ya V kiasili ilimaanisha sauti za "v" na "u" kwa pamoja katika Kilatini cha Kale. Iliandikwa kama V na matamshi yake yalitegemea nafasi yake katika neno pia lahaja mbalimbali. Tofauti ilikubwaliwa tu wakati wa Kilatini Kipya katika karne ya 16 ambako wataalamu wa Ulaya walikubaliana kutumia alama yenye kona V kwa sauti ya konsonanti na alama isiyo na kona U kwa vokali.

Waroma walipokea alama hii kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma (tazama F) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "u" lakini pia "v" kama ilikuwa mwanzoni wa neno. Waroma walipokea vile.

Tags:

Alfabeti ya KigirikiAlfabeti ya KilatiniIpsilonKiswahili

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WamasaiUnyevuangaManchester CityMafumbo (semi)LahajaKinjikitile NgwaleZabibuMlima wa MezaLongitudoUzazi wa mpangoUkoloniFasihi andishiTawahudiOrodha ya Marais wa KenyaAli Hassan MwinyiKina (fasihi)Chelsea F.C.DuniaMkoa wa RuvumaChakulaNileTashihisiVidonda vya tumboUandishiMohammed Gulam DewjiAzam F.C.Muungano wa Madola ya AfrikaSemiUturukiKitenzi kikuu kisaidiziHekimaMsamiatiOrodha ya Watakatifu wa AfrikaMfumo wa mzunguko wa damuMisemoKiburiKinyongaMnyamaMichezo ya watotoEe Mungu Nguvu YetuWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiSerikaliAkiliJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaHuduma ya kwanzaMoses KulolaMfupaHistoria ya uandishi wa QuraniWilayaWasukumaMkopo (fedha)MilaTamthiliaKalenda ya KiislamuNdoa katika UislamuMwanamkeMusaNetiboliLahaja za KiswahiliNambaKanga (ndege)WanyaturuMkoa wa KageraAgano JipyaViwakilishi vya pekeeFasihiMkoa wa PwaniClatous ChamaKigogo (Kinondoni)🡆 More