Sanaa Ya Mapigano

Sanaa za mapigano (kwa Kiingereza martial arts, art of fighting) ni jina la jumla kwa namna za kupigana zinazofuata mitindo na kanuni fulani.

Sanaa Ya Mapigano
Mchoro wa ukutani kuhusu wrestling katika kaburi huko Beni Hasan.

Asili ya sanaa za mapigano

Sanaa za mapigano zilitokea katika jamii nyingi duniani pale ambapo watu walipaswa kupigana kati yao. Hapo wapiganaji wenye uwezo walianza kuwafundisha wengine namna ya kushika fimbo, upanga, upinde na silaha za kila aina, namna ya kulenga, namna ya kuepukana na shambulio na namna gani kutumia mwili katika hali ya mapigano.

Mara nyingi mafundisho haya yalikuwa pamoja na mafundisho ya kiroho kuhusu umuhimu na mbinu za kujiandaa kwa mapigano, namna za kutawala fikra na mwili hadi namna za kupumua.

Katika tamaduni zilizojua maandishi kuna vitabu vilivyohifadhiwa tangu miaka elfu kadha vilivyotungwa kama mwongozo katika sanaa hizi.

Namna mbalimbali za sanaa hizi pamoja na kanuni zake zilisambaa duniani kutoka nchi na tamaduni za asili, kwa mfano mchezo wa ngumi kutoka Uingereza au judo na karate kutoka Japani. Hasa sanaa za mapigano kutoka Asia zinakuja pamoja na mafundisho ya kifalsafa.

Watu hujifunza sanaa za mapigano kwa shabaha ya kujitetea, matumizi katika jeshi au polisi, kwa maendeleo ya roho na pia kama namna ya michezo.

Sanaa za mapigano na michezo ya mapigano

Kwenye ngazi ya mafunzo na mazoezi sanaa hizi mara nyingi hutekelezwa sawa na michezo ya mapigano.

Hata ikifanana kwa namna nyingi shabaha ni tofauti. Katika michezo ya mapigano wanamichezo wanalenga kumshinda mpinzani katika mechi mbele ya watazamaji na chini ya usimamizi wa refa kufuatana na kanuni zinazokubalika kikamilifu.

Kiasili sanaa za mapigano zililenga mara nyingi kuandaa wapiganaji kwa vita. Leo hii kuna shabaha tofautitofauti pamoja na kuboresha uwezo wa kutumia mitindo mbalimbali, kujifunza nidhamu, kujiboresha kiroho hadi kujiandaa kwa mapigano halisi katika nafasi ya kujihami au matumizi ya kijeshi. Kwa hiyo mara nyingi si lazima kulenga ushindi dhidi ya mpinzani.

Aina za sanaa za mapigano

Mapigano bila silaha

Mapigano bila silaha hutumia mbinu za kupiga, za kushika na za kuunganisha zote mbili. Mbinu za kupiga

Mbinu za kushika Kumtupa chini mpinzani: Hapkido, Judo, Sumo, Wrestling Kumtupa na kumshika chini mpinzani: Hapkido, Jujutsu, jiu-jitsu ya Brazil, Sambo

Sanaa za kutumia silaha

Kwenye historia ya vita katika sehemu na tamaduni nyingi za dunia kabla ya kupatikana kwa silaha za moto kuna silaha mbalimbali zilizobuniwa na kupendelewa zaidi.

Mifumo ya kimsingi ya kupigana inafundishwa kwa matumizi ya mafimbo. Mfano ni kendo ya Kijapani iliyoanzishwa kama maandalizi ya kutumia upanga au kitara; kuna mifano pia katika sehemu nyingine za dunia.

Matumizi hodari ya silaha kama upanga au kitara yalihitaji mazoezi mengi yaliyofundishwa katika tamaduni zote, hasa kama silaha hizi zilikuwa silaha za watu wenye cheo.

Matumizi ya uta au upinde yalihitaji pia uzoefu mwingi. Hasa katika sanaa ya mapigano ya Asia kuna mazoezi mengi yaliyounganishwa na falsafa ya Kibuddha.

Viungo vya Nje

Sanaa Ya Mapigano  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sanaa ya mapigano kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Sanaa Ya Mapigano Asili ya sanaa za mapiganoSanaa Ya Mapigano Sanaa za mapigano na michezo ya mapiganoSanaa Ya Mapigano Aina za sanaa za mapiganoSanaa Ya Mapigano Viungo vya NjeSanaa Ya MapiganoKiingereza

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Chombo cha usafiri kwenye majiBunge la Afrika MasharikiChatuTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaFaraja KottaUnyanyasaji wa kijinsiaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuUwanja wa Taifa (Tanzania)Saidi NtibazonkizaKitenzi kikuu kisaidiziDhima ya fasihi katika maishaUkooPasifikiUtenzi wa inkishafiKalenda ya KiyahudiChatGPTUrusiZuchuDhambiUtamaduni wa KitanzaniaMtaalaKinembe (anatomia)John Raphael BoccoSilabiNetiboliAina ya damuFisiUandishiMkoa wa KageraUmoja wa MataifaOrodha ya MiakaViwakilishiWazaramoArusha (mji)Kalenda ya KiislamuMapigo yasiyo ya kawaida ya moyoSanaaWiki FoundationWallah bin WallahSeli nyeupe za damuOrodha ya majimbo ya MarekaniSamia Suluhu HassanImaniMongoliaHafidh AmeirMkoa wa MorogoroMkoa wa IringaAlhamisi kuuKiunguliaMbaraka MwinsheheNambaBrazilNamba za simu TanzaniaHarmonizeYoweri Kaguta MuseveniKiwakilishi nafsiPalestinaArudhiChama cha MapinduziWaheheNdiziMekatilili Wa MenzaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniNdovuZama za ChumaUhifadhi wa fasihi simuliziWapareMombasaMike TysonHoma ya iniTungo kishaziZana za kilimoSiku tatu kuu za PasakaPentekosteMuda sanifu wa duniaWaha🡆 More