Neptuni ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Np. Namba atomia ni 93 na uzani atomia ni 237. Jina limechaguliwa kutokana na sayari Neptun.
Neptuni (neptunium) | |
---|---|
Atomi ya Neptuni | |
Jina la Elementi | Neptuni (neptunium) |
Alama | Np |
Namba atomia | 93 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 237 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 22, 9, 2 |
Densiti | 20.25 g·cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 910 K (637 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4273 K (4000 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 4 · 10-17 % |
Hali maada | mango |
Neptuni ni metali na elementi ya tamburania. Kwa sababu hii haipatikani duniani kiasili isipokuwa kwa kiwango kidogo sana pamoja na plutoni ndani ya mawe ya mtapo wa urani. Inatokea katika tanuri nyuklia.
Ikiwa elementi tamburania muda wa nusumaisha si mrefu sana. Isotopi ya 237Np ina nusumaisha ya miaka milioni mbili. Lakini isotopi ya 235Np ina nusumaisha ya siku 396 tu.
Rangi ya Neptuni ni ya kifedha. Ina unururifu hivyo pamoja na muda wake wa nusumaisha yafaa kwa matumizi ya mabomu ya kinyuklia.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Neptuni (elementi) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Neptuni (elementi) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Neptuni (elementi), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.