Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani.
Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake.
Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.
Lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.
Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili iko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.
Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.
Kuna pia matatizo ya malambo:
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Lambo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.