Yosia

Yosia (kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake aliyeponywa na YHWH au aliyetegemezwa na Yah; kwa Kigiriki: Ιωσιας; kwa Kilatini: Josias; 649 KK – 609 KK) alikuwa mfalme wa 16 wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika wakati huo, kwa mchango wake pia.

Yosia
Mfalme Yosia akisomewa sheria za Mungu zilizopatikana hekaluni.

Hasa alitumia nguvu zake zote kutekeleza agizo la gombo lililopatikana mwaka 622 KK likidai sadaka zote zitolewe katika hekalu la Yerusalemu tu, kadiri ya msimamo wa Kumbukumbu la Torati: "Mungu mmoja, hekalu moja".

Ndiyo maana Biblia inamsifu kwa namna ya pekee pamoja na Hezekia kati ya wafalme wote wa Israeli na Yuda, mbali na Daudi aliyebaki kielelezo cha kudumu cha mtawala aliyempendeza Mungu.

Familia

Mwana wa mfalme Amon na Jedidah, Yosia alirithi utawala akiwa mtoto wa miaka 8 tu, kutokana na uuaji wa baba yake, akatawala miaka 31, kuanzia 641/640 KK hadi 610 KK/609 KK.

Anatajwa pia katika Injili ya Mathayo (1:10-11) kati ya mababu wa Yesu.

Lakini nje ya Biblia hatajwi popote.

Babu yake, Manase anatajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kwa jinsi alivyoelekeza raia zake kuacha ibada ya Mungu mmoja ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu, kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia.

Yosia alizaa watoto wa kiume wanne: Yohane, Eliakimu, Matania na Shalumu.

Kwanza Shalumu alimrithi Yosia kwa jina la Yehoahazi. lakini baada ya miezi miatu tu nafasi yake ilishikwa na Eliakimu kwa jina la Yehoyakimu, halafu na mtoto wa huyo, Yekonia; hatimaye alitawala Matania kwa jina la Sedekia. Huyo akawa mfalme wa mwisho wa Yuda kwa kushindwa na Babuloni aliyoisaliti, akapelekwa uhamishoni huko pamoja na Wayahudi wengi mwaka 586 KK.

Urekebisho

Yosia 
Ua wa ndani wa Hekalu la Solomoni.

Kwa miaka 13 tu (622 - 609 K.K.) Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya Waisraeli wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mwenyezi Mungu sadaka nje ya hekalu la Yerusalemu.

Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha nabii Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini Yosia alipokufa vitani kabla ya wakati mambo yakaharibika haraka sana, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na juhudi zake binafsi, mbali ya kuungwa mkono na watu wachache kama nabii Yeremia.

Tanbihi

Marejeo

  • The Bible Unearthed: Archaeology's New Vision of Ancient Israel and the Origin of Its Sacred Texts for the possible role of Josiah in creation of the Bible.
  • Hertz J.H. (1936) The Pentateuch and Haftoras. Deuteronomy. Oxford University Press, London.
  • Friedman, R. (1987) Who wrote the Bible? New York: Summit Books

Viungo vya nje

Yosia  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Yosia FamiliaYosia UrekebishoYosia TanbihiYosia MarejeoYosia Viungo vya njeYosia609 KK641 KK649 KKDiniIsraeliKiebraniaKigirikiKilatiniMfalmeToratiUfalme wa YudaUrekebishoYHWHYahweh

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

HadhiraNyaniJiniNeemaMajina ya Yesu katika Agano JipyaKiunguliaAlama ya uakifishajiOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMkoa wa MorogoroBaruaMashariki ya KatiNgonjeraMafua ya kawaidaMisimu (lugha)Vivumishi vya sifaMnururishoMongoliaBahari ya HindiIsaAdolf HitlerMkoa wa ArushaKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaUbaleheZakaAngahewaMkoa wa ManyaraOrodha ya miji ya Afrika KusiniKoreshi MkuuAli Hassan MwinyiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaBarabaraFigoAbby ChamsNguruweUfugaji wa kukuMsukuleNdoa katika UislamuChama cha MapinduziVielezi vya namnaMapambano kati ya Israeli na PalestinaInjili ya YohaneWiktionaryOrodha ya milima mirefu dunianiSabatoZama za ChumaMafarisayoWilaya za TanzaniaPesaNairobiSoko la watumwaDhambiElimuMaumivu ya kiunoKishazi tegemeziMkoa wa MtwaraOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniKifo cha YesuMbeguKuhani mkuuNdege (mnyama)Muda sanifu wa duniaMmeaNyati wa AfrikaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaKrismasiMji mkuuTaswira katika fasihiMohamed HusseinVivumishi vya pekeeJogooUtenzi wa inkishafiNgamiaJumamosi kuuKairo🡆 More