Skeli Ya Ugumu Ya Mohs

Skeli ya ugumu ya Mohs (skeli ya Mohs) ni skeli ya kupima ugumu wa madini iliyobuniwa na Friedrich Mohs, mtaalamu wa madini kutoka Ujerumani.

Mohs alibuni skeli yake inayofafanua ugumu wa madini ikilinganisha jinsi madini ya aina moja yanavyoweza kukwaruza mengine.

An example of the Mohs scale
Skeli ya Mohs, iliyopewa jina la Friedrich Mohs.

Miamba huundwa na madini ya aina moja au zaidi. Kulingana na skeli ya Mohs, ulanga ni laini kabisa: inaweza kukwaruzwa na madini mengine yote. Jasi ni ngumu zaidi: inaweza kukwaruza ulanga lakini si kalsiti (kabonati ya kalisi, calcite), ambayo ni ngumu zaidi. Madini magumu kabisa ni almasi (diamond) ambayo haiwezi kukwaruzwa na kitu kingine chochote.

Skeli ya Mohs inatumia madini kumi kwa kulinganisha ugumu. Hayo ni ulanga, jasi, kalsiti, fluoriti, apatiti, felspa, kwazi, topazi, korundi (mfano rubi), hatimaye almasi.

Skeli ya Mohs iliundwa miaka mingi iliyopita, hivyo si kamili kabisa, lakini wanajiolojia bado wanaitumia kwa sababu ni rahisi kutumika, hasa kwa utafiti nje ya maabara. Ndani ya maabara kuna pia vifaa vinavyoruhusu kupima ugumu halisi.

Ugumu wa Mohs Madini Fomula ya kikemia Ugumu halisi Picha
1 Ulanga Mg 3 Si 4 O 10 (OH) 2 1 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
2 Jasi ZABURI 4 · 2H 2 O 3 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
3 Kalsiti CaCO 3 9 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
4 Fluoriti CaF 2 21 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
5 Apatiti Ca 5 (PO 4 ) 3 (OH -, Cl -, F - ) 48 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
6 Felspa KAlSi 3 O 8 72 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
7 Kwazi SiO 2 100 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
8 Topazi Al 2 SiO 4 (OH -, F - ) 2 200 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
9 Korundi Al 2 O 3 400 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs
10 Almasi C 1600 Skeli Ya Ugumu Ya Mohs


Marejeo

Tovuti nyingine

Skeli Ya Ugumu Ya Mohs  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Skeli ya ugumu ya Mohs kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

MadiniMtaalamuSkeliUjerumani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MvuaHomoniMichezo ya jukwaaniOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMnyamaSalaSarufiUtoaji mimbaMuungano wa Madola ya AfrikaSimba S.C.Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Diamond PlatnumzWilaya za TanzaniaWanyamboMkoa wa SingidaMnara wa BabeliMfumo wa upumuajiChawaPonografiaOrodha ya vitabu vya BibliaKiingerezaWingu (mtandao)Jakaya KikweteAndalio la somoYordaniMkoa wa TangaUkoloniMisimu (lugha)SilabiTafsiriWakingaKitabu cha Yoshua bin SiraWaheheMafurikoKambaleElimu ya watu wazimaAfyaMnazi (mti)Ee Mungu Nguvu YetuKishazi tegemeziWaluoMbeya (mji)Nikki wa PiliUkweliSentensiKunguruMapinduzi ya ZanzibarDhima ya fasihi katika maishaMsichanaUnyanyasaji wa kijinsiaSanaaUzalendoBendera ya KenyaWanyama wa nyumbaniNetiboliOrodha ya Marais wa ZanzibarChristopher MtikilaNduniStephane Aziz KiMamelodi Sundowns F.C.BenderaMasafa ya mawimbiKinembe (anatomia)Awilo LongombaParachichiUwanja wa Taifa (Tanzania)Kilimanjaro (volkeno)Bikira MariaMkunduVipaji vya Roho MtakatifuMitume wa YesuMafua ya kawaidaDamuUundaji wa manenoKumaUfugaji wa kuku🡆 More