Sokwe mkubwa au sokwe peke yake ni jina la binadamu na nyani wakubwa wa familiaHominidae wanaofanana sana na binadamu. Tofauti na nyani wengine ni kuwepo kwa mkia; karibu nyani wote huwa na mkia lakini masokwe wakubwa hawana kabisa. Binadamu (Homo) anahesabiwa pia kama jenasi yenye spishi moja katika familia hii.
Masokwe wasiokuwa wanadamu wanaishi katika maeneo ya tropiki ya Afrika (masokwe mtu na ngagi) na Asia (orangutanu). Wote ni wakazi wa misitu ila tu masokwe mtu wanaoingia pia kwenye mbuga au savana. Wanadamu wanaishi duniani kote kwa kubadili mazingira yao, kuvaa nguo na kujenga majumba yanayowalinda kutoka joto kali ama baridi.
Ngagi Mashariki au Gorila Mashariki, Gorilla beringei (Eastern gorilla)
Ngagi-milima, Gorilla b. beringei (Mountain gorilla: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda)
Ngagi wa Uwanda wa Chini Mashariki, Gorilla b. graueri (Eastern lowland gorilla: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo)
Ngagi Magharibi au Gorila Magharibi, Gorilla gorilla (Western gorilla)
Ngagi wa Nijeria, Gorilla g. diehli (Cross River gorilla: Nijeria na Kameruni)
Ngagi wa Uwanda wa Chini Magharibi, Gorilla g. gorilla (Western lowland gorilla: Kameruni, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gaboni, Ginekweta, Kongo, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Angola)
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sokwe (Hominidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Sokwe (Hominidae), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses. ®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.